Kopi ya matokeo kila kituo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kopi ya matokeo kila kituo

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mdanganywa, Oct 18, 2010.

 1. M

  Mdanganywa JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 542
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Tuliwa tumebaki na siku 13 tu kuingia kituoni ni wazi kwamba pressure ya kulinda kura inaongezeka kila kukicha.

  Maoni yangu ni kwamba kila chama kina wakala wake kusimamia uchaguzi. Baada ya kuhesabu kura na kila mmoja akajulikana amepata ngapi naamini nakala hupelekwa NEC na mawakala wanatoka kituoni na nakala/kopi ya matokeo ya ushindi zikiwa na sahihi zao.

  Kama ni hivyo basi safari hii tusidanganyike. Tutumie mbinu ileile ya mitandao ambayo imefanikiwa kufumua siri nyingi za ufisadi ambazo nyaraka zake zenye sahihi zimetembea humuhumu mitandaoni.

  Kinachotakiwa ni nini? Wakala anatakiwa aipeleke kopi yake kwenye chama chake. Lakini chama pia kitoe ushirikiano kutuma kopi zile kwenye mitandao kwa njia ya kuzi-scan kama zilivyo-scan-iwa zile nyaraka.

  Nasema hivi kwa sababu itakuwa ni nafasi nzuri kuyasoma matokeo bila kubabaishana na bila kusubiri kupigiwa hesabu za kujumlisha na Tume ya uchaguzi.

  Tume ikishaona kopi za matokeo zinatembea mitandaoni na tunahesabu wenyewe haitakuwa na wataanzia wapi kutangaza vinginevyo?

  Huwa tunapenda kukwamisha hoja kwa kusema jambo fulani vijijini haliwezekani kama hili. Siku hizi si lazima ufanye scan kama miaka ile. Hata kupiga picha yaani snapshot inaweza kusidia kama font ya maandishi si kubwa kiasi hicho na kisha picha ikatumwa kwa mtu atakayeweza kuifikisha mitandaoni.

  Awezaye kuboresha wazo hili ruksa maana ni wazo limekuja ghafla kichwani kama ambavyo nafikiri wengi wetu sasa hivi wazo la kuibiwa kura au kuchakachuliwa matokeo ni kubwa kuliko chochote.
   
 2. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hilo ni wazo zuri sana.Mi nalia na suala la mawakala,mbinu ya kwanza ya ccm ni kupandikiza mawakala kwa wapinzani halafu wanasign matokeo ya uongo.Kama wakipatikana mawakala waaminifu basi ni jambo muhimu sana,naamini hili suala lilishaanza kufanyiwa kazi kwa muda mrefu sana.
   
 3. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hilo nalo neno mkuu!
  Vyama mbadala(ambavyo ndivyo hasa victims wa kuibiwa kura),hebu tupitie tena,tujiridhishe kuwa watu tutakaowateau kuwa mawakala si mamluki. CCM wana muda mwingi sana wa kufanya michezo michafu na ndio maana wanakosa kabisa muda wa kufanya jema lolote. Hivyo naamini kabisa kuwa wakati huu wanayo tayari kila sampuli ya wizi. Tuwe makini wana,huu muda asikubali mtu kutumwa dukani,na hakuna kupepesa ukope! It's critical! RED ALERT!!
   
 4. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Kipengere cha mawakala kwa sasa ni muafaka kikajadiliwa kwa mapana sana hum JF ili kupanuana uelewa ni vema kila siku tuwe na utaratibu wa kukumbushana mbinu mpya CCM kila siku wanajaribisha njia zao haramu na tumeshuhudia nyingi zinashindwa na leo tunasikia lori likiwa na kura limekamatwa.
   
 5. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Tunaweza kuanza na data za kawaida ambapo kila kituo kinaweza kupost matokeo hapa. Tuombe MODES watuwekee janvi jipya la matokeo ya uchaguzi ili tuweze kupost results kila kona ya Tz. Inaweza kuwa spread sheet or any format.
   
 6. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Great!!!!!! lifanyike hilo, uchaguzi wa mwaka huu ni shirikishi zaidi kila mwanachadema ashiriki kwa namna moja au nyingine.Matokeo yakizagaa kila mtandao itakuwa vigumu kuchakachuliwa, maana uchakachuaji unafanyika baada ya kura kuhesabiwa.
   
 7. kibhopile

  kibhopile JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2010
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  great idea,,
   
 8. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Kama inawezekana, hata kabla ya siku ya kura yenyewe, vyama vitoe orodha ya vituo vyote vya kupiga kura nchi nzima kwa kila Jimbo la Uchaguzi. Hii itatoa nafasi kwa watu walio sehemu mbali mbali kujitayarisha na kuamua ni maeneo yapi wanaweza ku-monitor matokeo na kuyapost kwenye board maalum ya JF au mtandao mwingine. Vyama vile vile vinatakiwa kuwa na organisation nzuri kwa kila Jimbo ili matokeo yakitangazwa kinyume viwe na ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa kura zimeibiwa. Kulalamika baada ya uchaguzi bila kuwa na ushahidi wa kitakwimu hakutasaidia kitu.
   
 9. F

  Fanfa JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hili ni wazo zuri sana. Mods hebu tuwekee hii itasaidia kuzuia mbinu chafu
   
 10. tempo_user1

  tempo_user1 Senior Member

  #10
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naunga mkono hoja!
   
 11. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,126
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo kwenye RED tusaidie. Unamaanisha lilikua limebeba kura zilizokwisha pigwa au shahada za kupigia kura?!
   
 12. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Zenye alama ya vema kwenye kiboksi chenye picha ya JK!
   
 13. Profesy

  Profesy Verified User

  #13
  Oct 19, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
 14. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono, kama JF wamejiandaa kuwa chombo kikubwa huko mbeleni, waanze na hili waanzishe Forum ya Matokeo kama ilivyo Forum ya Uchaguzi Tanzania 2010, kwenye hiyo forum kuwe na SPREAD SHEET(sticky) kama ile ya (Maoni ya urais) ambayo itatumika kupost matokeo. Member yeyote wa JF ofcourse atakapopata matokeo ya kituo chochote ata post kawaida kama tunavyofanya hivi lakini hataweza kupositi kwenye spread sheet, kama MODS au mtu yeyote atakaye kuwa assigned na Admn aki confirm matokeo hayo ni halisi toka kwenye kituo anaweza kuyajaza kwenye sticky spread sheet, sijui kama inawezekana kuwa automatic.

  Hiyo spread sheet inaweza kuwa na mfumo huu (si rasmi)
  Matokeo ya Uraisi/Ubunge

  Dar es salaam

  Jimbo ....Chama............Urais...................Ubunge
  1............A.....................xx..........................yy
  ..............B.....................xx..........................yy
  ..............C.....................xx..........................yy

  2............A.....................xx..........................yy
  ..............B.....................xx..........................yy
  ..............C.....................xx..........................yy

  3............A.....................xx..........................yy
  ..............B.....................xx..........................yy
  ..............C.....................xx..........................yy

  Mwanza

  Jimbo ....Chama............Urais...................Ubunge
  1............A.....................xx..........................yy
  ..............B.....................xx..........................yy
  ..............C.....................xx..........................yy

  2............A.....................xx..........................yy
  ..............B.....................xx..........................yy
  ..............C.....................xx..........................yy

  3............A.....................xx..........................yy
  ..............B.....................xx..........................yy
  ..............C.....................xx..........................yy

  etc.....
   
 15. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,126
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  Spreadshit yako inatoa matokeo ya jimboni ambayo ni jumla ya vituo vyote. Thread hii imeanza vizuri ikitaja uwezekano wa kila kitu kujulikana kura zake na ikibidi phocopy ya matokea yaliyo-sainiwa na mawakala wote.
  Ukiruhusu yaje kijumlajumla tujumlishiwe na Tume kama vile hatujui kujumlisha ndipo hapo tutakaporuhusu uchakachuaji.

  Kama inawezekana spreadshit ionyeshe kila kituo, wameajiandikisha wangapi, wamepiga wangapi, diwani fulani kapata ngapi nk.

  Tumeambiwa kuwa wiki moja kabla list ya majina itatoka. Basi tuanzie hapo. List ikitoka tu mimi nitakwenda kituoni kwangu siku hiyohiyo na kuwaletea idadi ya waliojiandikisha.

  Nitajitolea kutembea vituo hata vitatu na ikibidi zaidi hta vya majimbo mengine.
   
 16. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #16
  Oct 19, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Penye red hapo; tafadhali uwe unazungumzia watanzania wenye uchungu na nchi yao/wazalendo wa kweli. Kamwe haiwezekani wana-CHADEMA peke yao kuleta mageuzi na mabadiliko tunayoyahitaji kwasasa. Ni lazima wasio wana-CHADEMA washiriki. Ukifikiri kuwa wana-CHADEMA peke yao wanaweza kuleta ukombozi ni KUJIDANGANYA.

  Tuamke, tuikomboe nchi yetu kwa faida yetu na vizazi vyetu.
   
Loading...