Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 79
Habari nilizozipata nikiwa hapa Mara ni kwamba huko Tarime koo mbili zimeanza tena vita vya kugombea ardhi. Tayari damu imeanza kuwamwagika kwa watu kuchomana mikuki, mishale na kukatana mapanga. Naelekea eneo la mapambano kupata habari kamili. Kuna yoyote anayejua njia gani zitumike kuleta amani baina ya watu hawa? Inaelekea jitihada za Lowassa akiwa waziri mkuu hajizaa matunda yoyote. Wananchi wa hapa wanasema Bwana Chacha Wangwe alikwenda eneo la tukio lakini ameondoka ghafla kurudi Dar es salaam, inasemekana amekuja kuonana na Waziri Mkuu Pinda.
PM
PM