KONYAJI yamwaga vifaa vya usafi DSM;Matolori, mifagio, majembe badala ya Road Cleaning Machine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

KONYAJI yamwaga vifaa vya usafi DSM;Matolori, mifagio, majembe badala ya Road Cleaning Machine

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Nov 30, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145


  Na Mwandishi Wetu

  KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) inayozalisha pombe aina ya Konyagi, imelisaidia Jiji la Dar es Salaam vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 15, kwa ajili ya kufanyia usafi wa mazingira.

  Mkurugenzi wa TDL, David Mgwasa, alikabidhi vifaa hivyo jana kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadik Meck Sadik.

  Wakati wa hafla ya makabidhiano hayo, walikuwapo wakurugenzi wa manispaa zote tatu za Jiji la Dar es Salaam pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bakari Kingobi.


  Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na matoroli 50, kofia 60 za usalama, miwani 60 ya kuzuia vumbi, viatu jozi 60, mifagio 60, majembe 60, reki 60 na vifaa vingine.


  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mgwasa alisema kutolewa kwa vifaa hivyo ni mwendelezo wa misaada ambayo wamekuwa wakiitoa katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuisaidia jamii.


  "Mwaka huu nchi yetu inaadhimisha miaka 50 ya uhuru, lakini pia sisi TDL tunaadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa kiwanda chetu.


  "Kutokana na umuhimu wa matukio hayo, tukaona na sisi tuwe na njia zetu za kuadhimisha, kwa hiyo tukaanzisha huu utaratibu wa kufanya usafi na kwa kuanza tulianzia katika Jiji la Mwanza, ambako tulitoa vifaa vya Sh milioni 10 kisha tukaenda Arusha na kutoa vifaa vyenye thamani hiyo hiyo ya fedha.


  "Kwa kuwa utaratibu huu ni muhimu, kuanzia mwakani tutaangalia uwezekano wa kutoa vifaa hivyo katika mikoa mingi zaidi kwa sababu suala la uchafu liko kila eneo na wachafuaji wa mazingira ni sisi binadamu," alisema Mgwasa.


  Naye Mkuu wa Mkoa, alisema kitendo walichokifanya TDL ni cha kiungwana, kwa sababu wachafuaji wa mazingira ni binadamu, ingawa wanaolaumiwa ni viongozi wa Serikali, wakiwamo wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa maeneo husika.


  "Uchafu ni moja ya kero zinazowasumbua wananchi, kwa hiyo, mnapoamua kutumia faida ya biashara yenu katika kuboresha usafi wa mazingira, ni jambo la kufurahisha sana na linafaa kuigwa na taasisi nyingine.


  "Mimi natoka Mwanza, nilifurahi sana nilipoambiwa nyinyi ndiyo mmeweka ile sanamu ya samaki pale jirani ya PPF Mwanza, nikaona kumbe hawa jamaa wanaweza, kwa maana hiyo tumekubali kuwapa baadhi ya ‘round about' za hapa mjini muweze kuzitengeneza ziwe za kisasa," alisema Sadik.  JIJI LA DAR kwanini wasinunue vifaa hivi vya Usafi

  1. Linatumia Wafanyakazi wachache
  2. Ni bora na inaleta usafi murua
  3 .Ni rahisi kuliko kutumia Majembe na Matoroli
  4. Ni Salama
  5. Gharama ni rahisi


  [​IMG]

  [​IMG]
  [​IMG]

  [​IMG]
   
 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,711
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Dah!!! Kuna mambo mengine au misaada ukiaangalia imekaa kimatangazo ya kibiashara zaidi kuliko kusaidia au kuboresha
   
Loading...