Kongwa Beef kutoka NARCO sasa yaingia ofisini na nyumbani kwako

NARCO

Member
Mar 13, 2012
19
17
Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) Ltd imeanza utaratibu wa kuwasambazia wateja wake kuanzia maofisi hadi majumbani bidhaa mbalimbali za Kongwa Beef, Nyama Yenye Ubora wa Kimataifa, kutoka kwenye ranchi zake 10 ambazo zipo karibu kila pande ya nchi.Kongwa beef ni nyama “organic” yenye utamu asilia na ladha maridhawa. Ina ulaini wa kuvutia na mtawanyiko mzuri wa mafuta.Ukinunua nyama “Kongwa Beef” si-tu kwamba umepata nyama safi, salama, asilia na yenye ubora wa Ki-mataifa, lakini pia umechangia pato la taifa lako na ustawi wa nchi yetu.

Hapa nimeambatanisha na bei za baadhi ya bidhaa muhimu za “Kongwa Beef”

Bidhaa zetu Bei 1 Kg / (TSh)
Jembe (Blade) 6,500.00
Kongwa Beef (Kongwa Stew) Nyama Mchanganyiko 6,000.00
Kongwa Beef Steak 7,500.00
Beef Fillet 8,500.00
0x-Liver 7,500.00
0x-Tripe (Utumbo) 3,000.00
Ox-Tail (Mkia) 4,500.00
Ox-Head (Kichwa) 11,000.00
0x-Trotter (Kongoro) 1,500.00
Ox-Lungs (Pupu) 3,000.00


Tuko online tunasubiri kupokea email na simu yako.

Karibuni
=================================
Customer Service Desk
Kongwa Beef
National Ranching Company Ltd (NARCO)
Mavuno House, Azikiwe street
P.O. Box 9113
Dar Es Salaam
United Republic of Tanzania
Tel. +255 22 211 0393
+255 22 211 1956
Fax +255 22 211 1956
Mob. +255 766 123911
+255 655 123911
Email: customerservice@narco.co.tz
Skype: customerservice.narco
Web: www.narco.co.tz
==============================

For Quality & Affordable Beef
==============================
 
hii ni habari njema sana kwa jf. Hongera sana Ndg. Mexence Melo kwa kuja na wazo hili mpaka Kampuni ya nyama ya Taifa imeonelea ni vyema kuwa na ID hapa jamvini ni more valuable than kufungua website yao (kama ipo) kutokana na ukweli usiofichika kuwa watz wanao-access jf kwa sasa ni wengi.

lakini nawashauri NORCO walete advert hapa na walipie ili kiwezesha zaidi jf kuendelea kuwahudumia vizuri.
 
Narco,
Mimi ningependelea kununua nyama muda ninapokuwa nimetoka kazini, je ofisi/duka/bucha lenu linakuwa wazi mpaka saa ngapi?
 
hii ni habari njema sana kwa jf. Hongera sana Ndg. Mexence Melo kwa kuja na wazo hili mpaka Kampuni ya nyama ya Taifa imeonelea ni vyema kuwa na ID hapa jamvini ni more valuable than kufungua website yao (kama ipo) kutokana na ukweli usiofichika kuwa watz wanao-access jf kwa sasa ni wengi.

lakini nawashauri NORCO walete advert hapa na walipie ili kiwezesha zaidi jf kuendelea kuwahudumia vizuri.




duuuuh ! Kumbe imetushangaza wengi eee?!
Natamani mama rwakatare alisome hili tangazo,akirudi bungeni afunge mdomo wake juu ya jf !
 
Hongera narco. Kuongeza maboresho tafadhari fungua anuani twitter kwa ajili ya instant messeging.
 
mkuu...nadhani hapo nyuma nilikushauri mlete na maeneo ya huku Yaeda.....
hivi mmeshafungua branch.......?
nakuhakikishia hamtajuta......
 
Habari!
Nimekupata, tunayafanyia kazi maoni yako.Vilevile tunaweza kukuletea nyama hadi hapo ulipo endapo utachukua kg kuanzia 5. Wajulishe rafiki na jamaa zako
 
Tunashukuru kwa maoni yako. Kwa kipindi cha muda mfupi ujao, twitter yetu itakuwa hewani. Je, tukuletee kg ngapi za nyama.:smile:
 
Asante kwa maoni. Je, tukuletee kg ngapi,tunasubiri kusikia kutoka kwako.:decision:
 
Nyama yetu kweli ni tamu,na ukifanikiwa kuila hautatamani kuiacha.:smile:
 
Habari!
Nimekupata, tunayafanyia kazi maoni yako.Vilevile tunaweza kukuletea nyama hadi hapo ulipo endapo utachukua kg kuanzia 5. Wajulishe rafiki na jamaa zako

bado hamjaacha uongo?
 
mhhhh Kongwa??msije mkawa mnasindika panya mnatuuzie nyie wana?kongwa pale sijaona ng'ombe wenye nyama ya ubora wa kimataifa...!!!
 
Mimi ni mpenzi wa Figo, sijaona figo kwenye orodha yenu au kwenye bucha zenu figo hakuna? kama zipo naomba nijuwe bei yake na uzito nitakwenda mwenyewe pale kwenye duka lenu Nkrumah street.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom