Kongole sana kwa Waziri Suleiman Jafo (WOMRMM) kwa Kusajili mradi Kigoma

luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
6,325
6,864
Kama kichwa cha habari kisemavyo.

Binafsi nimevutiwa sana na uchapaji kazi wako baada ya kuhamia katika wizara ya ofisi ya makamu rais muungano na mazingira ndani ya siku takriban 60-70 tangu umetua ktk wizara iyo umefanya mambo ya tofauti sana ambayo awali hayakufanyika na watangulizi wako karibia wotee

Mosi, mjadalaa wa historia ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mdahalo ulifanyika pale dodoma ulikuwa very positive ktk kutoa elimu ya historia ya muungano huu ambao bado wengine tunauona una kasoro za kuzitolea macho kwa umakini

Lakini la pili ni kasi yako ya kutembelea miradi mbalimbali ambayo percee inagusa mazingira hapa mkuu una pita vizuri sana, awali kulijengeka nadharia kama EIA, ripoti ya tathimini ya athari ya mazingia ni kitu kinacho kwa misha maendeleo, majuzi ulifanya ziara mkoani kigoma ulitembelea miradi kadhaa lkn mradi ambao ulinigusa binafsi ni hii project ya uwekezaji katika utalii kwenye hotel ya GRAND BEACH CHALET, ni hotel nzuri lkn kwa kuwa EIA haikufanyika pale na matokeo yake yameonekana , ni majengo ya hotel kuvamiwa na maji ya ziwa Tanganyika ikisemekana ni athari ya mabadiliko ya tabia nchi kupelekwa ongezeko la maji katika fukwe za ziwa Tanganyika lakin itoshe kuamini ni matokeo ya kutokuona umuhimu wa EIA. Pale ni hasara. Tayari kwa mwekezaji .

Mhe. Waziri Jafo endapo kama utapitia UZI huu basi nikuombe ni vyema ktk kila halmashauri wawepo ma ofisa mazingira ambao wata saidia walau kusimamia hii kitu EIA maana maofisa mazingira walioko ktk halmashauri nyingi na manispaa zetu wengi wana focus ktk afya wakiamini ndio component kubwa ya mazingira ilihali mazingira ni kitu mtambuka, wakiwepo watu hawa sizani kama yatatokea tena kama haya ya GRAND BEACH CHALET hotel. Tusitegemee tu ofisi za NEMC za kanda.

====

JAFO ATOA SIKU KUMI KUSAJILI MRADI KIGOMA​

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo ametoa siku kumi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma kuhakikisha anasajili mradi wa ujenzi wa Machinjio ya kisasa ili uweze kupata cheti cha Tathmini ya Mazingira.

Akiwa katika siku ya pili ya ziara yake Mkoani Kigoma Waziri Jafo ametembelea machinjio ya Manispaa ya Kigoma na kubaini ujenzi unaendelea bila kufuata taratibu za kimazingira kwa kuwa hauna Cheti cha Tathmini ya Athari ya Mazingira.

"Naagiza mradi huu usajiliwe mapema iwezekanavyo, na lengo la kufanya hivi si kupata cheti tu bali muhimu ni kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala muhimu ya kuzingatia katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira" Jafo alisisitiza Waziri Jafo amesema endapo Manispaa ya Kigoma itashindwa kusajili mradi huo wa machinjio ya kisasa kwa kipindi tajwa atasitisha ujenzi huo.

"Hivi sasa kuna mfumo wa kusajili miradi kwa njia ya mtandao na miradi yote naiona hapa kwenye tablet yangu sasa ikifika tarehe 25/05/2021 sijaona mradi wenu nitasitisha ujenzi wenu" Jafo alisisitiza. Pia, Waziri Jafo amewataka wawekezaji kote nchini kusajili miradi yao ili iweze kukidhi vigezo vya kupatiwa cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira kinacho ainisha namna bora ya kupunguza madhara ya kimazingira yatikanayo na utekelezaji wa miradi.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha inahamasisha wawekezaji kuwekeza katika uzalishaji wa nishati mbadala ambayo ni rafiki kwa mazingira. Waziri Jafo ameyasema hayo mara baada ya kutembelea Mradi wa Nishati ya Jua na kuridhishwa na uzalishaji rafiki kwa mazingira ambao uzalisha kiasi Mega Watt 1 kwa sasa huku lengo likiwa ni kuzalisha Mega Watt 4.8 kufikia 2025.

Amesema umeme unaozalishwa kutoka katika Mini-grid ya Kigoma unafaida kubwa kimazingira kwa kuwa unapunguza matumizi ya umeme wa Mafuta ambao gharama yake ni kubwa na kupongeza Uongozi wa Mkoa wa Kigoma kwa kutumia Green Power

4%25281%2529.JPG

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akiangalia athari za Mabadiliko ya Tabianchi kutokana na kuongezeka kwa kina cha maji katika Ziwa Tanganyika. Pichani ni sehemu ya Majengo ya Hotel ya Grand Beach Chalets ambayo sehemu ya majengo hayo yamezingirwa na maji.
3%25281%2529.JPG

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akikagua Mradi wa Nishati ya jua (Ujiji solar Project) unaozalisha Mega Wat 1 kwa sasa, lengo likiwa ni kuzalisha mega watt 4.8 kufikia mwaka 2025.
2%25281%2529.JPG

Jengo la Machinjio ya Kisasa la Manispaa ya Kigoma ambalo ujenzi wake haujafuata taratibu, Waziri Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma kufuata utaratibu.
1%25281%2529.JPG

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akikagua machinjio ya kisasa ya Manispaa ya Kigoma ambayo ujenzi wake umeanza bila kufuata taratibu za kimazingira za kutosajili Mradi huo kwa ajili ya kupata Cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira. Waziri Jafo ametoa siku 10 kwa Manispaa hiyo kusajili Mradi huo Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
 
Jafo hakuna kitu pale.
Ni sifuri inayolazimisha mambo.
Jafo anapenda sana media attention, kutwa anazurura na kikundi cha waandishi wa habari wanaolipwa posho na wizara ili kuripoti ziara zake in a positive way.

Jafo na Kigwangwalla ni mapacha.
 
Safi sana Prof Jaffo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom