Kongole Samsung

Hardlife

JF-Expert Member
Apr 11, 2021
2,750
6,246
Sipo hapa kutangaza biashara. Nina TV yangu flat ya Samsung 32" nilinunua mwaka 2013 na naitumia tu chumbani. Sasa kutokana na athari za mvua hapa Dar iliingia maji mengi sana kwakuwa niliiweka karibu na dirisha na sikufunga na sikuwepo.

Asubuhi narudi nikawasha TV bila kuangalia vizuri ikagoma kuwaka. Kufuatilia maji yameingia ndani. Leo asubuhi nikatest ikawaka but haionyeshi vizuri. Baada ya hapo nikaiweka juani na nikaiwasha saa 3 usiku. TV imerudi nzima utafikiri haikupata janga lolote.

Aisee hapa ndio nimeelewa maana ya kununua kitu OG.

Maana baada ya kuweka ON tu asubuhi maana yake ingekufa kabisa.

Asante Sana SAMSUNG
 
Ushauri wa bure kama imekubali kuwaka basi fanya jitihada upeleke kwa fundi akaisafishe hiyo Tv au vinginevyo kifo chake kitakua kibaya sana.Maji huweka kutu kwenye electronics device kikubwa haikupata madhara ila hayo maji bila kwenda kusafishwa kwa dawa maalumu basi tegemea balaa kubwa ndani miezi michache ijayo.Ni ushauri tu kama vip unaweza kupotezea
 
Ukipeleka kwa fundi usicheze mbali kua nae benet mwanzomwisho mafundi janja janja nyingi asije akanyofoa spare OG akakuwekea kanyanga
 
Pole na hongera pia kaka.

Endelea kuombea watanzania wenzako nao wafunguke akili, unakuta mtu anaenda nunua tecno ya laki 3 mpaka laki 4 kisha anaacha Samsung A series ya bei hiyo hiyo.
Hahaha hapo sasa. Mimi kwakweli kununua vitu vya bei rahisi siwezi. Hata kama sina hela nitajichanga mdogomdogo mpaka nipate hata kama ni miezi 6.
Faida ya vitu OG naijua sana.
Just imagine TV ninayo miaka 9 mpaka sasa na ipo vizuri sana.
 
Ushauri wa bure kama imekubali kuwaka basi fanya jitihada upeleke kwa fundi akaisafishe hiyo Tv au vinginevyo kifo chake kitakua kibaya sana.Maji huweka kutu kwenye electronics device kikubwa haikupata madhara ila hayo maji bila kwenda kusafishwa kwa dawa maalumu basi tegemea balaa kubwa ndani miezi michache ijayo.Ni ushauri tu kama vip unaweza kupotezea
Hapo kwa kusafishwa nakubaliana na wewe.
 
Sio tu samsung
Ukiweza kupata kitu OG chenyewe kile kampuni yoyte lazima kitadumu hiyo scenario yako ipo home kuna LG 40' nayo ilipata changamoto kama hiyo yako mtoa mada maji yaliingia kupitia dirishani tena ya kushato lakini mzgo una piga kazi kama kawa na ina timiza mwaka sasa toka imepatwa na hiyo dhoruba
Nb
Haikupelekwa kwa fundi hata ila kuna jamaa kashauri ikasafishwe ndo nime fikiria ilo ni la muhimu nitalishughulikia.
 
Back
Top Bottom