Kongole kwa Wanahabari wote tukiadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari

SueIsmael

JF-Expert Member
Dec 11, 2013
932
1,280
Nawatakia wanahabari wote, ikiwemo timu nzima ya Jamii Forums, maadhimisho mema ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari. Hii ni tasnia ngumu sana na inahitaji ujasiri wa hali ya juu. Ukipewa jukumu la kutetea ukweli, ni rahisi kutengeneza maadui wengi, hata wale wanaokolewa na ukweli huo.

Tuzidi kuwakumbuka katika sala wale waliotangulia mbele za haki, wengine wakiwa wanatekeleza majukumu yao. Mola azidi kuwapa Rehema wapumzike kwa amani.

Msikate tamaa, msirudi nyuma, msiache sauti za wanyonge zipotee bure; sio jambo rahisi lakini nawatakia kazi njema majemedari wetu.

Asanteni sana kwa kujitoa kwenu.

Maxence Melo Asha D Abinallah Pascal Mayalla Roving Journalist na wengine wote. Mungu awabariki sana!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom