Kongole ATCL na Precision Air kwa kupunguza makali ya maisha kwa waajiriwa sekta ya anga kipindi hiki cha janga la Coronavirus

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,324
17,829
Kutokana na mashirika mengi ya usafiri wa anga kusitisha safari zake baada ya nchi nyingi kuzuwia kupokea wageni au kuruhusu waliopo ndani kuondoka, kumeibuka kitisho kikubwa cha watu kusitishiwa ajira au mishahara yao sekta ya usafiri wa anga.
Taasisi nyingi za binafsi zinazo jiendesha kibiashara zikitegemea faida zitashindwa kuwalipa mishara wafanyakazi wake wa kudumu na kufuta kabisa nafasi za vibarua wanaolipwa kwa juma au kila siku.

Sitaelezea hapa athari kubwa inayo enda kuambukiza sekta zingine sababu wote tunajua jinsi tunavyotegemeana kiuchumi.
Hawa wa anga wanalipia gharama za kusomesha watoto wao shule na vyuo mbalimbali, wanafanya ujenzi na kuwekeza kibiashara sekata zingine.

Kwa bahati kubwa sana wazo la Raisi wetu Mh. Magufuli kufufua shirika letu la usafiri wa anga ATCL amesaidia kupunguza makali haya, maana ndege zitafanya kazi angalau safari za ndani ya nchi.
Hii itapunguza sana ugumu wa maisha kuliko ambavyo kungekuwa hakuna ndege hizi kama hapo miaka ya kati.
Nichukue nafasi hii pia kuwapongeza Precision Air kwa kupambana kubaki sokoni na kupunguza makali ya maisha ya wanufaika wake kwenye ajira za kudumu na za muda mfupi hadi za wale wanaotoa huduma na zabuni kwa mashirika haya mawili ya ndege.

Najuwa kuna mashirika yanayofanya kazi na haya mashirika niliyotaja na pia na mashirika mengine ya kimataifa kam KLM, Emirates na mengineyo yatapunguza wafanyakazi lakini kwa vyovyote vile yatabakiza baadhi ya wafanyakazi waweze kuhudumia hizi ndege. Kam kusingukuwa na ndege hizi za ndani basi wote wangebaki nyumbani na kukosa hata nusu mshahara.

Ningependa pia kuwashauri wenye uwezo kutumia usafiri huu sababu hakuna mbanano, usafi wa hali ya juu, pia watu tumia muda mfupi kukaa pamoja safarini, huenda hii itasaidia kupunguza hatari ya maambukizi ya COVID-19.
Fikiria hatari iliyopo mbele yako kwenye usafiri mwingine pale unavyotumia masaa zaidi ya 10 kama humo ndani ya chombo kati yenu kuna watu wenye huu ugonjwa, kisha linganisha na kukaa nao pamoja chini ya saa mbili (2 hrs).

Mungu awabariki sana waliohusika kuhakikisha huduma hii inakuwepo, hapa nawazungumzia wote waliopo serikalini na huko sekta binasi kama shirika la Precision Air pamoja na mashirika mengine yenye ndogo zinazofanya chartered flights za ndani.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
 
Hapa serikali imefanya kile alicho shauri Zitto kwamba serikali isaidie sekta ya utalii kwa kuwapa pesa waweze kushikilia waajiriwa wake, lakini hapa imefanya kwa sekta nyingine na kwa mtindo mwingine ambao serikali itarudishiwa pesa yake na ATCL, itapata gawio na kodi toka ATCL.
Kizuri zaidi serikali imetoa pesa hii kipindi ambacho janga lilikuwa halijaingia na makusanyo yake yalikuwa makubwa.
Kwa kuwekeza pesa ATCL imesaidia kupunguza makali sekata ya usafiri wa anga.

Waswahili wanasema akiba haiozi na sasa tunaona akiba ya serikali kwa uwekezaji wa ATCL unaisaidia serikali sasa ktk wakati mgumu.

Nawashauri pia wawaangalie Precision Air kama kuna namna wanaweza kuwapa nguvu kiuchumi iwe ruzuku (grant) au mkopo (loan) wa mashariti nafuu au bila riba kama wenyewe Precision Air wanaona wana uhitaji huo.
 
Kicha cha habari na content vitu viwili tofauti.

Cha ajabu mtu kama wewe inawezekana kabisa una familia na watoto wanakuita mama.

Hatari sana.
Umemaliza kushauri mkuu wangu?
Huo ndio uwezo wangu wa kuandika, nitajitahidi kuboresha kadiri utakavyo zidi kunikosoa.

Sitakujibu matusi wala kejeli, kwa hivyo ongeza matusi tu ufurahi.
Ahsante kwa maoni yako.
 
Kutokana na mashirika mengi ya usafiri wa anga kusitisha safari zake baada ya nchi nyingi kuzuwia kupokea wageni au kuruhusu waliopo ndani kuondoka, kumeibuka kitisho kikubwa cha watu kusitishiwa ajira au mishahara yao sekta ya usafiri wa anga.
Taasisi nyingi za binafsi zinazo jiendesha kibiashara zikitegemea faida zitashindwa kuwalipa mishara wafanyakazi wake wa kudumu na kufuta kabisa nafasi za vibarua wanaolipwa kwa juma au kila siku.

Sitaelezea hapa athari kubwa inayo enda kuambukiza sekta zingine sababu wote tunajua jinsi tunavyotegemeana kiuchumi.
Hawa wa anga wanalipia gharama za kusomesha watoto wao shule na vyuo mbalimbali, wanafanya ujenzi na kuwekeza kibiashara sekata zingine.

Kwa bahati kubwa sana wazo la Raisi wetu Mh. Magufuli kufufua shirika letu la usafiri wa anga ATCL amesaidia kupunguza makali haya, maana ndege zitafanya kazi angalau safari za ndani ya nchi.
Hii itapunguza sana ugumu wa maisha kuliko ambavyo kungekuwa hakuna ndege hizi kama hapo miaka ya kati.
Nichukue nafasi hii pia kuwapongeza Precision Air kwa kupambana kubaki sokoni na kupunguza makali ya maisha ya wanufaika wake kwenye ajira za kudumu na za muda mfupi hadi za wale wanaotoa huduma na zabuni kwa mashirika haya mawili ya ndege.

Najuwa kuna mashirika yanayofanya kazi na haya mashirika niliyotaja na pia na mashirika mengine ya kimataifa kam KLM, Emirates na mengineyo yatapunguza wafanyakazi lakini kwa vyovyote vile yatabakiza baadhi ya wafanyakazi waweze kuhudumia hizi ndege. Kam kusingukuwa na ndege hizi za ndani basi wote wangebaki nyumbani na kukosa hata nusu mshahara.

Ningependa pia kuwashauri wenye uwezo kutumia usafiri huu sababu hakuna mbanano, usafi wa hali ya juu, pia watu tumia muda mfupi kukaa pamoja safarini, huenda hii itasaidia kupunguza hatari ya maambukizi ya COVID-19.
Fikiria hatari iliyopo mbele yako kwenye usafiri mwingine pale unavyotumia masaa zaidi ya 10 kama humo ndani ya chombo kati yenu kuna watu wenye huu ugonjwa, kisha linganisha na kukaa nao pamoja chini ya saa mbili (2 hrs).

Mungu awabariki sana waliohusika kuhakikisha huduma hii inakuwepo, hapa nawazungumzia wote waliopo serikalini na huko sekta binasi kama shirika la Precision Air pamoja na mashirika mengine yenye ndogo zinazofanya chartered flights za ndani.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
IMG-20200322-WA0058.jpg
 
Hapa serikali imefanya kile alicho shauri Zitto kwamba serikali isaidie sekta ya utalii kwa kuwapa pesa waweze kushikilia waajiriwa wake, lakini hapa imefanya kwa sekta nyingine na kwa mtindo mwingine ambao serikali itarudishiwa pesa yake na ATCL, itapata gawio na kodi toka ATCL.
Kizuri zaidi serikali imetoa pesa hii kipindi ambacho janga lilikuwa halijaingia na makusanyo yake yalikuwa makubwa.
Kwa kuwekeza pesa ATCL imesaidia kupunguza makali sekata ya usafiri wa anga.

Waswahili wanasema akiba haiozi na sasa tunaona akiba ya serikali kwa uwekezaji wa ATCL unaisaidia serikali sasa ktk wakati mgumu.

Nawashauri pia wawaangalie Precision Air kama kuna namna wanaweza kuwapa nguvu kiuchumi iwe ruzuku (grant) au mkopo (loan) wa mashariti nafuu au bila riba kama wenyewe Precision Air wanaona wana uhitaji huo.
Mkuu angependa kuona Precision Air ikifa mchana huu wewe unasema aipe ruzuku. Anashangaa kwanini bado ipo angani.
 
Mkuu huu ni mtazamo wako tu.
Lakini haujavunja sheria yoyote, huenda unachodhania siyo sahihi.
 
Back
Top Bottom