Kongole AirTanzania, mnaimarika katika kuitekeleza ndoto ya Rais Magufuli

Tatizo nauli mkuu ..shirika halina ata offer ndogo ndogo kwa abiria wake ,that why watu wengi wanashindwa ku afford

Wanafanya Biashara mkuu, Hii Biashara wanavyocharge wanaangalia vitu vingi, muda unaosafiri, msimu mliopo mfano high au low,mshindani anafanyeje, garama za uendeshaji nk...ukitaka kufurahia usafiri wa anga kata ticket miezi mitatu kabla ya safari ndio utaona unafuu, sio unasafiri kesho unakata ticket leo,,lazima iwe gali tena saana
 
Kweli tatizo nauli zao si rafiki wajaribu ku adjust kidogo mbona wenzao fast jet walimudu kwa nauli rafiki ambapo wengi tulifaidika? Sasa ATCL mpaka mtu wa kawaida mnyonge na masikini wa Magufuli ukune kichwa sana kumudu nauli zao
Lakini kumbuka Precision Air nauli zilikua juu sana kupita za ATCL na bado watu walizimudu. Ni kuamua tu. La sivyo acha tusubiri Treni ya mwendo kasi nasisi tutatesa kivyetu!!!!
 
Tatizo ni kuua washindani wake, katika Biashara huwezi kujipima kama huduma ni zuri au la bila kua na mpizani wa dhati katika hiyo biashara, hiyo nikama propaganda tu. Mkubalie fast jet umpe na hizo route zote ndani ya mwezi moja utaona Atcl niwababaishaji I swear...

Hao jamaa hawapendi ushindani kabisa, wao wanataka kuwa peke yao then wanajisifia. Angali wameua fastjet then wanasema eti ATC inafanya vizuri na siti zinabaki mbili au tatu tu. Sasa kama hakuna mbadala wasafiri watapanda nini? Punda ama?
Sehemu nyingine angalia katika siasa, wapinzani hawaruhusiw kufanya siasa ila wao kila uchwao wako wanafanya siasa then wanakuja na ngonjera kuwa jiwe anakubalika sana ili hali pamoja na kufanya hivyo bado wananchi hawamtaki.
Bungel live hakuna ila wengine mpaka kuzindua kiwanda cha zamani wako live (usisahau uzinduzi wote ni yeye tu hataki ushindani)
 
Hivi fastjet alikuwepo hapa Tanzania kwa miaka mingapi huku ATC akiwa hoi na hakuweza kutupa huduma zaidi ya kuchangua njia zenye abiria wengi tu Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro? Wajinga ndio waliwao.

Kulikuwa na haja gani ya kuwafukuza kama nyie mnaweza kutoa huduma bora na kwenda huko wao wasiko kwenda?
 
Fastjet ilikuwa ni Low Budget Airline na ndiyo maana imeshindwa kwani operational costs ziko juu mno na ndiyo maana walishindwa.

Hawakushindwa, walifanyiwa figisu ili atc ibaki pekee. Jamaa hawawezi/hawapendi hushindani
 
Eti toka aingie hujanufaika na chochote..

Mkuu endelea kupanua mdomo atakuja kukuingizia tonge mdomoni kwako.

Hata mimi sijanufaika na lolote zaidi ya kuleta hofu na kuua uchumi pamoja na kuigawa jamii
 
Pongezi kwa Air Tanzania, pia hilo suala la nauri nafikiri wahusika watalifanyia kazi ili mambo yawe mazuri zaidi

Ama kweli ccyemu inapendwa na wajinga au mbumbumbu pamoja na masikini, sasa nauri ndiyo nini. Kuna mmoja kama wewe aliwahi kusema hiyo ni typing error
 
Wanafanya Biashara mkuu, Hii Biashara wanavyocharge wanaangalia vitu vingi, muda unaosafiri, msimu mliopo mfano high au low,mshindani anafanyeje, garama za uendeshaji nk...ukitaka kufurahia usafiri wa anga kata ticket miezi mitatu kabla ya safari ndio utaona unafuu, sio unasafiri kesho unakata ticket leo,,lazima iwe gali tena saana
IMG_5397.JPG

Hii ndio tiketi ya miezi mitatu kabla ya safari haina tofauti ni tiketi ya week mbili zijazo so unakipi cha kusema hapo
IMG_5398.JPG
 
Wakati unafurahia hiyo exceptions ya kupanda dreamliner kwa safari za ndani, elewa pia kuwa haipo kwa afya ya chombo chenyewe

Wataalamu wanasema ndege huwa zinachoka na routine ya kupaa na kutua, na kila Aina ya ndege Ina idadi yake ya hizo cycle za kupaa na kutua, idadi ya cycle hupungua Kutokana na kadiri ukubwa wa ndege unavoongezeka, kwa maana hiyo dreamliner haviwezi kuwa Sawa na bombardier kwa idadi ya cycles,

Inasemekana ili dreamliner uweze kurudisha pesa vizuri inatakiwa ikae angani at least masaa kumi kwa siku, Maana yake ni kuwa ufanye cylce Moja tu kwa siku

Kutendo Cha kurusha dreamliner kweli kwa africa kinafanywa Tanzania tu kama unavosema, technically kitaifanywa iwe scraped ikiwa bado Mpya kabisa
Si lakini Mkuu anapata kiki za kisiasa mengine badaye
 
Ndege zetu nzuri sana, uwekezaji mkubwa ila customer service ya ATCL bado sana. Wajitahidi kupokea simu za customer care na kujibu emails, dunia kw sasa ni digital waendeshe shirika kisasa.

Mfano: kubadili flight sio lazma nitembelee duka la ATCL mambo yawe mtandaoni tujihudumie huko.

La mwisho ambali bado ni mwiba ni NAULIIIIIIIIII . Jamani NAULI za ATCL bado kubwaaa licha ya kuwa na soko lote la TZ peke yao ila bado hakuna nafuu.
 
Waungwana wa JF nawasalimu,

Nipo safarini kuelekea Kigoma kikazi. Hivi sasa tunatua Uwanja wa Ndege wa Tabora kwakuwa tunapitia hapa kwenda Kigoma. Tupo na Ndege TC 128 aina ya bombardier. Nalazimika kulipongeza Shirika letu la Ndege kwa kuimarisha huduma.

Nimekuwa nikisafiri na Ndege za AirTanzania kwa muda mrefu hapa nchini na hata nje ya nchi. Nikiri kuwa kwa safari za ndani ya nchi,huduma zimeimarika sana. Kuanzia Cabin Crew, Marubani na Watumishi wengine wa AirTanzania, ukarimu na umakini unatamalaki.

Kwa safari zangu za Kigoma kwa Ndege za kuelekea Burundi na kupitia Tabora, leo nimeshuhudia Ndege yetu ikibakiwa na siti tupu tatu tu. Ni jambo la kutia faraja na kuonyesha wananchi kuridhishwa na huduma za AirTanzania. Kongole sana kwenu AirTanzania!

Kuimarika kwa huduma za AirTanzania ni kuisimamia kwa vitendo ndoto ya Rais wetu Dr. John Pombe Magufuli aliyejitoa kwa uwezo na maarifa yake yote kuhakikisha AirTanzania inaimarika na kuwa nembo yetu kitaifa.

Najivunia AirTanzania, najivunia kuwa mtanzania!
Nimewahi sema siku hizi wewe jamaa umepatiwa kîtengo serikalini....
 
Ndege zetu nzuri sana, uwekezaji mkubwa ila customer service ya ATCL bado sana. Wajitahidi kupokea simu za customer care na kujibu emails, dunia kw sasa ni digital waendeshe shirika kisasa.

Mfano: kubadili flight sio lazma nitembelee duka la ATCL mambo yawe mtandaoni tujihudumie huko.

La mwisho ambali bado ni mwiba ni NAULIIIIIIIIII . Jamani NAULI za ATCL bado kubwaaa licha ya kuwa na soko lote la TZ peke yao ila bado hakuna nafuu.

Nauli zao sio rafiki kwa watanzania wasio na kipato ..shirika nauli na early booking na booking ya kawaida zinafanana ..shirika halitoi ata offer
 
Ufanisi wa biashara aupimwi kwa testimony za abiria wake especially pale ambapo route zenyewe hana mshindani.

Watoe financial statement kama wana biashara nzuri hiyo ndio njia kupima mafanikio yao.

We biashara gani unaona mkurugenzi kutwa anajitokeza akiwa na sijui mara mzungu anaewaambia wapeleke ndege Gatwick mara balozi wa Nigeria. Kwenye akili zake kupata route za nje ni sawa na mkulima kupata accesss ya soko ya mazao yake.

Someone needs to tell that guy safari ya ndege ni demand ya hiyo route kutokana na ushahidi wa mahitaji ya abiria, sasa kuja mbele na mabalozi kuutangazia umma ya kuwa balozi anashauri waende nchini kwao ndio evidence ya market intelligence hiyo.

Yule jamaa sio mfanyabiashara i tell you na nitashangaa sana kama shirika lina faida nzuri sio kwa sababu naliombea mabaya, la hasha watu badala ya kulipa changamoto za kuboresha biashara wanaleta siasa za kupongezana mambo yasiyo na msingi na wala tija kwenye kuwaimarisha kifikra management.
Mbona linapiga loss za 100b+ kila maaka tangu kufufuliwa....

Maskini wanali subsidize shirika ili middle na upper class wapande ndege kwenye routes zisizo na demand.
 
Hovyoooo! kwa lipi toka awe Rais sijanufaika kwa lolote nilokuwa nayapata enzi za JK ni yaleyale, yani jamii yangu yoteee hatuoni lolote we're still the same.
.
2020 nendeni nae gamboshi mkaloge sio Ikulu
Kapange mstari lango la ikulu huwa kuna mgawo kila ijumaa jioni
 
Wakati unafurahia hiyo exceptions ya kupanda dreamliner kwa safari za ndani, elewa pia kuwa haipo kwa afya ya chombo chenyewe

Wataalamu wanasema ndege huwa zinachoka na routine ya kupaa na kutua, na kila Aina ya ndege Ina idadi yake ya hizo cycle za kupaa na kutua, idadi ya cycle hupungua Kutokana na kadiri ukubwa wa ndege unavoongezeka, kwa maana hiyo dreamliner haviwezi kuwa Sawa na bombardier kwa idadi ya cycles,

Inasemekana ili dreamliner uweze kurudisha pesa vizuri inatakiwa ikae angani at least masaa kumi kwa siku, Maana yake ni kuwa ufanye cylce Moja tu kwa siku

Kutendo Cha kurusha dreamliner kweli kwa africa kinafanywa Tanzania tu kama unavosema, technically kitaifanywa iwe scraped ikiwa bado Mpya kabisa
Wanaona raha kurusha dreamliner locally kumbe it is inefficient.

Ni sawa na kutumia Yutong Dar-Bagamoyo, tena hulijazi hata level seat.
 
Back
Top Bottom