Massenberg
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 1,173
- 1,370
Mnakosea sana mnapodhani kuwa hatima ya taifa hili iko mikononi mwa wapinzani. Hivi mnaamini kabisa kuwa jukumu la kuhakikisha katiba mpya au tume huru inapatikana ni la wapinzani?
Huu ni muelekeo mbovu na finyu kifikra sababu masuala haya mawili yanabeba maslahi ya taifa, taifa ambalo lina watu chungu nzima wasio na chama wala kupenda siasa.
Kudhani hivyo ni sawa na kuharibikiwa na gari nyumbani halafu ukae pembeni huku ukisema eti fundi ndiyo anapaswa kuja kutoka huko aliko alikokote yeye mpaka lifike gereji wakati kumbe wewe unaweza kufanya yote hayo na yeye akawa na jukumu lake la kulitengeneza tu.
Kitakachobadili mambo hapa ni mass movement ya watu waliopevuka fikra na kuona kuwa sasa imetosha hatuwezi kuendelea kupita njia ile ile ambayo mbele imezibwa na kwamba ni lazima wananchi wenyewe kwa wingi wao washike usukani.
Wapinzani wana mchango wao lakini si sahihi kutegemea kuwa mabadiliko ya nchi hii yako mikononi mwao na sisi wengine ni watazamaji tu. Hii ni vita ya kila mtu sababu matokeo yake yana manufaa kwa maisha ya kila mtu, mwenye chama na asiye na chama.