Kongamano mbadala la UDASA juu ya katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kongamano mbadala la UDASA juu ya katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by NewDawnTz, Jan 16, 2011.

 1. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kuna tetesi ambazo zimeanza kuzagaa huku niliko (Dom) na jana niliisikia nikapuuzia lakini leo asubuhi hii nimepita mitaa fulani nikasikia watu tena wanazungungumzia habari ya kuwepo na kongamano mbadala la ku-justify kutokuwepo haja ya kufanya mabadiliko ya katiba kwa kipindi cha karibuni kwa kuuonesha umma kuwa wanaolilia katiba mpya ni watu wenye haraka na walioko nje ya system na hawajui ugumu ulioko kwenye kuandika katiba mpya

  Mpango wenyewe unazungumziwa kuhusisha pia taasisi ya mojawapo ya elimu ya juu na "wataalamu wa mambo ya katiba" ili kupangua hoja mbalimbali zinazoendelea ku-justify haja ya kuwepo na katiba mpya. Hata hivyo haijawa clear zaidi ni chuo kipi kitatumika kuandaa mpango husika na hao watakaotumika ni wakina nani ila inadaiwa mpango kamambe upo jikoni kwa ajili ya kuweka haya.  Mtazamo wangu: Japo kuwa tetesi hazina haja ya kuzifuatilia lakini naanza kuona hizi zinaweza kuwa na uzito wake maana kama jana nimezisikia kwa mtu niliesoma nae chuo na ni mtu ambae ni kada wa karibu na baba yake aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa mmojawapo kanda ya ziwa na yeye ngazi za jengo la chama anazijua hadi idadi yake

  Pia naweza kuhisi uko usahihi katika hili kwa kuangalia namna ambavyo TBC1 walivyoripoti Kongamano la UDASA jana

  Kama hili jambo ambalo ni tetesi ni sahihi na huo mpango upo, basi bado watanzania tuna vita kali kuelekea kule tunakofikiri kufika MAANA VIONGOZI WETU NA CHAMA KILICHOSHIKA HATAMU YA DOLA BADO WAKO KWENYE USINGIZI MZITO SANA.
   
 2. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Mtazamo wangu: Japo kuwa tetesi hazina haja ya kuzifuatilia lakini naanza kuona hizi zinaweza kuwa na uzito
  Suala la kuwa na katiba mpya ni lazima tu no matter inamuudhi nani au nani ana allege akisikia suala hili...hii si habari njema kwa makada wa chama tawala wasioamini katika mabadiliko...hivyo haiingii akilini kusitisha mchakato kwa kua kada fulani kasema hivi ama vile... wafanye tu makongamano mengi iwezekanavyo ikiwezekana kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wananchi kupuuza katiba mpya lakini nikuhakikishie hizi ni dalili za mfa maji tu! salaam zako!
   
 3. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ni kweli. Hili ni jambo lisilowezekana.

  Kuhusu TBC1, binafsi inanikera tokea Tido atoke pale. Wamekuwa vibaraka wa CCM. Unaweza kuona namna wanavyozungumzia suala la Arusha. Kwa hiyo, bila shaka mjadala huo utarushwa na TBC na sidhani kama utaungwa mkono na watu.
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Jan 16, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,606
  Likes Received: 3,906
  Trophy Points: 280
  Mbona watu mnapenda sana kuukwepa ukweli?? watu wengi tu watasema katiba haitakiwi! ndio maana kuna kuwa na kupiga kura, ni ujinga na udikteta kukwepa uukweli kuwa tumetofautiana sana kimtazamo, haijalishi ni msomi au la!

  wanaopinga katiba kwa sababu ya kutokujua ni wajibu wetu kuwashinda kwa hoja na si kwa matusi, wanaopinga katiba kwa sababu ya kulinda maslahi yao ni wa kupingwa hata kwa kuuawa! It is very difficult not to encounter any in the forementioned categories.

  so wawe udasa, bunge, n.k we need new katiba, huo moto hauzimishwi kirahisi na utapata upinzani tu!!!!

  Juzi kwenye mdahalo wa Nkrumah kuna watu walisema hivyo pia, wale ambao kila siku mnawaita mashujaa!!
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ebu todokezee zaidi ulivyosikia ni taasisi gani hiyo inayotaka kuandaa hilo kongamano...
   
 6. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  BAADA YA KUANZA KUGUNDUA KUWA KATIBA MPYA NI NDOTO.....mnaanza kutapatapa..... taja mapungufu yaliyopo pamaoja na maboresho yanatakiwa yaweje si kusema tu kuwa katiba haifai
   
Loading...