Kongamano La Wanataaluma Katika Baadhi ya Picha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kongamano La Wanataaluma Katika Baadhi ya Picha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sanctus Mtsimbe, Jan 4, 2010.

 1. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #1
  Jan 4, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kwa taarifa kamili ya Kongamano, tazama link hii:

  https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/48885-kumbukumbu-na-maazimio-ya-kongamano-la-wanataaluma-waishio-ndani-na-nje-ya-nchi-2009-a.html

  [​IMG]
  Baadhi ya Wanataaluma Kutoka Ndani na Nje ya Nchi Katika Picha ya Pamoja; Golden Tulip Hotel: 18-12-2009

  [​IMG]
  Wanataaluma Wakifuatilia Waongeaji

  [​IMG]
  Changamoto: Mzalendo Mbuya ambaye amemaliza darasa la saba tu na kisha kuwa msaidizi wa fundi wa umeme. Baadaye alianza shughuli za ujasiliamali wa halali. Ufundi - Pikipiki-Teksi. Sasa hivi anayo kampuni ya Usafirishaji akiwa ana gari ndogo 4 na za mizigo 3, nyumba nzuri na anasomesha watoto elimu ya juu. Je Mafanikio ya mtu ni lazima awe amasoma sana?  [​IMG]

  Mzalendo Membe akitoa majumuisho ya maada yake ya Dual/Smart Citizenship. Kushoto Mz. Mtsimbe

  [​IMG]

  Mz. Maige akitoa Vote of Thanks. Kulia ni Mz. Consolata Maimu - TPN National Treasurer na Kulia Kabisa ni Mz. Janet Mbene - Member of Executive Committee
   

  Attached Files:

 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Dah tunashukuru sana mkuu Sanctus vp unaweza tupa hotuba ya baadhi ya wazarendo walionza maisha magumu mpaka wakawa watu wa maana kama huyo fundi mpaka kumiliki magari ya usafirishaji?
   
 3. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #3
  Jan 4, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mkuu; ninayo DVD za Mkutano wote, lakini pia nina maelezo binafsi aliyoyaandaa. Jamaa kila siku ilikuwa lazima auone mlango wa benki kwa chochote anachopata kwa siku. Na ni nusu benki nusu anatumia. Ana mafaili kibao ya bank deposits. gari alikuwa anaagiza mwenyewe toka Japan.

  Alitoa changamoto sana kwa wanataaluma hasa katika suala la uraia wa nchi mbili.
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyu mzarendo amenivutia sana,
  Je wapo wengine wazarendo halisi kama huyu?
  Tunahamu sana kama kuna uwezekana unaweza weka DVD hiyo na sisi tukang'amua?
   
 5. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #5
  Jan 4, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Mz. Membe. Aliamua kuweka hotuba yake pembeni na kutoa Mada ya Uraia wa Nchi Mbili kama Mwanataaluma. Lugha iliyotumika ilikuwa Kiswanglish

  [​IMG]
  Mz. Dr. Masau, naye alikuwa na yake ya kuongea yalitoa changamoto zaidi. Mimi familia yangu iko Texas na wana uraia wa huko. Mimi nina uraia wa TZ. Niliamua kuja kuwekeza nyumbani. Lakini mmmmh. Mazingira . . .  [​IMG]
  Mz. Modesta Mahiga - MD Professional Approach. Mimi nilikaa sana nje kisha nikaamua kurudi . . . . Kujiamini na kuwa na ubunifu na right attitude inalipa.

  [​IMG]
  Mz. Mutani - Executive Secretary TANLAP. Katiba inatupa kila aina ya mamlaka ya kuwawajibisha watendaji wazembe. Tuamke na tutumie haki yetu. Mikakati ni hii . . .

  [​IMG]
  Advocate: Ardhi ni mali ya nani? Mtanzania ana nini anachomiliki ili ajivunie? Right of occupancy ni miaka 99 tu. Afterall ardhi ni mali ya Rais kwa niaba ya wananchi . . . .
   

  Attached Files:

 6. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #6
  Jan 4, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Dr. Hassan Mshinda - DG COSTECH. Lazima tujenge Knowledge Based Economy. Tuthamini maendeleo yetu ya Sayansi, Teknolojia na Tafiti zetu. Tunayo mifano mingi tu ambayo Watanzania wengi wanafanya vema katika nyanja hiyo nje ya nchi.

  [​IMG]
  Mtsimbe - Naomba moja kati yenu iniambie: Inakuwaje nchi yenye utajiri mkubwa kama hii na rasilimali tele na wazalendo wanataaluma kama nyie na wengine wengi hawapo hapa mpaka leo hii tuko hapa. Moja aniambie inakuwaje Singapore ambayo tulikuwa nagazi moja kimaendeleo miaka michache iliyopitita sasa hivi inapaa na sisi tuko hapa? Asiye tayari kwa mabadiliko asithubutu kutaka kuleta mabadiliko. Tunataka tu walio tayari.

  [​IMG]
  Mz. Janet Mbene. Akisoma Salaamu maaluma za Mz. Maua Dfatari - Mlezi wa TPN ambaye alikuwa katika matibabu.

  [​IMG]
  Mjasiliamali na Mtaalamu wa ICT Mayunga - Nataka kuwa kama Mbuya. Du! Hii ni hatari.

  [​IMG]
  Dr. Olomi - Mkurugenzi wa Kituo Cha Ujasiliamali UDSM akifuatilia. Wanataaluma lazima tutoe Leadership na Culture Change. We need to change our attitude.
   

  Attached Files:

 7. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #7
  Jan 4, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Kushoto Mz. Magesa - Deputy President TPN. Katikatika Deputy Vice Chancellor , Prof. E.T.N. Bisanda DVC Academic[​IMG], Open University of TZ. Kulia Mz. Bakuza Secretary General TPN.  [​IMG]
  Karibuni katika Mkutano huu. Nyumbani Ni Nyumbani. Na wote tuko level moja hapa kitaaluma kwa kuwa hakuna taaluma iliyo juu ya nyingine. Mkutano huu ni wenu na ni nyie mnaougharamia.

  [​IMG]
  Prof. E.T.N. Bisanda DVC Academic; Open University. Tuna wanafunzi wengi kuliko chuo chochote. Hata hivyo bado graduates hawatoshelezi mahitaji. Mnaoweza njooni muwekeze nyumbani. In 5 years to come taifa hili litakuwa halina wasomi wa kutosha kukabili changamoto zilizopo kama hatutafanya kazi ya ziada. Tusipoangalia kama taifa tutaingia katika mgogoro mkubwa sana.

  [​IMG]
  Mz. Steven Kisandu; Financial Analyst from Kansas USA akitoa maada ya Mchango wa Diaspora katika maendeleo ya Nchi. Steve anaweza kuongea Lugha 5 za Kimataifa zikiwemo Kiingereza; Kijerumani; Kifaransa; Kiswahili nk.

  [​IMG]
  Modesta: Mpaka kieleweke.
   

  Attached Files:

 8. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  MR Mtsimbe nadhani mlijadili jinsi watanzania hususani waliopo nje wanapohamua kuja kuwekeza hapa nyumbani wanpokumbana na matatizo

  Nakumbuka kama ni kuteseka na kubaniwa na watawala alikuwa ni Mz. Dr. Masau,hilo liliwakatisha tamaa watanzania wengi saana, naamini kama serekali kipindi kile haikuwa inafanya Upasuaji wa moyo ndo ulikuwa wakati muafaka wa kuungania nae lakini walikuwa ni watu wakwanza kukatisha tamaa na hata kumnyanyasa Dr Masau tumshukuru kwani angekuwa si mzalendo angeweza kwenda hata Rwanda au uganda,

  Nionavyo mimi kuna baadhi ya watendaji wa serekali wanroho mbaya saana na hawataki maendeleo ya watanzania wenzao, hili halina kipingamizi na linawakatisha tamaa saana, ndo maana wazalendo wengi waliopo nje wanasita kurudi na kuwekeza nyumbani
   
 9. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #9
  Jan 4, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mkuu walikuwepo wengi tu. Kuna vijana 4 waliunganisha nguvu zao leo hii kampuni yao ina mapato zaidi TZS Billion 10. Yuko Mzalendo kajenga hoteli ya Kitalii Peter Vava yenye thamani inakaribia Billion 10. Tembelea www.mwanzoparklodges.co.tz nk.
   
 10. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #10
  Jan 4, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mzalendo; Story ya Dr. Masau ilimsikitisha kila mtu. Mzalendo Membe pia alitoa visa vingi sana vya kusikitisha alivyokutana navyo nje.

  Tumeliona hilo na liko katika maazimio na tunaliwekea mikakati ya utekelezaji na uwajibishaji.
   
 11. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  je mlialika watu wa upinzani na kuwapa nafasi ya kuongea?

  maua daftari ni mlezi wa TNP na ni kiongozi wa ccm, je kuna mlezi/kiongozi hata mmoja wa TNP ambaye yuko upinzani??

  je maua daftari kuwa mlezi wa TNP hakuleti picha nyingine kwa hii org??
   
 12. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #12
  Jan 4, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160

  Mzalendo Semilong;

  Kongamano hili lilikuwa ni open kwa kila Mwanataaluma. hakuna yeyote aliyealikwa kwa upendeleo maalumu. Wote walikuja kwa nia zao, uzalendo wao na gharama zao. Mialiko imetolewa openly katika mitandao, magazeti, Radio, TV na hata email circulations.

  Pili Kongamano hili halikubeba agenda za upinzani wala chama tawala, lilibeba agenda za maslahi ya taifa katika mitazamo ya kitaaluma na mada zote zilijadiliwa bila kuegemea kokote. Unaweza kupata details hapa:

  https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/48885-kumbukumbu-na-maazimio-ya-kongamano-la-wanataaluma-waishio-ndani-na-nje-ya-nchi-2009-a.html

  Wapo Wanachama na wapenzi wengi wa TPN kutoka kada mbalimbali wakiwepo viongozi wa vyama vya upinzani mfano, NCCR, CHADEMA, PPT nk. Dr. Maua Daftari alipochaguliwa, alipita katika mchakato kati ya mapendekezo mengi yaliyotolewa na hatimaye akapita kutokana na vigezo vilivyowekwa. Tulitaka mtu ambaye tukimhitaji anapatikana bila ya visingizio vya Ubusy au majukumu, anajitihada za kweli za kuwiwa na maendeleo ya nchi, ni kiungo katika ya watu wa kada zote, pia bara na visiwani, na ambaye akiitwa katika vikao atakuja.

  Mpaka sasa hatujaona dalili ya kuegemea katika ushabiki wa kisiasa. Mimi Binafsi si mwanachama wala mpenzi wa chama chochote cha siasa wala sina maslahi ya namna yoyote ile katika chama chochote.
   
 13. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,054
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 280
  Vipi Mz. Membe aliongelea nini kuhusu dual citizenship????Je mmepanga tarehe ingine kwa mkutano wapili???Anyway tunashukuru kwa hizi news nzuri next time nawengine tutajitahidi kuhudhuria.Good staff and keep it up.
   
 14. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #14
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mz. Membe is in support of Dual/Smart Citizenship na alitoa mifano mingi hai ambayo kwa kukosa kuwa na dual citizenship tunapoteza "Akili-Kazi" ya taifa. Pia alizungumzia kuwa Diaspora wasichukuliwe kama wasaliti na ni vema tuandae mazingira mazuri kwa wale wanaotaka kurudi. Mada yake na Steve Kissandu toka Kansas USA na michango mingi ya washiriki na kisha maazimio yote yanaendana. Angalia hapa:


  Kongamano limechambua na kukubaliana kuwa Watanzania Wanataaluma wengi wanahamia na kuishi nje ya nchi kwa sababu zifuatazo:

  ·Kupata Elimu ya juu na hasa ya vyuo vikuu huku baadhi wakitafuta uraia wa nchi husika ili kupata unafuu wa maisha yanayotokana na gharama za chini za elimu, matibabu n.k kwa raia ukilinganisha na wageni.

  ·Kutafuta ajira za kitaaluma katika sekta tofauti kama Afya; Elimu, Sayansi na Teknolojia; na wengine hutafuta ajira zisizo za kitaaluma katika sekta tofauti. Ajira nzuri katika nchi husika huwa rahisi kupata kama tu utapata uraia.

  ·Kutafuta, kufanya biashara na kuwekeza katika nchi husika

  ·Kupata uraia wa nchi husika: Sababu zinategemea mhusika mwenyewe na mazingira yake zikiwemo sababu za kindoa; michezo au kupenda tu kupata kibali/uraia wa kuishi huko kwa sababu mbalimbali.

  ·Sababu nyingine ni kama kupata mikopo; matibabu n.k

  Kongamano pia limetambua faida na michango inayotolewa na Wanataaluma wanaoishi nje ya nchi ikiwa ni pamoja na:

  ·Kutuma pesa nyumbani kwa ndugu jamaa na marafiki kwa ajili ya mahitaji mbalimbali yakiwemo ya kifamilia, ujenzi, biashara n.k.

  ·Kuunganisha na Kufanikisha shughuli za Kibiashara kati ya Wafanya biashara waTanzania na wa Nchi husika

  ·Kupata ujuzi wa Kitaaluma na Kisomi kwa baadhi ya fani kutoka kwa Watanzania wa Nje kusaidia nyumbani katika sekta tofauti.

  Kongamano pia limetambua changamoto mbalimbali zinazowapata Wanataaluma waliopo nje ya Nchi. Changamoto hizi ni pamoja na:

  ·Kukosa kutambuliwa, ushirikiano hafifu au kukosa kupata misaada toka kwenye baadhi ya balozi zetu nje na hata serikali kwa baadhi ya mambo kwa sababu mbalimbali; lakini zaidi ni ile dhana ya kuwaona watu walioenda kuishi nje kama wasaliti.

  ·Kukosekana kwa umoja wa kindugu kwa baadhi ya Watanzania walioko nje ili waweze kusaidiana katika mambo ya kimsingi na ya maendeleo.

  ·Kukosekana kwa taarifa za msingi za watanzania Wanataaluma waliopo nje ya nchi i.e. idadi; fani, matukio muhimu toka nyumbani, fursa za kazi katika mashirika ya kimataifa huko huko nje ama hata nyumbani nk.

  ·Kukosekana kwa sheria ya kuruhusu uraia wa Nchi mbili ili kwa wale walio na uraia wa Nchi za Nje wawe wanakubalika kuwa na wao ni raia wa Tanzania.

  ·Kukosekana kwa mikakati na sera nzuri kwa wale walioamua kurudi nyumbani na kuja kuwekeza ili kuchochea wengi waweze kufanya hivyo kirahisi.

  ·Kutokuwako mipango na mikakati ya maendeleo ya muda mrefu yanayoweza kuwapa uhakika wa maisha yao endapo watarudi nyumbani.

  ·Matatizo ya rushwa na usimamizi mbovu wa rasilmali na utawala usio wa uwazi na kuwajibika hapa nchini huwakatisha tamaa ya kurudi nyumbani haswa wakizingatia jinsi maswala ya utawala bora yanavyopewa kipaumbele huko nje wanakoishi.

  ·Kiwango cha huduma za jamii bado hakiridhishi sana kiasi cha kuwatia wasiwasi kama watoto wao na familia kwa ujumla watapata elimu na huduma za afya bora pamoja na mambo mengine ya ustawi wa jamii. Hii pia inachangiwa na ukweli kuwa viongozi wengi watoto wao wanasoma nje na baadhi wanapata matibabu yao nje ya nchi.

  Kutokana na hoja zilizotajwa hapo juu; Kongamano limeazimia yafuatayo:

  ·TPN iwe ni chombo mahsusi cha kuwaunganisha Wanataaluma walio nje na ndani ya nchi (kupitia vyama na Jumuiya zao, n.k.) na kushughulikia na kufuatilia masuala yao hapa nyumbani na hata yale ya kule nje hususani toka kwa balozi zetu na ofisi za serikali mbalimbali ndani na nje ya nchi.

  ·TPN iwe ni chombo cha kuwasemea hapa nyumbani katika masuala yao mbalimbali, vipaumbele vyao na mambo mbalimbali kuhusiana na uhamiaji na maendeleo kwa ujumla kwa Serikali ya Tanzania na Jumuiya ya Kimataifa hapa nyumbani.

  ·Wanataaluma wa Nje ni ndugu, jamaa na marafiki zetu na hivyo ni sehemu muhimu kwa maendeleo ya nchi. Hivyo basi wito umetolewa kwa madau mbalimbali kuweka mipango ya mbeleni na sera ambazo zitazingatia pia mahitaji ya wanaoishi nje.

  ·Ni vema wadau na vyombo husika vikaandaa mazingira mazuri kwa wale wenye nia ya kurudi na kuja kuwekeza nyumbani kwa kuweka vivutio na urahisi wa wanaorudi kuanzisha miradi yao.

  ·Kuhusu uraia wan chi mbili:

  a)Kwa kuwa kuna raia wa nchi za nje wanaopewa uraia nchini Tanzania lakini bado ni raia au wanatambulika katika nchi zao walizotoka,

  b)Na kwa kuwa tunao wanataaluma Watanzania wengi ambao ni wataalamu katika fani mbalimbali nchi za nje wanakoishi na wamepewa uraia wa nchi husika ingawa walizaliwa huku na ni ndugu na jamaa zetu lakini kwa ajili ya sheria yetu ya uraia wa nchi mbili haiwatambui,

  c)Na kwa kuwa wanataaluma hawa wanachangia maendeleo ya nchi yetu kwa namna mbalimbali kama ilivyoainishwa hapo juu

  Kongamano linatoa wito kwa Watanzania na vyombo husika kutowaona wanataaluma hawa kama wasaliti au kuwakatalia uraia warudipo nyumbani badala yake tuliangalie suala hili kwa mtazamo wa kimaendeleo na kuweka utaratibu makini wa kukubali kuwa na sheria ya kukubali uraia wa nchi mbili baada ya kuridhika na vigezo Muhimu vitakavyowekwa.

  ·Kongamano pia limetambua na kuipongeza hatua ya serikali katika kipindi hiki ya kuwatambua wanaoishi nje kama eneo maalumu na hata kuamua kuliundia Idara maalumu ya kushughulikia masuala yao. TPN inaahidi kufanya kazi kwa karibu na idara hii katika kushughulikia masuala ya waliopo nje kama kiungo chao au chombo maalumu katika masuala mbali mbali.

  ·TPN iendelee kuandaa Kongamano kama hili kila mwaka litakalowakutanisha wanataaluma Watanzania wa ndani, nje, wanazuoni; wafanyabiashara; serikali na wadau wengine kuzungumzia masuala mbalimbali ya Kitaaluma na yanayohusu maendeleo ya nchi.

  ·TPN ishirikiane na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi kuhusiana na suala zima la utumaji wa pesa nyumbani. TPN ifuatilie bank kuu kuona ni vipi inaweza kupunguza au kuondoa gharama za kutuma pesa na pia kuangalia uwezekano wa kuanzisha Diaspora/Investment Bank.

  ·TPN kwa kushirikiana na wadau wengine na wanataaluma ianze kuandaa Database ya wanataaluma waliopo nje na ndani ya nchi kwa madhumuni ya kuwatumia walio makini katika kazi za kitaalamu (consultancy and contract works) badala ya kazi hizo kufanywa na wataalamu toka mataifa mengine. Database hii pia itatumika kuunganisha walio nje lakini wanapenda kurudi kufanya kazi au kuwekeza na makampuni mbalimbali nchini.

  ·TPN iwe kama kiungo cha kusaidia kupata taarifa mbalimbali juu ya Tanzania katika mambo mbalimbali hasa yanayohusu utalii na biashara au uwekezaji.

  ·Wito umetolewa kwa wale ambao kwa kuishi kwao nje hawana maendeleo yoyote warudi nyumbani na kusaidiana kujenga nchi – Nyumbani ni nyumbani. Imedhihirika wakati wa Kongamano kwa mfano ulio hai kuwa mafanikio pia yanaweza kupatikana hapa nyumbani. Mwanataaluma mmoja wa darasa la saba aliyepata kuwa msaidizi wa fundi wa umeme tu, kwa sasa ana maendeleo makubwa sana ya kiuchumi na maisha kwa ujumla. Kama tukiwa makini na mikakati bora mafanikio yanaweza kupatikana hata nyumbani.

  ·TPN ifanye jitihada za makusudi za kuanzisha matawi nchi mbalimbali waliko Watanzania Wanataaluma ili kuunganisha nguvu za kimaendeleo
   
 15. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #15
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mkuu; tarehe bado hatujapanga tena. Lakini muelekeo ni kuwa henda ikawa December 2010 May be tarehe 15 (Ijumaa) au tarehe yoyote nyingine itakayokubalika.
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hongereni sana kwa hilo kongamano and keep it up. Ila mkuu hii takwimu na kinachoonekana kwenye hiyo site havifanani, mambo kama haya huwa yanaathiri credibility ya information. Hasa ukizingatia kipindi hiki ambapo kuna mjadala mkali kuhusu gharama halisi ya nyumba ya gavana
   
 17. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #17
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160

  Mzalendo Nyambala; asante kwa angalizo. Hakika nimekosea nadhani nimechanganya revenue ya 10 Billion ya wale vijana wanne na huyu Mzalendo wa Hoteli. Kwa uhakika ujenzi na expansion inayoendelea pale inatia moyo. Mimi nimeshatembelea. Ujenzi mpaka ulipofika umegharimu USD 2 Million kwa Phase II inayoendelea sasa hivi. Phase III itagharimu kama karibu TZS 10 Billion. Unaweza kupata details za uhakika kutoka kwa owner Mzalendo Mr. Peter A Vava [pav@mwanzoparklodges.co.tz]
   
 18. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #18
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Baadhi ya Wazalendo wa Kamati ya Maandalizi: Toka kushoto - Gervas Lufingo; Sanctus Mtsimbe; Consolata Maimu; Steve Kissandu (USA); Method Bakuza; Phares Magessa.

  [​IMG]
  Time to Network. Peter Vava (White Shirt & Jeans) of Mwanzo Park Lodges. "Let me take out my Business Cards"  [​IMG]

  "Mz. Membe sisi watatu sisi watatu unaotuona hapa tumetoka nje ya nchi kwa nauli zetu wenyewe. No Per diem, no allowances - Uzalendo bado tunao". "Na wewe hongera, niliona hotuba umeweka pembeni ukatoa Presentation iya Kitaaluma liyoenda shule".

  [​IMG]
  Dr. Olomi - Mkurugenzi Kituo Cha Ujasiliamali UDSM: Nasema hivi Wanataaluma tujitahidi kufanya yafuatayo:

  1. Kuanzisha na kutoa uongozi (Leadership) kwa mabadiliko ya mazoea ya Kifikra (Attitude Change) na Kiutamaduni (Culture Change) tukianzia na sisi wenyewe kila mmoja binafsi .
  2. Kuhamasisha na kuongoza mikakati yetu wenyewe na miradi yetu huku tukijifunza kutokana na makosa/mafanikio ya nyuma na kutoka nchi nyingine ambayo moja kwa moja yanalenga katika kutatutua changamoto za Kimaendeleo katika nyanja ya uchumi, siasa, jamii, nk.
  3. Kuwajibika na kuwa na moyo wa kizalendo huku kila moja wetu akijiuliza ni nini anaweza kuchangia katika kutatua maendeleo ya nchi badala ya kutaka kuona tu Serikali na wadau wengine ndiyo wanaotakiwa wafanye kila kitu.
  4. Kubuni mfumo wa Elimu na Mafunzo ambayo itatoa ujuzi wa kiutendaji na mabadiliko ya Kifikra na Utamaduni kutoka ngazi ya chini.
  5. Kuanzisha huduma mbalimbali za kifedha zinazoendana na mahitaji na changamoto za Kitanzania mfano wa Muhamad Yunus Grameen Bank Scheme
  6. Kubuni na Kuanzisha huduma ambazo zitaendana na mahitaji ya kijasiriamali kwenye miradi ya kilimo, au ofisi/nyumba za biashara, ufugaji, umeme, incubators (Sehemu za kuzalisha au kutoa Wajasiriamali), ushauri nasaha wa kitaalamu kuhusiana na sheria na taratibu, nk.
  7. Kuhakikisha kuwa kuna mipango madhubuti ya kuwawezesha wengi kuwa na taarifa na kujua mifumo ya masoko na nini kinatakiwa kifanyike.


  [​IMG]
  Thinking Critically while following the presentation . . . .
   

  Attached Files:

 19. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #19
  Jan 6, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Wazalendo na Wanataaluma Wenzangu;

  Tunalo deni katika Nchi yetu la kutambua kuwa sisi kama Wasomi na Wanataaluma tunayo sehemu kubwa sana katika kuleta maendeleo na mabadiliko ya kweli katika nchi yetu.

  Ni kweli kuwa Serikali na Viongozi wanayo sehemu yao ya kufanya katika kubuni mikakati na sera za kuleta maendeleo ikiwa ni pamoja na kuleta maendeleo ya ujumla. Ingawa pia katika katiba raia anayo haki ya kuwajibisha watendaji hasa wa serikali. Ni sisi tu kuchukua hatua za kisheria kufuatana na taratibu zilizopo.

  Lakini ikumbukwe pia kwamba, kila mtu binafsi anayo nafasi yake ya kuleta maendeleo ya nchi kwa kuanzia yeye binafsi, familia, jamii nk. Haitoshi kwetu sisi kuridhika kuwa kwa kuwa tunazo kazi nzuri na bora, na kwa kuwa tuna viapato vya kuridhisha na nyumba za kuishi na usafiri na kusomesha watoto katika shule tunazopenda, basi suala la maendeleo zaidi halituhusu sana japokuwa tunao uwezo mkubwa sana wa kuleta mabadiliko .

  Umefika wakati sasa lazima tukubali kuwa Wanataaluma na wasomi sasa tunayo nafasi kubwa sana ya kufanya kuliko wakati mwingine wowote. Kila mtu anayo sehemu yake na tunatoa wito kuwa wakati sasa umefika.

  Tafakari sana na amua sasa kuunganisha nguvu zetu za kiakili, kitaaluma na kisomi kuleta mabadiliko ya kweli.

  Fanya kila uwezalo kuhudhuria kuwa sehemu ya mabadiliko ya vitendo na wala si maneno ambayo hazijatufikisha kunakostahili.

  Tunatoa mwito sasa ni vema kila mtu anyevutiwa akajisajili kuwa mwanachama wa Mtandao wa Wanataaluma. Registration ni TZS 50,000/=. No Monthly fees ni TZS 10,000. Unaweza kulipa kwa njia yoyote rahisi hata kwa kukatwa airtime kidogo kidogo tu.

  Pia tunapenda kutoa mwito kuwa sasa Wanataaluma wanachukua nafasi yao ya kuleta maendeleo na mabadiliko katika nchi. Tunahitaji rasilimali zote hasa Utaalamu na Pesa.

  Kama uko tayari kujitolea katika lolote tafadhali tueleze na tuwasiliane.

  Pia kama uko tayari kuchangia kila siku kupitia kukatwa automatically Air-Time kila siku kati ya TZS 150 hadi TZS 1200 kwa siku, tafadhali tujulishe. Kuna utaratibu tunaandaa lakini tunahitaji sana support yenu.

  Kwa walioko nje ya nchi na Mikoani; tunahitaji kufungua matawi au Chapters kila mahali. Kama una uzalendo na nia ya kweli ya kusaidia maendeleo ya nchi kwa kuweka maslahi ya taifa mbele, tafadhali tuwasiliane. Tuunganishe nguvu na akili zetu.

  Fanya sehemu yako.

  Kwa walio tayari wawasiliane moja kwa moja na mimi au:
  Mr. Emmanuel Mmari
  TPN Finance and Administrative Manager
  Email: emmammari@yahoo.com
  Mobile: 0715 740 047

  Wasalaam


  Sanctus Mtsimbe
  President - TPN
  ---------------------------------------------------
  Tanzania Professionals Network
  TOHS Building - Dar Group
  Nyerere/Mandela Road
  P.O. Box 21605
  Dar Es Salaam, Tanzania
  ---------------------------------------
  Dir. Tel: + 255 - 22 - 216 3805
  Fax Line: + 255 - 22 - 2115 571
  Mob. Tel: + 255-754 833 985
  ---------------------------------------------------
  E-Mail: president@tpn.co.tz
  Web: www.tpntz.org

   
 20. m

  mdini Member

  #20
  Jan 6, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aaahhhh!!
  Sijaona muislamu hata mmoja hapo katika hiyo list.
  Jamani huu ni mkakati wa kinchi au kidini zaidi?
   
Loading...