Kongamano la Vyuo Vikuu Zanzibar; CCM bado ni tishio znz.

security guard

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
773
1,000
Nipo katika kongamano la vijana wa mkoa maalum wa vyuo vikuu wa chama cha mapinduzi unguja-Zanzibar. Kongamano limehudhuriwa na vijana wasomi makini wengi mno, mpaka mgeni rasmi makamu wa pili wa serikali ya mapinduzi zanzibar na mjumbe wa kamati kuu ya ccm balozi Seif Ally Iddy ashangaa kuona umati mkubwa wa wanavyuo kuwahi kutokea Zanzibar.

Katika Kongamano hilo ambapo wasomi wa Zanzibar wanapata kujikunbusha na kujifunza tunu za Mapinduzi na historia iliyotukuka ya visiwa vya Zanzibar, limechukua sura mpya baada ya watoa mada wakiongozwa na msaidizi wa makamu wa Rais Ndugu Suleyman Haji, Steven Masatu Wassira na Wilmo Mihayo mmiliki wa Kampuni ya Uhuru one kueleza umuhimu wa wasomi katika maendeleo ya jamii.

Mmoja wa wageni waalikwa ndugu Masauni Hamad Yusuph alieleza kwanini hatuwezi kuzungumza historia ya zanzibar na maendeleo yake bila kuitaja na kutambua nafasi na mchango wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndipo ukumbi ulipolipuka kwa shangwe na nyimbo za kuisifu CCM.

Kwa hali niliyoiona Upinzani hasa kwa Zanzibar bado wanasafari ndefu ambayo haina uhakika wa kufika katika kituo chao.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
 

TEMILUGODA

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
1,372
1,500
nipo katika kongamano la vijana wa mkoa maalum wa vyuo vikuu wa chama cha mapinduzi unguja-zanzibar. Kongamano limehudhuriwa na vijana wasomi makini wengi mno, mpaka mgeni rasmi makamu wa pili wa serikali ya mapinduzi zanzibar na mjumbe wa kamati kuu ya ccm balozi seif ally iddy ashangaa kuona umati mkubwa wa wanavyuo kuwahi kutokea zanzibar.

Katika kongamano hilo ambapo wasomi wa zanzibar wanapata kujikunbusha na kujifunza tunu za mapinduzi na historia iliyotukuka ya visiwa vya zanzibar, limechukua sura mpya baada ya watoa mada wakiongozwa na msaidizi wa makamu wa rais ndugu suleyman haji, steven masatu wassira na wilmo mihayo mmiliki wa kampuni ya uhuru one kueleza umuhimu wa wasomi katika maendeleo ya jamii.

Mmoja wa wageni waalikwa ndugu masauni hamad yusuph alieleza kwanini hatuwezi kuzungumza historia ya zanzibar na maendeleo yake bila kuitaja na kutambua nafasi na mchango wa chama cha mapinduzi (ccm) ndipo ukumbi ulipolipuka kwa shangwe na nyimbo za kuisifu ccm.

Kwa hali niliyoiona upinzani hasa kwa zanzibar bado wanasafari ndefu ambayo haina uhakika wa kufika katika kituo chao.

Kidumu chama cha mapinduzi.

cuf imefulia?
 

Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,712
1,225
Kwani si kongamano la CCM? Unashangaa nini iwapo waliokuwepo ni wao na huijuwi Zanzibar kaulize mikutano ya Pemba inavyojaa watu na mwisho wa siku CCM huambulia kitu?
 

SlaaSlaala

Senior Member
Apr 30, 2013
107
170
Mtoa mada kana kwamba CCM ilishakufa, kutokea kongamano kumetoa mshangao flani kama ipo!! Acha kudanganya watu Zanzibar CCM imekwisha na inazidi kuuliwa na Viongoz wenyewe wa CCM kushindwa kubadili sera zao zilizopitwa na wakati.


Zanzibar chama cha CCM kimebakia Makunduchi na baadhi ya vijiji vya kusini,,, na humo kuna makundi ya watu walioichoka.
 

Falconer

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
809
500
Security guard amenifurahisha sana kwa namna ya mmandishi yake. Ni kweli kabisa kuwa CCM ipo zanzibar wala hilo halina mjadala. Ninalo shangaa mimi ni kuwa viongozi wa juu wanashangaa kuwa bado CCM iko hai Zanzibar wakati hatujaizika bado. Iko cku yake ya kusomewa hitima lakini bado. Tupo kwenye UZALENDO wa kuitetea Zanzibar.
 

bendaki

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
954
250
Historia ya zanzibar kuonekana kuwepo umuhimu wa ccm? Ccm ilianza 1977 na zanzibar ina historia nyuma kwenye biashara ya utumwa. Ebu nijuze kilicho historia nione kilichowagusa vijana hadi kulipukia au ndio tuamini walilipuka kwa kusikia jina la kitu kilichowahi kufa.
 

security guard

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
773
1,000
Historia ya zanzibar kuonekana kuwepo umuhimu wa ccm? Ccm ilianza 1977 na zanzibar ina historia nyuma kwenye biashara ya utumwa. Ebu nijuze kilicho historia nione kilichowagusa vijana hadi kulipukia au ndio tuamini walilipuka kwa kusikia jina la kitu kilichowahi kufa.

Mkuu inaonekana haujui kabisa nini CCM..na kwa maana hiyo haujui historia ya nchi yako na kwa maana kuwa haujui identity yako, unahitaji darasa.
 

bendaki

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
954
250
Mkuu inaonekana haujui kabisa nini CCM..na kwa maana hiyo haujui historia ya nchi yako na kwa maana kuwa haujui identity yako, unahitaji darasa.

Mjaribu kuwa wapevu. Wakati mwingine ya ASP au ya TANU mnayaiita ya CCM, si sahihi. Mimi nilikuwa ASP lakini sio CCM.
 

Isalia

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
1,153
1,500
Mkuu inaonekana haujui kabisa nini CCM..na kwa maana hiyo haujui historia ya nchi yako na kwa maana kuwa haujui identity yako, unahitaji darasa.

CCM ndio nini katika mapinduzi ya z'bar hahihusiki hata mkijaribu kuihusisha ni sawa na kujitekenya mwenyewe na kucheka mwenyewe halafu usijidanganye kusema ccm inakubalika z'bar ni nguvu tu na ubabe wanaotumia kuwanyamazisha wapinzani wake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom