Kongamano la Vijana wa CHADEMA vyuo Vikuu DSM-Dr Slaa,Zitto,Mnyika,Marando Kuunguruma

thanks dada wa ukweli, nitakuwepo hapo mapeema kabisa na vijana wangu kadhaa, ila dada yangu mpendwa, siku nyingine msisahau kupeleka hii muv kwa vijana wa mikoani kwenye vyuo na watu wengi kama Dodoma, Mbeya, Mwanza na arusha, huko vijana wana mwamko mkubwa sana, BG UP CHADEMA msiwaige viwavi jeshi wa ccm UVCCM kwa matusi na kejeli zao
 
Ningeshauri Kama kuna uwezekano wa kustream online live, hata kwa audio ili watu wa mikoani tufaidi..ikishindikana wekeni podcast ya mada zote muhimu tufaham yaliyojiri, podcast ziwe uploaded mapema.
 
Tunakushukuru mheshimiwa. Ila dada yetu siku hizi umepotea sana kwenye jamvi,usiwe mbali na umma ulio kwenye mtandao. Mwambie hata mh.mbowe,mnyika na Dr.slaa either warudi hapa jf kwa ukamili au kama wapo watujuze ID zao mpya,maana ni muhimu sisi wananchi kupata habari kutoka kwao kabla ya kuchakachuliwa,kupata ushauri na kujengana kiujumla. Kumbuka kuwa kwa sasa hamna chombo chenye 'raw data' ambazo hazijahaririwa kama Jf. Hapa tunapata taarifa directly kutoka kwenye vidole vya mhusika. Mwisho,nashauri msitoe uanachama kwa waombaji wa zamani wa online kuanzia kabla ya uchaguzi kuepuka double registration. Mfano sie tulioomba online tangu agosti2010,tayari tumefika pale Ufipa kuomba upya physically na tayari ni wanachama,labda kama mtu atajaza baada ya system kuwa ok,ndo angepata usajili online. Pia mi binafsi nahitaji kupata kadi kama 500 au zaidi ili niweze kuwafikishia walioniomba kwa kushindwa kufika ofisi za chama sana sana walio maofisini. Hapa naomba unishauri ntazipataje,na kama kuzinunua nipate utaratibu maalum ili adhima yangu ya kufika 2012 tayari niwe nimeleta wanachama 700 kama mchango wangu kwa chadema. Kesho msisahau kutuletea Video cd,au dvd za tukio la Arusha kwa gharama yoyote,wananchi hawapendi kuona ile ya polisi iliyokwisha haririwa. Nakushukuru na natumaini majibu. Dada Regia,all the best,kesho tupo pamoja hapo mabibo.
 
PJ.Nimekupata.Kama kawaida sisi huwa hatuna muda wa kujibu nonsense sisi tunajadili mustakabali wa nchi.Mada zote zitatolewa na Viongozi wetu makini niliowataja ambao sidhani kama tutakuwa na muda wa kujadili ya hao wenzetu wa upande wa pili.Siasa za majitaka hazina nafasi kwetu.

Aluta Continua

Safi sana,tukiwa na akina dada kama wewe angalau 20 kila chuo/kata hapa nchini watatutosha sana kuleta mabadiliko mno.Sisi hapa Dodoma tunayo maandamano makubwa ambayo pia yatahitimishwa na Mkutano Mkubwa.Tupeane taarifa ya kila kinachoendelea tafadhali.Peoples.........!!!!.
 
Msituangushe mlo nyumbani, saa ya ukombozi wa taifa imewadia... hakuna atakayewaongoza ila ni dhamira zenu za dhati na mapenzi yenu ya dhati kutoka mioyoni mwenu kwa nchi yetu!!!!
 
Umesikika Mkuu.Tunapozungumzia Hali ya Kisiasa chini hayo yote uliyoyasema yanajadiliwa humo.Haya huwezi kuyakwepa..

Tup pamoja Aluta Continua
Tunahitaji tamko lililoenda shule,Tamko ambalo litaamsha hamasa kwa Wananchi.Sio tamko lililojaa matusi.Ni vyema likatolewa mapema kwani mchuzi wa Mbwa hunyweka ungali wa moto.

Dada Regia, polisi vp mmemalizana nao? nina pepa next wiq nisije kufanyia kitandani. Afu pale pale wekeni utaratibu tupate kadi mpya.
 
Baraza la Vijana CHADEMA(BAVICHA) linawakaribisha wanachama na wapenzi wa CHADEMA kuhudhuria kwenye Kongamano kubwa na la aina yake litakalofanyika kesho siku ya jumamosi tarehe 22 Jan 2011 katika Viwanja vya uwekezaji(Mkapa) Mabibo.

Kongamano hilo linatarajiwa kuanza saa 7 mchana mpaka saa 11 Jioni. Mada kuu zitakazojadiliwa ni Hali ya Siasa na Wajibu wa Vijana Wasomi,Mchakato na Maudhui ya Katiba Mpya,Wajibu wa Wanavyuo na nafasi yao katika Chama na nyinginezo.

Watoa mada watakuwa Dr Slaa,Zitto,Mnyika,Marando na Bi Regia.

Hili ni Kongamano la kwanza baada ya uchaguzi.

Vile vile kutakuwa na zoezi la kufungua ofisi ya Tawi la Wanafunzi.

Tafadhali usikose Kongamano hili muhimu.Ukipata taarifa mwarifu na mwenzako.

Nyote Mnakaribishwa!!!!!

Aluta Continua.

Mkuu,kama muda unatosha na kuna nafasi nami ningeomba kutoa mada hapo kesho.Najua sijachelewa sana,hivyo naomba unijuze asap ikiwezekana nifanye final touch ya nondo zangu!
 
Baraza la Vijana CHADEMA(BAVICHA) linawakaribisha wanachama na wapenzi wa CHADEMA kuhudhuria kwenye Kongamano kubwa na la aina yake litakalofanyika kesho siku ya jumamosi tarehe 22 Jan 2011 katika Viwanja vya uwekezaji(Mkapa) Mabibo.

Kongamano hilo linatarajiwa kuanza saa 7 mchana mpaka saa 11 Jioni. Mada kuu zitakazojadiliwa ni Hali ya Siasa na Wajibu wa Vijana Wasomi,Mchakato na Maudhui ya Katiba Mpya,Wajibu wa Wanavyuo na nafasi yao katika Chama na nyinginezo.

Watoa mada watakuwa Dr Slaa,Zitto,Mnyika,Marando na Bi Regia.

Hili ni Kongamano la kwanza baada ya uchaguzi.

Vile vile kutakuwa na zoezi la kufungua ofisi ya Tawi la Wanafunzi.

Tafadhali usikose Kongamano hili muhimu.Ukipata taarifa mwarifu na mwenzako.

Nyote Mnakaribishwa!!!!!

Aluta Continua.

Asanteni sana Mheshimiwa Dada Mtema kwa mapambano mnayoyakabili kwa niaba ya waTanzania wote. Nashukuru kuwa chama chetu kimetayarisha Kongamano hili na nina uhakika litafanikiwa. Wote wapenzi wa chama ambao hatutaweza kuhudhuria tutawawekeni kwenye mawazo yetu na tuna uhakika safari hii yetu itaishia pazuri. Nashukuru pia kuwa mnalitizama hili swala la online registration na hata kama ingewezekana mkawa na namna nyingine ya wale walioko nje kujiunga hata kwa njia ya zamani tu ya kuomba kadi kwa posta, tungeitumia kwa sababu tuna uchu sana ya kujiita wanachama kamili wa hiki chama chetu. Asanteni na poleni kwa mapambano. Aluta Continua.
 
I started hating CCM when they started hating my country and I started loving Chadema when they shone their light of love to my country! Its me and my beautiful country Tz!

Back to the topic, big up kwa kongamano lakini hii haitoshi, inatakiwa mkatoe somo vijijini maana huko wazalendo ni wachache sana, wao wanaimba sisi em tu hata kama inawaibia!

Nawatakia kila lakheri, tutafika tu Kanaani hata kama kuna majitu!
 
Nimekupata Bluetooth.Ni kweli tumekuwa na hili tatizo kwa muda mrefu kutokana na sababu mbalimbali.Chama kinafanya utaratibu wa kuhakikisha wanachama wote wanaojiunga online wanajiunga na wanapata majibu kwa maana ya kupata namba zao za uanchama.Mambo yakiwa yameiva nitakujulisha na ninaamnini automatically wale wote mliojiunga mtapatiwa majibu.

Asante.

Aluta Continua

great..! i appreciate na nitawafikishia ujumbe huu na pia ninaamini wameupata pia kupitia hapa JF
 
Sister Regia,

Mimi ninacho kiona hivi sasa chadema imeshaingia akilini mwa watu wote walioko miji mikubwa na hakuna atakayewabadilisha tena na hasa vijana na wasomi.
1. Tatizo ambalo bado tunalo ni namna ya kuwabadilisha ndugu zetu walioko vijijini ambao CCM huwatumia kama mtaji wao kwa sababu ya kutojua kinachoendelea.
Je kama chama tunao mkakati gani(japo yapaswa iwe siri ya chama) wa kubadili mitazomo ya hawa ndugu zetu wa kijijini. Kwa kuwa nguvu ya chadema ni vijana na wasomi, tunaamini kuna wadogo zetu wengi wapo vijijini na wamesoma japo shule za kata, Je hatuwezi kutumia kundi hili kuwashauri wazazi wetu. Nionavyo mimi makongamano kama haya ni budi pia yafanyike vijijini siyo mijini tu. Hatunahaja ya mikutano ya hadhara ambayo polisi hawaitaki lakini tunaweza kufanya makongamano ya ndani katika vijiji. Makongamano ya mijini yawe ni kwa ajili ya kuwaandaa vijana wasomi kwa ajili ya kuwatuma vjijini kwa makongamano zaidi.
Nadhani wapo vijana wengi ambao wanavipaji vya uongozi vyuoni na sekondari ambao chadema inawaandaa kwa ajili ya baadaye, basi hawa wafanye hii kazi ya kufanya makongamano huko vijijini kama sehemu ya training zao.

2. Kitu kingine da Regia ni kutokuwepo Chadema kwenye baadhi ya wilaya, hii ni lazima ifanyiwe kazi haraka, ni lazima kila wilaya sasa iwepo ofisi ya chadema na zipewe malengo na mikakati ya kukuza chama ndani ya wilaya zao kwa ajili ya maandalizi ya 2015. mfano mzuri wa wilaya amabazo hazina chadema ni baadhi ya wilaya za mkoa wa shinyanga ambako ni eneo potential kwa chadema.
 
Nimekupata Bluetooth.Ni kweli tumekuwa na hili tatizo kwa muda mrefu kutokana na sababu mbalimbali.Chama kinafanya utaratibu wa kuhakikisha wanachama wote wanaojiunga online wanajiunga na wanapata majibu kwa maana ya kupata namba zao za uanchama.Mambo yakiwa yameiva nitakujulisha na ninaamnini automatically wale wote mliojiunga mtapatiwa majibu.

Asante.

Aluta Continua
Ahsante dada Regia, mimi si mwanachuo lkn nilipitia huko vyuoni miaka kadhaa iliyopita lkn natarajia kuwepo leo na ikiwezekana kuwakokota na vjn wengine, naomba nyie viongoz wetu mjitahidi media ziwepo; kueneza chama kunahitaji coverage ya media vilevile.
Ushauri: Tovuti ya chadema iwe updated kila siku kutegemea na matukio sio tunaona mambo hayo hayo kila tukifungua. Hii pia itasaidia kukuza chama.
 
Natamani ningekuwepo,ila umbali huuuuuuuuu duuuuuuuuu.
hongera dada kwa taarifa
wanajf tunaomba mrecord then mtuletee hapa jf
hata nasi tulio mbali tuipate hiyo

mapinduziiiii daimaaaaaaa:kev::A S-fire1:
 
Mapambano yanaendelea mpaka kieleweke. Lazima tuwaonyeshe UVCCM kwamba sisi Vijana Wa Chadema zetu hoja za nguvu na siyo majungu wala matusi wala hoja sizizokuwa na mantiki.
 
Baraza la Vijana CHADEMA(BAVICHA) linawakaribisha wanachama na wapenzi wa CHADEMA kuhudhuria kwenye Kongamano kubwa na la aina yake litakalofanyika kesho siku ya jumamosi tarehe 22 Jan 2011 katika Viwanja vya uwekezaji(Mkapa) Mabibo.

Kongamano hilo linatarajiwa kuanza saa 7 mchana mpaka saa 11 Jioni. Mada kuu zitakazojadiliwa ni Hali ya Siasa na Wajibu wa Vijana Wasomi,Mchakato na Maudhui ya Katiba Mpya,Wajibu wa Wanavyuo na nafasi yao katika Chama na nyinginezo.

Watoa mada watakuwa Dr Slaa,Zitto,Mnyika,Marando na Bi Regia.

Hili ni Kongamano la kwanza baada ya uchaguzi.

Vile vile kutakuwa na zoezi la kufungua ofisi ya Tawi la Wanafunzi.

Tafadhali usikose Kongamano hili muhimu.Ukipata taarifa mwarifu na mwenzako.

Nyote Mnakaribishwa!!!!!

Aluta Continua.

Nashukuru kwa taarifa japo nafikiri taarifa zimechelewa sana. Watu wa mbali kama UDOM, SUA, SAUT, MUCE, Tumaini, Theofilo Kisanji, etc hawataweza kuja in a short notice. This should have been a well coordinated activity just to show the strength of the youth in CDM especially after the UVCCM tamko!
 
hizi ni habari njema sana ,zimefika wakati muafaka kabisa,
Ahsante Mh.Mb. Regia kwa taaifa yako.
 
Lazima niwepo ingawa nina test kesho duh!
Ok lakini suala na online registration niliwahi kusema kwamba kuna watu tuko tayari kushiriki katika ku-develop system free na wakaongezeka wengi tu katika hoja hiyo,as a student ningefurahi kushiriki as sehemu yangu ya mazoezi lakini mh,kimya and its stull not functioning
 
Back
Top Bottom