Kongamano la Vijana wa CHADEMA vyuo Vikuu DSM-Dr Slaa,Zitto,Mnyika,Marando Kuunguruma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kongamano la Vijana wa CHADEMA vyuo Vikuu DSM-Dr Slaa,Zitto,Mnyika,Marando Kuunguruma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Regia Mtema, Jan 21, 2011.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Baraza la Vijana CHADEMA(BAVICHA) linawakaribisha wanachama na wapenzi wa CHADEMA kuhudhuria kwenye Kongamano kubwa na la aina yake litakalofanyika kesho siku ya jumamosi tarehe 22 Jan 2011 katika Viwanja vya uwekezaji(Mkapa) Mabibo.

  Kongamano hilo linatarajiwa kuanza saa 7 mchana mpaka saa 11 Jioni. Mada kuu zitakazojadiliwa ni Hali ya Siasa na Wajibu wa Vijana Wasomi,Mchakato na Maudhui ya Katiba Mpya,Wajibu wa Wanavyuo na nafasi yao katika Chama na nyinginezo.

  Watoa mada watakuwa Dr Slaa,Zitto,Mnyika,Marando na Bi Regia.

  Hili ni Kongamano la kwanza baada ya uchaguzi.

  Vile vile kutakuwa na zoezi la kufungua ofisi ya Tawi la Wanafunzi.

  Tafadhali usikose Kongamano hili muhimu.Ukipata taarifa mwarifu na mwenzako.

  Nyote Mnakaribishwa!!!!!

  Aluta Continua.
   
 2. Nicazius

  Nicazius Senior Member

  #2
  Jan 21, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Asante sana Mhe. Dada Regina kwa taarifa hizo muhimu, tutakuwepo pamoja kuwakilisha, hakikisha mnakuja na kadi nyingi na watu wengi wa kusajili wanachama wapya kwani vijana wengi sana waha uhitaji huo wa kuwa wanachama wa CDM.

  Aluta Continua...
   
 3. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,035
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Asante Bi. Regia kwa taarifa, japo wengine tupo mbali tunawatakia kongamano zuri na lenye mafanikio mazuri kwa ukombozi wa nchi yetu.

  Peeeeeeeeeeeeeeeplez

  Power
   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,202
  Trophy Points: 280
  Asante Regia kwa taarifa yako.
   
 5. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Move makina sana
   
 6. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  regia.., nashukuru kupata nafasi hii kuweza kufanya collaboration na wewe... watu wengi wakiwemo wa nje ya nchi wanajaribu kujiunga na CDM online kwa kujaza online registration forms lakini hawapati majibu naomba unipe maelekezo sahihi
   
 7. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2011
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,218
  Trophy Points: 280
  Vipi polisi hawajakusanya bado taarifa za kiintelijensia isiyo na intelligence yoyote? Twawajua hawa vilaza wetu na mbinu zao mfu.
   
 8. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #8
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nahsukuru sana.Jina langu Ni Regia sio Regina
   
 9. M

  Mzalendoo Member

  #9
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mlioko huko plz muwakilishe vizur,nadhan pia ni muhm kw wale waishio street bas mshke mkono ndug,rafk au hat jiran yako mwende pamoja.
   
 10. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kila la kheri, saa ya ukombozi ni sasa na majira ya kufunguliwa kutoka ktk vifungo ni haya. Vipi, Dr Slaa kesha ruhusiwa toka hospitali, kwani kuna thread ilisema kalazwa hospitali kwa ajili ya mkono ndo maana hakuonekana ktk mahakama Arusha, Mola amjaliye afya ktk ili atimize vema majukumu yake ya kitaifa
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nimekupata Bluetooth.Ni kweli tumekuwa na hili tatizo kwa muda mrefu kutokana na sababu mbalimbali.Chama kinafanya utaratibu wa kuhakikisha wanachama wote wanaojiunga online wanajiunga na wanapata majibu kwa maana ya kupata namba zao za uanchama.Mambo yakiwa yameiva nitakujulisha na ninaamnini automatically wale wote mliojiunga mtapatiwa majibu.

  Asante.

  Aluta Continua
   
 12. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Shukrani sana kamanda wa umma, Da Regia;

  Kina mambo mawili ambayo yangewekwa yangezidisha nguvu ya umma ktk ufuatiliaji na changamoto husika.

  1. Suala la kupanda kwa gharama za maisha kama umeme, nauli, gesi nk wakati viongozi wanachezea rasilimali za umma na ufisadi wa mabilioni.
  2. swala la ukosefu wa uongozi wa dira kitaifa na kusababisha viongozi serikalini kutoa kauli za kuzozana na kuyumbisha wananchi, hasa kama suala la Dowans.
  3. Suala la wananchi kukosa imani na utawala uliopo, je vijana wanalo jukumu gani kujenga dira sahihi?

  Tupo pamoja na pamoja tutafika...Aluta Kontinua...
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mheshimiwa
  Dada Regia,
  Nakuheshimu sana.
  Kabla sijasahau napenda nitoe credit kwenye mawazo yenu ya kufanya kongamano, hasa kwa wakati huu. Kuna mengi sn ya kujadili, hata hiyo time frame mliyoiweka haitoshi.
  Wakati uvccm wameamua kukaa na kuibuka na agenda za matusi, nyie nendeni kisomi zaidi, na tazameni zaidi kwenye mustakabali wa nchi.
  Big up dadaangu-wish were there!
   
 14. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #14
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  asante dada.kesho sie tinaandamana dodoma.moto kila mahala hadi kieleweke
   
 15. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #15
  Jan 21, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asante sana dada yetu Regia. Pongezi CHADEMA kwa kuamua kuwatumia vijana kujenga Taifa.

  Ombi langu muwakumbushe vijana jukumu la kuwa kioo cha Tanzania, kuwa sehemu ya mabadiliko, tuwape elimu ndugu zetu mambo kwa namna moja au nyingine hawana ufahamu wa kutosha kuhusu hali ya nchi yetu na viongozi wa serikali/ccm uzivyowajali wananchi.
   
 16. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #16
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Umesikika Mkuu.Tunapozungumzia Hali ya Kisiasa chini hayo yote uliyoyasema yanajadiliwa humo.Haya huwezi kuyakwepa..

  Tup pamoja Aluta Continua
   
 17. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #17
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,035
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Mtakao kuwepo msisahau kutujuza yanayojiri hatua kwa hatua kupitia jukwaa hili la mabadiliko
   
 18. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #18
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,035
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Aise dada huyu zitto vipi? mbona hatumuelewieliwi yupo kwenye mstari wa mbele kwenye mapambano au anarudi nyuma na kwenda mbele?
   
 19. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #19
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  PJ.Nimekupata.Kama kawaida sisi huwa hatuna muda wa kujibu nonsense sisi tunajadili mustakabali wa nchi.Mada zote zitatolewa na Viongozi wetu makini niliowataja ambao sidhani kama tutakuwa na muda wa kujadili ya hao wenzetu wa upande wa pili.Siasa za majitaka hazina nafasi kwetu.

  Aluta Continua
   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0


  Katiba ni SHERIA MAMA ambapo sheria zote za nchi hupatikana na kufanyiwa kazi.

  Wakati sheria za kawaida hutungwa na wawakilishi wa wananchi kwa maana ya Wabunge kule bungeni Dodoma, Katiba ni sheria mama yenye UPEKEE KATIKA JAMII HUSIKA ambapo utungaji wake ni JUKUMU LA RAIA WOTE katika nchi.

  Sasa Ugomvi mkubwa kati ya vyama vya upinzani na Wanaharakati, kwa upande mmoja, dhidi ya CCM ni katika kusema kwamba NI HAKI YA KILA MTANZANIA KUSHIRIKI MOJA KWA MOJA katika kutekeleza wajibu wao kutunga Katiba Mpya.

  Lakini wao CCM wakiongozwa na Mafisadi wao wanasema Rais ANATOSHA KUTUTUNGIA TU KATIBA KWA KUSHIRIKIANA NA LOWASA, CHENGE na akina ROSTAM AZIZI kututungia tu katiba hiyo kupitia KIKUNDI CHA MADALALI WAO KWA JINA LA WATAALAM WALIOBOBEA KWENYE SHERIA.

  Sasa swali hapa ni kwamba; tangu lini Watanzania tukasikia KIKUNDI CHA Mi-FISI wakatunga sheria murua ya kulinda maslahi ya SWALA jangwani???

  UWEZO TUNAO, haki hapewi mtu bali ni kwamba haki hufuatwa na kuchukuliwa. Kazi inaendelea kila kona ya nchi kwa watu tunaojali maslahi ya taifa letu. Hakuna kulala!!!
   
Loading...