Kongamano la Sanaa la Mwalimu: Rais Magufuli apiga simu mbashara na kutoa pongezi, achangia Shilingi Milioni 100

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,598
141,413



Kongamano.jpg


Wageni waalikwa wameshaingia ukumbini wakiongozwa na mgeni rasmi Waziri mkuu Kassimu Majaliwa. Mhe. Kassim.

Majaliwa anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika kongamano la Sanaa la Mwalimu Nyerere linalofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaaam.

Waalikwa wengine ni Spika Ndugai, Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru Ally Waziri Mwakyembe Waziri Karume , RC Makonda na mzee Butiku.

> Rais John Magufuli amempigia simu rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania Ado Novemba na kumwambia anafuatilia shughuli hiyo ya kongamano la Sanaa la Mwalimu Nyerere jijini Dar.


KUSUASUA KWA MIKOPO YA WASANII

> RC Paul Makonda amemuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutoa neno kuhusu kusuasua kwa mikopo ya wasanii.

Akizungumza katika kongamano hilo, Makonda amesema mkoa huo uliomba ridhaa ya Bunge kwamba wasanii wapewe mikopo isiyo na riba kupitia fedha za manispaa lengo ni kuwawezesha kuendesha shughuli zao.

“Mwaka jana tulipata nafasi ya kwenda Dodoma bungeni katika uwasilishaji wa bajeti. Tuliomba wasanii wakopeshwe mikopo isiyo na riba, wabunge walituelewa na wakatupa nafasi hiyo.”

“Jambo hili linasuasua na halijafikiwa katika malengo, wasanii wanaambiwa waandike maandiko wanajitahidi wanaandika kila aina ya maandiko lakini hawapewi hizo fedha,” amesema

Makonda amesema fedha hizo zingekuwa zinatolewa ingepunguza malalamiko ya wasanii kukandamizwa na wasambazaji wa kazi zao.


HARAMBEE YA UCHANGIAJI WA MFUKO WA WASANII

Kuanzishwa mfuko huo kumekuja kufuatia ombi la wasanii ili uwawezeshe katika uendeshaji wa shughuli za sanaa Tanzania walilolitoa leo Ijumaa Novemba 15, 2019 katika Kongamano la Sanaa na Mwalimu Nyerere lililofanyika jijini Dar es Salaam.

“Mfuko huu kwa wasanii ni muhimu sana, ni sisi wasanii hatukuwa tayari kuwa nao kwa sababu hatukujua tutaufanyia nini. Mkiusimamia vizuri mtaona manufaa yake, Serikali inaunga mkono kuwepo kwa mfuko huu,” amesema Waziri Mkuu.

Pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ameanza kwa kuchangia milioni 5, viongozi wengine waliohadidi kuchangia fedha kwenye mfuko huo ni pamoja na:

Mh. Spika Job Ndugai, ambaye amesema, ''Wabunge wamenituma kwamba tunachangia milioni 5 na mimi mwenyewe naahidi kuchangia milioni tano, kwahiyo jumla ni milioni 10''

Waziri Mwakyembe, ambaye amesema, ''Wizara inaweka shilingi milioni 5''

Waziri wa Vijana, Utamaduni Sanaa na Michezo, Ali Abeid Karume (Zanzibar) naye amechangia shilingi milioni 5

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amechangia Sh laki 5, huku Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akichangia Shilingi laki 5 na CCM kama chama kikichangia Shilingi milioni 4.

RC Paul Makonda, ambaye ameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 5 (5,000,000)

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sofia Mjema ameahidi atatoa milioni moja (1,000,000) na kuahidi pia kuwashawishi wakuu wa Wilaya zingine za Dar es Salaam kutoa milioni moja kila mtu.

Naye msanii wa vichekesho Masanja Mkandamizaji ameahidi kutoa Sh 50,000 ''ya mchele'' kuchangia mfuko huo.

Lawrence Masha, ambaye aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, ametoa ahadi ya milioni 1 huku Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Dk Hassan Abasi atatoa milioni 3.

RAIS AMPIGIA SIMU WAZIRI MKUU NA KUCHANGIA SHILINGI MILIONI 100

Rais John Magufuli amempigia simu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kueleza kuwa anasikiliza kinachoendelea kwenye Kongamano la Sanaa la Mwalimu Nyerere.

“...Nayafuatilia na maagizo yenu nimempa Waziri Mkuu atawapa, nawapenda sana, endelea kusoma nasikiliza,” Rais Magufuli amesikika.

Rais Magufuli alitakiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo linalofanyika leo Ijumaa Novemba 15, 2019 ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam lakini amewakilishwa na Majaliwa ndipo alipopiga simu kueleza anasikiliza kinachoendelea.

"Nimepokea simu kutoka kwa mtu muhimu sana, kutoka kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema wasanii ni watoto wake hivyo atachangia Milioni 100," alisema Waziri Mkuu Majaliwa.


Waziri Mkuu Majaliwa amesema zaidi ya Sh140 milioni tayari zimechangwa.
 
Tunaambiwa Rais Magufuli anapenda sana ukweli na amesikika Mara nyingi akisema msemakweli mpenzi wa Mungu.
Kazi mpya ya msanii Roma Mkatoliki ijulikanayo kama "Anaitwa Roma" imejaa ukweli na uhalisia.
Nadhani mheshimiwa atakuwa kafurahishwa nayo sana hivyo ataagiza Roma naye apate mgao wa fedha kama furaha kwa kazi nzuri.
Screenshot_20191115-175711.jpeg
 
Mgao wake upo akijisahau tuu atapewa ule aliopewa kumbe hakuidhika nao
Tunaambiwa Rais Magufuli anapenda sana ukweli na amesikika Mara nyingi akisema msemakweli mpenzi wa Mungu.
Kazi mpya ya msanii Roma Mkatoliki ijulikanayo kama "Anaitwa Roma" imejaa ukweli na uhalisia.
Nadhani mheshimiwa atakuwa kafurahishwa nayo sana hivyo ataagiza Roma naye apate mgao wa fedha kama furaha kwa kazi nzuri.View attachment 1263810
 
Mwenye huo wimbo auweke hapa,tuusikie

State agent
 
State agent unaishi wapi wewe mpaka wakati huu hujausikiliza wimbo bora wa mwaka.
Kwa heshima yako ngoja nikuwekee uone jinsi kijana alivyo mzalendo kwa nchi yake.

Unatupa Bomu kwenye Mochwari halafu unajidai umeua.....hahahaaaa.


Roma Ishi Milele baba
 
Nampongeza sana msanii Roma kwa ujasiri wake! Siyo wale wenzangu na mimi walioamua kwa makusudi kabisa kujikomba komba kwa kusifia hata vitu vya kawaida.
 
Tunaambiwa Rais Magufuli anapenda sana ukweli na amesikika Mara nyingi akisema msemakweli mpenzi wa Mungu.
Kazi mpya ya msanii Roma Mkatoliki ijulikanayo kama "Anaitwa Roma" imejaa ukweli na uhalisia.
Nadhani mheshimiwa atakuwa kafurahishwa nayo sana hivyo ataagiza Roma naye apate mgao wa fedha kama furaha kwa kazi nzuri.View attachment 1263810
Kwetu huduma ya afya ni bora kuliko ndege.....Hakuna wa kumstopisha Roma.

Duuj Jpm kazi anayo.
 
Iwafikie Dungai na wapuuzi wote walioitisha et azimio la kumpongeza Mywether Leo.Hiki Ki nchi hovyo sn sn sanaaaaaaa.

Sasa mbona wanalazimisha watu kujiandikisha? Sasa mbona wanataka lazimisha watanzania kupiga kura?


Ccm jueni watanzania wote hawawataki.
 
Back
Top Bottom