Kongamano la Mwalimu Nyerere UDSM, kwanini wanatumia Kiingereza?

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,599
3,673
Pale Chuo Kikuu Mlimani (UDSM) Kunaendelea Kongamano la Mwalimu Nyerere, nawaona vingunge akiwamo Mkapa, Waryoba na wenzao pale pamoja na wageni mashuhuri. Kinachokera ni matumizi ya lugha ya kiingereza badala ya kutumia lugha yetu ya Taifa.

Wangeweza kabisa kuachana na ukoloni kwa kutumia vifaa vya kutafsiri ili wageni ndio wasikilize kwa kiingereza na lugha yetu itumiwe na wote watakaotoa mada.

Ukoloni, ukoloni tu.
 
Wameboa kweli,hapo wali wengi watakimbia kuusikiliza maana lugha ni "very big problem" kwa walio wengi!!!
 
Labda wameamua kufanya systematic discrimination; kuwapunguza watu wasiotumia kisomo katika mjadala!
 
Tusubiri watujibu
Wabongo bana ni shida tu. Mbona hukuhoji kwa nini Kingereza kinafundishwa sekondari na vyuo vikuu? wewe ambaye lugha yako imeendelea unaviwanda vingapi? usijilinganishe na China au Japan wale pale uchumi wao ni mkubwa. Isitoshe wa china wengi wanasoma wingereza kama unabisha just google ni wachina wangapi wanaosoma nchini wingereza.

Kiswahili peke yake hakiwezi kukufanya wewe uwe tajiri na kujitegemea, kama unabisha jiulize kwa nini kabila lako haliendelei? kabila lako lina lugha na kila kitu ila bado ni tegemezi na uchawi mwingi tu. Mimi napenda sana Kiswahili lakini kujifanya eti kutumia kingereza ndo utumwa mimi napinga kwa nguvu zote. Kama tu kwa kutumia kishwahili hiko hiko watu wanalogana, wengine wanakandamiza democrasia. Kiswahili hiko hiko kinatumika kuwakandamiza watu wa hali ya chini.

Afu acheni unafki, nje mnadai kua hamtaki Kingereza wakati watoto wenu wanasoma English Medium na wengine wako nje ya nchi. usipo kubali ukweli utaishi kwa bla blaa tu. Utatumia nguvu nyingi kujiaminisha kua uko sahii.
UDSM wako sahii kuendesha mjadala kwa lugha ya Kingereza maana ndo lugh ya kufundishia pale na watu wanajifunza. wewe kama huwezi kuchangia kaa pembeni.
 
Kingereza ni lugha ya taaluma.
Isitoshe, Wanaokuja hapo sio watanzania pekee, ni watu toka mataifa mbalimbali ambao kupitia sera au matendo ya Nyerere wamenufaika nao.
Pia, Nyerere alikuwa international figure. Sio rahisi kongamano linalomuhusu yeye liendeshwe kienyeji.
 
Wabongo bana ni shida tu. Mbona hukuhoji kwa nini Kingereza kinafundishwa sekondari na vyuo vikuu? wewe ambaye lugha yako imeendelea unaviwanda vingapi? usijilinganishe na China au Japan wale pale uchumi wao ni mkubwa. Isitoshe wa china wengi wanasoma wingereza kama unabisha just google ni wachina wangapi wanaosoma nchini wingereza.

Kiswahili peke yake hakiwezi kukufanya wewe uwe tajiri na kujitegemea, kama unabisha jiulize kwa nini kabila lako haliendelei? kabila lako lina lugha na kila kitu ila bado ni tegemezi na uchawi mwingi tu. Mimi napenda sana Kiswahili lakini kujifanya eti kutumia kingereza ndo utumwa mimi napinga kwa nguvu zote. Kama tu kwa kutumia kishwahili hiko hiko watu wanalogana, wengine wanakandamiza democrasia. Kiswahili hiko hiko kinatumika kuwakandamiza watu wa hali ya chini.

Afu acheni unafki, nje mnadai kua hamtaki Kingereza wakati watoto wenu wanasoma English Medium na wengine wako nje ya nchi. usipo kubali ukweli utaishi kwa bla blaa tu. Utatumia nguvu nyingi kujiaminisha kua uko sahii.
UDSM wako sahii kuendesha mjadala kwa lugha ya Kingereza maana ndo lugh ya kufundishia pale na watu wanajifunza. wewe kama huwezi kuchangia kaa pembeni.
wingereza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom