Kongamano la kumuenzi baba wa taifa Mwl JK Nyerere

segwanga

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
2,789
729
Great thinkers heshima kwenu,
Kongamano limeshaanza sasa hivi mwenyekiti mh Ben Mkapa ndo anatoa hotuba ya ufunguzi na anamfagilia J.KN kuwa alikuwa akipinga udhalimu,uonevu na unyonyaji.

Anaendelea kusema kumbukumbu za waasisi wa taifa hili lazma zitunzwa na anaipongeza serikali kwa kulifanyia kazi suala hili.
Amemaliza,amefungua kongamano
 
linaonyeshwa kwenye TV gani?

Baba hii ndo bongo bana,hakuna tv yoyote inayoosha cha kushangaza hili kongamano la kitaifa lililoandaliwa na OFISI YA RAIS,MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA.
Labda ningeandaliwa na ccm tbc1 wangeonyesha live.
Kongamano linazidiwa na la jana pale UDSM kwani hapa hakuna hata maji ya kunywa hata msosi baadaye.LABDA KWA SABABU NI NCHI MASKINI
 
WALIOPO HIGH TABLE:
Mh:Willy Ben MKAPA,Jaji Sinde Warioba, pius msekwa,kingunge,hawa ghasia,butiku,madaraka nyerere
 
mnmmmmmnhhhhhh......TANZANIA TANZA NIA..... bwe bwe bwe bweeeeeeeeeeeer reeedd wuuuuuuuuu, juhuuuu
 
sasa hv tunaangalia movie ya maisha ya mwl
Swali.Kwenye picha za mwanzo mwl alionekana akivaa tai,lakn baadaye hajavaa tena tai mpaka alikufa,hii imekaaje wadau?
 
Baba hii ndo bongo bana,hakuna tv yoyote inayoosha cha kushangaza hili kongamano la kitaifa lililoandaliwa na OFISI YA RAIS,MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA.
Labda ningeandaliwa na ccm tbc1 wangeonyesha live.
Kongamano linazidiwa na la jana pale UDSM kwani hapa hakuna hata maji ya kunywa hata msosi baadaye.LABDA KWA SABABU NI NCHI MASKINI
wewe umeenda kwenye kongamano au umeenda kula na kunywa? tupe habari ya yanayojiri na sii hizi porojo zako za kipuuzi.
 
Nina wasiwasi na waongoza kongamano...sioni hata maana ya TBC kuirusha make waliopo tu high table tayari ni mkanganyiko mtupu

Hapatakuwa na ushawishi wa upande wa criticism,bora nikaendelea kuangalia star tv live na mustakabali wa katiba mpya kutoka A.town
 
prof shivj anaongea kuwakilisha kigoda cha taaluma
1.Anaelezea kigoda cha taaluma kilianzishwa lini na lengo lake.Amesema kigoda sio taasisi wala idara
2. kigoda ni arena ya wanazuoni wa udsm kwa ajili ya kuchambua fikra za mwl kwa mtazamo wa kitaaluma
3.kigoda katka malengo yake ni kuendesha mihadhara na kila mwezi wa nne kuna tamasha la mwl nyerere ambopo wasomi wanajadili fikra za mwl,pia wameanzisha jarida la chemichemi.
AMEMALIZA
 
hahaha,teteh,kwikwi mhuu!

Ayo maji ya Kilimanjaro uliyopewa ni toi?
Rejea rtb kipengele namba 14..kuna rtb ya 'vuburudisho'...apo ndo panakuhusu sana..

Unles azawiz get back to ishu ya msingi...msikilize Butiku anaongea.
 
Butiku akiwakilisha taasisi ya mwl.
Kumuenzi baba wa taifa ni kutekeleza aliyokuwa akiagiza mwl.
Lengo kuu la taasisi ni kudumisha amani,umoja na maendeleo katka nchi,
Kila m2 ana haki mbele ya sheria.
Mwl alisema maneno makubwa hayafi mawazo hayo{yeye} hawezi kuyapinga.
Taasis hii si chama cha siasa lkn mambo yake ndo siasa. Amani siasa,umoja siasa,ardhi siasa etc
tuangalie wapi tumekosea si pale tulipofanya vzur

MZEE HUYU CHAI NYINGI ANAHHTIMISHA LKN POINTI CHACHE
 
MWAKILISHI WA CHUO CHA MWL NYERERE.
Ni chuo kilichoanzishwa kwa michango ya wananchi na mwl alisema chuo hiki ni chuo chetu watanganyika
Jukumu la chuo ni kuleta maendeleo kwa umma na wale watakafanikiwa kumaliza kwenye chuo hicho ni kama hamira kwenye mkate.
Chuo kilikuwa ni mali ya chama hapo awali,kuwaandaa viongozi.
chuo kinamwezi mwl kwa mitaala kuhusisha mambo aliyokuwa akiyasimamia,bodi kumuenzi mwl kila mwaka siku aliyozaliwa.
Mchango wa chuo kitaifa ni kuandaa viongozi wa taifa hili aidha wanafunzi wamekuwa wakifundishwa maadili na shughuli mbalimbali kama ukulima,ufugaji. Chuo kinatumia kiswahili. Chuo kitaanzisha tawi lake zanzibar na watadahili wanafunzi wa ngazi ya vyeti.
AMEMALIZA,YUKO VZURI SIO CHAI,Sasa hvi ni prof paramagamba kabudi
 
kabudi:mwl aliasisi muungano wa tanganyika na zanzibar ambao ni muungano wa kipekee barani afrika. Kuuvunja muungano huu ni pigo kwa bara zima la afrika.
Mwl alipigania usawa na alitaka kujitegemea"tusiwe kupe" my take wapi Vasco da gama?
Mwl katuachia tunu ya amani inayoundwa kati haki na umoja

Mwl alisimamia maadili mema,mwl alipinga rushwa ,udhalimu,ubalakala
Msingi mwingine mwl alotuachia ni demokrasia shirikishi.Kwa sasa siasa za uhasama zimeanza kumea na kama hatua sitahili hazitachukuliwa taifa litakuwa hatarini.
AMEMALIZA SASA MAWAZO YA WASHIRIKI
 
sasa hv tunaangalia movie ya maisha ya mwl
Swali.Kwenye picha za mwanzo mwl alionekana akivaa tai,lakn baadaye hajavaa tena tai mpaka alikufa,hii imekaaje wadau?
Vipi kuhusu yale manguo ya kijani na njano, kuna mahali alivaa??
 
hussein bashe maoni yake
sitaifikia tz ninayoitarajia
Amefunguka kuwa taifa linajadili dini,ukabila na viongozi wapo kimya.Atakayelaumiwa ni wazee hawa kwa kukaa kimya
 
fomu six toka ben mkapa,viongozi hawana maadili na wamekosa uzalendo,vijana tujifunze wapi?
 
linaonyeshwa kwenye TV gani?

Baba hii ndo bongo bana,hakuna tv yoyote inayoosha cha kushangaza hili kongamano la kitaifa lililoandaliwa na OFISI YA RAIS,MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA.
Labda ningeandaliwa na ccm tbc1 wangeonyesha live.
Kongamano linazidiwa na la jana pale UDSM kwani hapa hakuna hata maji ya kunywa hata msosi baadaye.LABDA KWA SABABU NI NCHI MASKINI
 
Wadau kuna mechi kali kati ya liva na manu,so kwa herini naenda kutimiza moja ya nguzo zangu za maisha yangu.Kwa sababu wadau wengine wamesusa kuripoti so poa baadaye
 
Great thinkers heshima kwenu,
Kongamano limeshaanza sasa hivi mwenyekiti mh Ben Mkapa ndo anatoa hotuba ya ufunguzi na anamfagilia J.KN kuwa alikuwa akipinga udhalimu,uonevu na unyonyaji.
Shetani hana soni!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom