Kongamano la kisiasa la waislamu tanga tarehe 4/3/2011 na umbumbu wa wengi wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kongamano la kisiasa la waislamu tanga tarehe 4/3/2011 na umbumbu wa wengi wao

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by tanga kwetu, Mar 30, 2011.

 1. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  nikiwa njiani kuelekea kazini leo asubuhi nilikutana na matangazo kuhusu kongamano la kisiasa la waislam jijini Tanga. Matangazo haya yapo kwenye karatasi za ukubwa wa A4 na ni black and white.

  Mada kongamano hilo, kwa mujibu wa matangazo hayo, ni kama ifuatavyo
  • tathmini ya kongamano la kitaifa la waislam lililofanyika jijini Dar
  • nini mwelekeo wa nchi kwa sasa na hali ya waislam nchini
  • je, maandamano ndio njia sahihi ya kuwaondoa viongozi madarakani?
  wakati nasoma tangazo hilo stand kuu wa mabasi, wazee wawili walionekana wapo safari moja (probably wa kiislam) walini-join kusoma tangazo na kuapa lazima wahidhurie kongamano hili maana inaonyesha litakuwa zuri sana kwa mujibu wa mada zake.

  Nilianzisha mjadala nao kwa kuwauliza, mada gani nzuri? nikajibiwa zote...
  nikaongeza swali la pili, maandamano gani yanataka kuitoa serikali madarakani? nikajibiwa,ya CDM?.....
  nikuliza swali la tatu,kwa vipi maandamano ya CDM mfano yale ya kanda ya ziwa yataitoa serikali iliyopo madarakani?nikjibiwa kwani wewe hujui na huoni??? nikajua kwa jibu hili, hawajui kitu ni mkumbo tuu
  ....nikauliza swali la nne, tangu mwaka gani CDM imekuwa adui namba 1 wa waislam na CCM imekuwa rafiki namba 1 wa waislam? nikajibiwa kwa swali 'wewe kwani dini gani?' kwa jibu hili nikajui hawajui kitu ni mkumbo tuuu!!!

  Watanganyika wenzangu, sikumbuki lini niliwahi kuwapongeza CCM ila leo kwa mara ya kwanza nawapongeza sana sana sana CCM kwa kufanikiwa kuwateka waislam na gea ya udini dhidi ya CDM!!!

  Naililia Tanganyika yangu maana ndugu zetu waislam walioshiriki kwa dhati vita ya kumtoa mkoloni mweupe leo wanamkumbatia mkoloni mweusi CCM kwa ahadi hewa ya OIC na mahakama ya Kadhi tu!!! Ahadi hewa maana nina uhakika hivyo vitu havitakuwepo Tanganyika hii labda nchi jirani ya Zanzibar.
   
 2. It is Sur_Plus

  It is Sur_Plus Senior Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na wewe pia ni miongoni mwa hao mambumbu unao wasema kwasababu. Yalikuhusu nini haswa hadi ukaanza kujadili yasio yako tena unawakejeli kwa masuala usioyajua hata wewe majibu yake
   
 3. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani watz, tuendelee na utaratibu wetu wa kuunga mkono au kupinga hoja kwa mantiki au nguvu ya hoja badala ya kuunga au kupinga hoja kwa misingi ya kidini, ni hatari. Tusidandie hoja bali tutafakari na kupembua hoja,siyo ukiambiwa maandamano yale yatavunja amani basi unapokea bila kutafakari kama kasuku bila kujiuliza kivipi? Pembua kabla.
   
 4. 2

  250689 Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mh..sidhani uko sahihi unaposema umbumbumbu wa waislamu.,nadhani ungekua sahihi kusema umbumbumbu wa watanzania katika masuala ya kisiasa.binafsi nimeshakutana na watu wanaohusisha imani zao(uislam na ukristo) na vyama vya siasa hususani cdm na ccm..ucegemee upande mmoja,watanzania bado tuna safari ndefu kisiasa...HAYA NI MAONI YANGU.
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ndugu tanga kwetu, kila mtu nchi hii anao uhuru wa kutoa maoni na kuchanganua mambo kadri anavyoweza yeye bila yaa kuvunja sheria.
  Inapotokea mtu amechanganua mambo kwa jinsi anavyoona yeye, mtu mwingine huna sababu ya kuwakejeli na kuwaita mbumbumbu kwa sababu tu hawana mtazamo sawa na wewe.
   
 6. A

  Anold JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 180
  Ni kweli CCM imefanikiwa, tena imefanikiwa kumpata adui muhimu ambaye kwa muda mrefu alikuwa inamhofia. Sasa hivi njia ni nyeupe kwa CCM kufanya itakavyo maana wamemteka aliyekuwa mlalamishi mkubwa wa sera zake toka uhuru. Sasa Tanzania itakuwa vilevile, maana nijuavyo mimi watu wenye ujasiri wa kudai haki zao kwa nguvu ni waislam, wakristo wanaeleweka wazi kuwa sio utamaduni wao kudai haki zao kwa nguvu au kupaza sauti zao kama kundi, mara nyingi wao wanasema inapobidi halafu mengine wanamuachia Mungu, maana wanaamini "anayekupiga shavu la kulia mgeuzie la kushoto". Waislamu wametoa upenyo bila kujijua na wasitegemee kufanikiwa kwa lolote. Ndiyo maana juzi walipotaka kuandamana walipigwa stop kiana na kufungwa vilemba vya ukoka ili wafanye tu mkutano bila maandanao na hili walitii. Nawapongeza sana kwa utii huu ila waelewe wazi kuwa katika kutetea haki zao za msingi ili kujikomboa na kufika pale ambapo wanadhani hawajafika, inawabidi wasiangalie Nani ni nani, wakiangalia CCM waone rangi ya kijani wasimwone Kikwete, mzee yusuph makamba n.k. inabidi waangalie ni namna gani chama hicho nawatu hao wanashughulikia shida na kero za wananchi bila kubagua.

  Mambo ya dini ni vizuri yakafanyika kwenye maeneo husika, ila inapofikia maswala yanayogusa maisha yako ya kila siku wewe pamoja na watoto wako usiyafanyie mzaha, maana wakati mtoto wako anapiga chafya kwa vumbi lililopo darasani mtoto wa aliyesababaisha hali hiyo anahimiza mwalimu apunguze kiyoyozi maana kinaweza kumletea mafua. Ninachotaka kusema hapa ni kuwa ni vizuri mkatumiwa kwa mambo mengine lakini haya yanayogusa maisha yenu na haja zenu jamani msiangalie CHAMA angalieni SERA na sio sera tu bali angalieni uwezo wa hao watu na rekodi zao. Pia msisahau njaa ya jana kwa pilau ya harusi!!! sio vizuri kujibainisha na chama au watu maana siku kikiondoshwa/wakiondoshwa hata nyie mmeondoshwa.
   
 7. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  UJUMBE WANGU KWA CCM:-
  1. Tuliwatisha kuwa wapinzani watatufikisha Rwanda, wakatishika, wakajificha, hali ilipoanza kutulia walihoji mantiki ya hoja yetu, kabla hatujajiba au badala ya kujibu tumetoa kitisho kingine kwamba;
  2. wapinzani ni wadini na wanatugawa, tayari wameshatishika, naamini hali itakapoanza kutulia watauliza mantiki ya hoja zetu, hapo tutaibuka na hoja nyingne!! JAMBO MOJA MUHIMU TUNALOTAKIWA KUZINGATIA NI:-
  SIKU MOJA WATATAKA MAJIBU YA MASWALI YOOTE WALOTUULIZA, KAMA HATUTAKUWA NA MAJIBU THEN, SISI PAMOJA NA WENYE VINASABA VYETU WATATIWA HATIANI, ITAKUWA NI VILIO NA KUSAGA MENO!! KINACHOTOKEA KWA NDUGU ZETU WAISLAM KWA SASA NI KUTISHIKA KWAO NA VITISHO TULIVTOTOA KAMA NDUGU ZETU WA KANDA YA ZIWA WALIVYOTISHIKA PALE WALIPOAMBIWA YATAWAKUTA YA RWANDA!!!! [I was there at that time]
  UJUMBE WANGU KWA MAKAMBA NA KIKWETE:-
  Huenda mnajipa moyo kuwa wakti watakapohitaji hayo majibu ninyi hamtakuwa viongozi tena huenda mtakuwa mlishakufa, lakini kuna jambo moja hamtalikwepa kwamba "justice cannot be undone!!" and that we are all not sure what does exist after DEATH!!
   
 8. m

  msosholisti Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikwete ndio chaguo la mungu- walisema maaskofu. mmmhhh umbumbumbu( kutojua) au kitu gani? nani mbumbumbu ?
   
 9. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Kilaini ndo alisema, nina wasiwasi kama alikuwa anawakilisha maaskofu wote(inc. My Zachary Kakobe)
   
 10. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,931
  Trophy Points: 280
  Inadhihirisha jinsi gani aliseme out of good will bila kusombwa na udini. Hii ndio tofauti ya msemaji na hawa wanaoandaa makongamano ya kulishana udini kwa kivuli cha siasa
   
 11. S

  SELEWISE Member

  #11
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo umenena kaka
   
 12. S

  SELEWISE Member

  #12
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya yote yanatokea wapi na chanzo ni nn? nadhan kila mtu anjaribu kuvutia upande wake,fikiri chukua hatua na heshimu mawazo ya wengine
   
Loading...