Kongamano la Katiba Mpya kuendelea Mkoani Mwanza, vigogo kadhaa kutoa mada

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
87,261
2,000
Hii ndiyo Taarifa mpya inayosambaa kila mahali hivi sasa , na kwamba watoa mada ni miongoni mwa wazito kadhaa , idadi yao inatajwa kwamba huenda ikazidi wale waliojitokeza Dar es Salaam

MUHIMU : Wahudhuriaji wanaombwa kuzingatia mwongozo wa WHO wa kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona

Kituo_kinacho_fuata_ni_mwanza..jpg
 

MdogoWenu

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
556
1,000
Mwaka 2025 hata bila katiba mpya CCM hawatafanya kosa la kuengua wapinzani wote wakabaki wao tu bungeni.

Kilichogundulika sasa ni kwamba wapinzani wasipokuwemo bungeni wanapata muda mwingi wa kufanya siasa hizi zinazowagharimu sasa CCM.

Haipiti wiki utamsikia mara Heche, mara Msigwa, mara Sugu, mara Tundu Lissu na watu wanawasikiliza wao hakuna mwenye habari na bunge.
 

Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,799
2,000
Hii ndiyo Taarifa mpya inayosambaa kila mahali hivi sasa , na kwamba watoa mada ni miongoni mwa wazito kadhaa , idadi yao inatajwa kwamba huenda ikazidi wale waliojitokeza Dar es Salaam

MUHIMU : Wahudhuriaji wanaombwa kuzingatia mwongozo wa WHO wa kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona

View attachment 1853477
Safi saana
 

Evarist Chahali

JF-Expert Member
Dec 12, 2007
994
1,000
Mwaka 2025 hata bila katiba mpya CCM hawatafanya kosa la kuengua wapinzani wote wakabaki wao tu bungeni...
Suala si kusikika bali kusikika huko ku-translate into kura. Opposition ilisikika sana wakati wa utawala wa Kikwete. What happened 2010 na 2015?
 

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
16,467
2,000
Suala si kusikika bali kusikika huko ku-translate into kura. Opposition ilisikika sana wakati wa utawala wa Kikwete. What happened 2010 na 2015?
Kura ziliongezeka kutoka mil 2 za Slaa hadi milioni 6 za Lowassa.

Wabunge waliongezeka kutoka 11 2005 -2010 hadi wabunge 48 2010-2015.

Kutoka 48 wa 2010-2015 mpaka 110 2015-2020.

Hii ilikuwa positive increase muhimu sana kilichotokea baada ya 2015 kila mmoja anajua ikiwemo wewe kuwa siasa ilikuwa shughuli hatari zaidi Tanzania kuliko ujambazi wa kutumia silaha.

Nyongeza CHADEMA 2010 waliweka wagombea kwenye majimbo 68 tu nchi nzima. 2015 waliweka zaidi ya 3/4 ya majimbo yote na mengine yalikuwa katika UKAWA MOU.2020 CHADEMA waliweka wagombea wa ubunge katika majimbo yote ya Tanzania na Unguja isipokuwa Pemba tu kwa kuwaachia ACT Wazalendo.

2020 ccm ililazimika kuengua wagombea kwenye majimbo ili wapite bila kupingwa na kutumia uharamia kupata vituoni.

Hivyo kusema upinzani umesikika ila sauti yake haijaupa kura siyo sawa.
Upinzani umefanikiwa kuigeuza sauti yake kuwa kura na ndiyo maana ccm inaogopa upinzani sasa hivi kuliko wakati mwingine wowote.

NB naweza nikawa sijaweka exact figures lakini kulikuwa na ukuaji wa haraka sana wa upinzani.
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,312
2,000
Suala si kusikika bali kusikika huko ku-translate into kura. Opposition ilisikika sana wakati wa utawala wa Kikwete. What happened 2010 na 2015?
Hey mkuu acha kujidhalilisha wewe ni mtu wa facts pls keep that way,waambie ccm wafanye kitu kimoja tu,wa level playing field then itisha uchaguzi mkuu next week uone nani ataibuka kidedea,kwa uozo huu wa kila kitu kimeelemea ccm unategemea nini?

CCM ilishindwa toka uchaguzi wa 1995 ,NCCR.M moto waliuwasha na ukamlazimu aliyeacha siasa na kurudi kijijini kwake kuamua kurudi tena kuokoa jahazi!
 

Tata

JF-Expert Member
Dec 3, 2009
5,800
2,000
Siasa haijawahi kufanyika ndani ya kuta za bunge bali mitaani. Hawa jamaa maadamu wana wafuasi wataendelea kufanya siasa bila shida. Hata ANC iliyokuwa imezuiliwa kufanya siasa na kuitwa chama cha kigaidi ilitokea mitaani na kushika dola.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom