Kongamano la amani: Wanenaji ni Askofu Kakobe, Askofu Malasusa na Sheikh Abdallah

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,902
141,845
Kongamano kubwa la amani na maendeleo linafanyika leo katika ukumbi wa Golden Tulip jijini Dsm.

Mwezeshaji wa kongamano hilo ni askofu Gamanywa wa BCIC na wanenaji watakakuwa askofu Kakobe askofu Dr Malasusa na shehe Abdallah.

Kongamano hilo litarushwa mubashara na runinga za TBC, Channel ten na radio ya WAPO kuanzia saa 2:30 asubuhi.
Wote mnakaribishwa.

Source Shallom tv

Up dates;

Mwezeshaji wa kongamano askofu Gamanywa ameshafungua mjadala na sasa mwakilishi wa Katibu mkuu wa TEC Dr Kitima ambaye alikuwa atoe mada, ndio anazungumza.

Askofu Kakobe anasema uchaguzi huu Polisi wamekuwa soft sana kiasi cha kusukumwa na kukaa kimya hivyo amewasihi polisi kuangalia viashiria vya uvunjifu wa amani na kuchukua tahadhari.

Shekh Alhad Salum anasema Waislamu na Wakristo ni kitu kimoja na mama yake Yesu yaani Mariam ana sura yake kamili katika kitabu kitakatifu cha Quran inaitwa Surat Mariam

Askofu Malasusa amepingana na askofu Kakobe na amesema polisi hawako soft bali wanatumia hekima ili kuleta amani kwa watu wote

Maendeleo hayana vyama!
 
Kongamano kubwa la amani na maendeleo linafanyika leo katika ukumbi wa Golden Tulip jijini Dsm.

Mwezeshaji wa kongamano hilo ni askofu Gamanywa wa BCIC na wanenaji watakakuwa askofu Kakobe askofu Dr Malasusa na shehe Abdallah.

Kongamano hilo litarushwa mubashara na runinga za TBC, Channel ten na radio ya WAPO kuanzia saa 2:30 asubuhi.
Wote mnakaribishwa.

Source Shallom tv

Maendeleo hayana vyama!
Hao wote Ni wapiga debe wa MAGUFULI. Hamna anayeweza kumwambia hapana.
Malasusa , kakobe na Gwamanywa na Gwajima Ni walevi wa Pombe za ikulu
 
Back
Top Bottom