Kongamano la akina Butiku na wenzie - kijiwe cha malalamiko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kongamano la akina Butiku na wenzie - kijiwe cha malalamiko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Marigwe, Dec 6, 2009.

 1. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2009
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Kabla ya kongamano hilo kukutana, nilikuwa nimejaa na matumaini kwa kijana Nape Nnauye nikawa nimeamua kama mkazi wa Ubungo, kumpigia kura ya maoni kwa ajili ya jimbo la Ukonga. Lakini baada ya kongamano lile nimeghairi. Nimetambua Nnape is just a philosopher/theoretician academician kama Baregu na Dr Azaveri Lwaitama. They are good at criticising only kama mashabiki wa mpira wa Kitanzania ambao wanajiona wao ni bora zaidi ya Maximo. Ukimpa Nnape aongoze hataweza. Mimi nayasema haya from experience. Tunaemjua Jackson Makwetta enzi zake kabla hajawa Mbunge akifundisha IDM naye alikuwa hivi hivi kama akina Baregu na huyu kijana Nnape. Leo Makwetta ana miaka 30 ndani ya jimbo Njombe kaskazini wapiga kura hata kumuona hawataki. Hilo la kwanza.

  La pili nielezee kongamano. Hilo kongamano mwanzoni nilifikiri limeitwa kwa ajili ya kuzungumzia mustakabali wa taifa within the context of the changing times and trends ndani ya utandawazi. Ah wapi Bwana kumbe ilikuwa ni mkusanyiko wa wazee ambao walikutana na kulia, kulalamika na kumlaumu kijana JK. Na wakaamua kumchapa Lowasa lakini hawakuwa na ujasiri wa kumtaja hata kwa jina. Basi wangemwalika ahudhurie. Sisi tunaoijua historia ya nchi yetu tunafahamu kuwa hao wazee ndiyo walioweka msingi mbovu wa utawala kiasi kwamba leo akina JK wanahangaika. Mimi ambaye Baba yangu alifanya kazi enzi za Nyerere wakati akina Butiku wakiwa ndiyo Private Secretary wa Rais, tunakumbuka alivyojenga himaya enzi zile. Butiku alikuwa very powerful kuliko hata Katibu Mkuu Kiongozi. Sasa akikumbukia enzi hizo lazima atakuwa nostalgic. Enzi zile zilikuwa za ujima ndiyo maana akina Butiku walimharibia mzee Nyerere mpaka akawa anaitwa Musa na mzee Haambiliki. Au Butiku amesahau jinsi alivyokuwa anapendelea watu wa kabila la kutoka Musoma ndiyo maana akina Warioba wakainukia. Enzi zile watu wa Musoma wakiitwa true Northerners. You had to come from true north to be given responsibilities especially sensitive ones kama jeshi, usalama wa taifa BOT n.k Kama hutoki huko hupewi cheo cha maana hata kidogo. Butiku amesahau hilo?

  Enzi zile hazikuwa kama leo ambapo nchi imebadilika kiteknolojia kwa hiyo huwezi ukategemea JK afanane na Nyerere au Mwinyi. Akitaka kufanana hivyo mnamtaka awe Dikteta? Jk anasoma alama za nyakati na anajua anachopaswa kufanya. Tanzania ya leo yule Prosper Mbena amabye ni Private Secretary wa Rais JK au kabla yake yule David Jairo hawawezi kuwa powerful kama alivyokuwa Butiku. Why? Kwa sababu mazingira ya leo siyo kama yale akina Nyerere. Jamani miaka hiyo Butiku ndiyo aliekuwa anawapa watu vyeo.Ukitakata kuukata upewe cheo lazima ukalambe miguu ya Butiku na akukubali. Muulizeni Mhe. Kitine alivyopanda kutoka kuwa Major kule chuo cha Monduli na kufikia cheo cha Mkurugenzi
  Mkuu wa Usalama wa Taifa. Badala ya kufanya kazi cheo kikampanda kichwani akawa anatembeza ubabe na starehe tu. Siku zile Radio moja TRD, Magazeti mawili Daily News la Serikali na Uhuru/Mzalendo la CCM. Kwa hiyo upuuzi wao ukawa hauandikwi. Isipokuwa zilikuwa zinadumishwa fikra za Mwenyekiti wa CCM.

  Tanzania ya leo haiwezi kurudi huko. Ninawaomba hao wazee watulie waandike vitabu na wale pensheni zao. Wakijiingiza kwenye uharakati wa siasa pensheni zao zitaliwa na madalali wa kisiasa ambao wako wengi siku hizi. Tanzania ya leo ni ya dotcom. Wawaachie akina Nnape, Masha,Serukamba, Vita Kawawa, Mnyika, Mbowe na kizazi cha akina JK na Lowasa ndiyo wawe wana kongamano kwa nia ya kuipeleka nchi mbele.

  Hebu angalia wale wazee kwenye kongamano lile. They are all spent forces. Hawana jipya. Mimi ningefurahi kama UDSM na vyuo vingine wangewatumia wazee hao kama wahadhiri ili wawafundishe vijana uzoefu wao.
   
 2. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Tell it to the birds!
   
 3. O

  Omumura JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu, hapo umenena haswa!wale wazee pale tusipoangalia wanalipeleka taifa pabaya. Ni kweli kabisa kile kilikuwa kijiwe cha malalamiko rather than providing alternative solution. Musa Nkangaa na Mateo Qares wlikuwa hawana jipya zaidi ya kulalamika simply because wapo nje ya system kwa sasa.
   
 4. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2009
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Ndugu zanguni,
  Hivi ni kweli hamuoni kuwa tunayumba?Wazee wale wamezungumza na pamoja na kuwa ni spent force tutafakari waliyosema.Butiku ameelezea pesa ilivyoyumika 1995 mpaka Nyerere akasimama kukemea,tujiulize ni nani aligawa pesa wakati huo,if you can read between the lines utamjua na utaona madhara ya hiyo network iliyoanza kugawa fedha 1995.
  Hivi hatuoni udini unavyotutafuna na pia upendeleo.
  Kuna mtu kachaguliwa uenyekiti wa bodi wakati mamlaka anayoiendesha iko hoi,je anayechagua hajui haya?
  hivi kweli kuna haja ya kuwa na mbunge wa kuchaguliwa na akapewa ukuu wa mkoa wakati vyuo vikuu vinamwaga watu mtaani kila mwaka?
  Siamini kuwa kile ni kijiwe na kama wakubwa wana busara wachukue hatua mapema.
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kawaambie waliokutuma kwamba umeshafanya kazi yao!!!
   
 6. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi skubaliani naye anaposema watu wa kaskazini ndio waliokula nchi enzi za nyerere. hili ni wazo lenye kitu nyuma yake! kikianguliwa kitaonekana vizuri

  ila nakubaliana naye kuhusu kulalamika kwa hawa watu. hawa ndio wale walioshindwa kuwa "mbuzi" kwenye hadithi ya kalumekenge enzi za uongozi wao na leo wantaka kuwa"mbuzi" wakiwa nje ya uongozi

  lakini nataka hili lijulikane kuwa naungana na wale wanaotaka rais afanye kazi inayotakiwa na watanzania na alitoapa uifanya, tena aifanye kwa mkono imara, aache ulegevu mbele ya waliomzunguka pindi wanapotakiwa kushughulikiwa kisheria
   
 7. J

  Jmpambije Member

  #7
  Dec 6, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kadanganye watoto wasiojuwa kusoma wala kutafakari
   
 8. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huu ni uongo wako wa kwanza ili kujenga hoja ya kumkandia dogo Nnauye.....

  ......Baada ya kujidai kuwa ulikuwa upande wa Nnape, then unaanza kumkandia bila kutoa sababu. Eti baada tu ya yeye kuongea kwenye kongamano ndio akamjua Nnape kiasi cha kujua jinsi uongozi wake utakavyokuwa miaka 10, 20, 30...ijayo.

  Hili ungelifanya ndio hoja yako ya kwanza kwani ndio ulilotumwa kulifanya kwenye uliyoandika.

  Nia yako halisi imeonekana hapa. Kwanza kulifanya kongamano ni la wazee ukianza kwa kufanya watu kama Nnauye walioshiriki kuwa si lolote.

  Pili unajaribu kumfanya Mzee kwa umri, Jakaya Kikwete (~miaka 60) ambaye pia kazi imemshinda, kuwa eti ni kijana. Ni vema ukatafuta uongo mwingine, maana sifa ya ujana JK hanayo tena.  Kama unataka kuwalaumu walimtangulia JK kuwa waliweka misingi mibaya, basi mjumlishe na yeye JK, aliyekuwa kiongozi mkuu chamani na serikalini tokea mwaka 1976.
  1. JK ndiye aliyekuwa Waziri wa Nishati wakati IPTL iliposainiwa.
  2. JK ndiye aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wakati Balozi Daraja alipoenda Texas kukutana na akina Mohamed Gire waliotuletea Richmond.
  3. JK ndiye raisi pekee tokea nchi ijitawale aliyeshindwa kuchukulia hatua mawaziri na watumishi wake walioshutumiwa kuwa mafisadi.
  4. JK atakapomaliza urais wake atakuwa raisi pekee aliyeitia nchi hasara kutokana na safari za kuzurura duniani zisizokuwa na faida kwa taifa.
  Positions, 'Sensitive ones', zilikuwa uwaziri wa mkuu, fedha, nje, usalama taifa n.k. Hebu tuambie true north gani hiyo iliyowapa akina Sokoine, Msuya, Salim, Malecela, Mtei, Mwakawago, Mkapa n.k.??

  Hapa unatuonyesha wazi kabisa kuwa ni nani unaowapalilia kwenye ulichoandika, Lowassa na JK.


  Unachochombezea hapa ni kuwa, eti wana-mtandao, ambao tayari wameshaifilisi nchi kwa muda mfupi tu waliopewa madaraka;
  1. Ni vijana wenye 'nguvu na ari mpya'
  2. Wanafaa sana kuiendeleza nchi kuliko watu wengine wowote.
  Hapo hapo unajitahidi kutaka kuwaziba midomo akina Salim, Butiku n.k., kwa kudai kuwa ni 'vizee' vya kutupwa visivyofaa kusikilizwa na wananchi pamoja na vyombo vya habari.

  Lakini hapo hapo unataka hao 'vizee' wakajifiche vyuoni. Nia yako ikiwa ni kwa hao 'vizee' wakae kimya ili wana mtandao waendelee kuila nchi bila bugudha.

  Shame on you.
   
 9. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Waambie hao waelewe safi sana.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,598
  Trophy Points: 280

  Ahsante sana ndugu yangu. Mafisadi yameamua kuwapandikiza watetezi wao hapa jamvini kwa fujo sana. Eti anaandika kwamba Kongamamno la akina Butiku na wenzie ni kijiwe cha malalamiko! :confused: Hawajasikia kauli za viongozi mbali mbali wa dini zetu wakitamka kwamba nchi inaelekea kubaya, hawajasikia malalamiko ya Watanzania mbali mbali ndani na nje ya nchi kuhusu Kikwete na Serikali yake kushindwa kabisa kupambana na ufisadi na pia kushindwa kutimiza ahadi zake zote ikiwemo kuiandika upya mikataba ya uchimbaji dhahabu ili Tanzania inufaike na rasilimali zake na madudu mengine chungu nzima katika Serikali hiyo. Tutaona viroja vingi kuelekea 2010 pamoja na kuitwa wehu. Makamba akisimama na Nkangaa na Qaresi na mtu kaambiwa kwamba kati ya watu hawa watatu kuna mwehu mmoja basi 99% watamchagua Makamba kama ndiye mwehu.
   
 11. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2009
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Sawa wana JF. Hayo ni maoni yangu ambayo siyo lazima yafanane na yenu au akina Butiku. Jambo ambalo nalisimamia ni kuwa huwezi kujifanya mtakatifu zaidi ya Pope. Miaka 60 ya JK mkabala na miaka 72 ya Buyiku na wenzie JK ni kijana.

  Ukiwasikia hao wazee kama uko nje ya nchi u get an impression kuwa Tanzania ya leo is in the same league as Somalia. That our country is ungovernable!! My foot!!
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  Dec 7, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Mhh hapa kazi ipo!
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama mwandishi ameeleza yote vile inavyotakiwa kuelezwa. Kama wazee nao hawana kosa kutoa dukuduku zao ili mradi hawavunji sheria. Haya mambo ya kutaka kuona vichwa tu vinatembea bila kusikia sauti yalikuwa enzi zile za Hilter na Mussolini.Waache waeleze yale yanayowasibu halafu tuyapime na kuamua
   
 14. M

  Mchili JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Awaambie nini hapo? Mbona anajikanyaga kanyaga tuuu.
   
 15. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Hauko sahihi chief, hizi ni propaganda zako na walio kutuma, wape ujumbe kwamba tunayumba, upo shimoni, tupo utupu, hatuna matumaini na serikali ya Chama Chenu, taifa linazikwa.
   
 16. R

  Rwechu Member

  #16
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13


  Nadhani wakati umejipinda kuandika upuuzi wako ubongo uliamua kuupindua, any way hata kama umetumwa kuwafanyia kazi mafisadi umeifanya kizembe mno, hoja zako zinaelea mno. Kama yaliyoongelewa yote hukuona la maana basi utakuwa na shida.

  Njaa itakuuwa!! Hakuna wa kumdanganya kitoto namna hiyo.
   
 17. g

  gangilonga New Member

  #17
  Dec 7, 2009
  Joined: Dec 11, 2007
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli nchi hii inakwenda kubaya mtu akitoa maoni anaangalia maslhi yake hata wale waliokusanyika pale kujadili mustakabali wa nchi ukiangalia historia yao walikuwa na mgombea wao,mm kama mimi namchukia MAKAMBA
   
 18. D

  Dalilah Member

  #18
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa, especially kwenye upande wa kuwapa vyeo vitatu vitatu watu wa zamani wakati hivi sasa kuna vijana wanaoweza kufanya kazi kwa hiyo "kasi mpya" ila cha kushangaza ikitokea opening wanatafutwa "old dogs"
   
 19. D

  Dalilah Member

  #19
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Asante kwa kumuweka sawaChief, hadithi yake ndeefu na ujumbe finyuuuu!! poropaganda
   
 20. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kweli mmeichoka Tanzania yetu...

  omarilyas
   
Loading...