KONGAMANO KUBWA LA KUIBUA FURSA ZA UCHUMI MKOA WA KAGERA KUFANYIKABUKOBA

Datus

Member
Nov 24, 2009
10
20
Asasi ya "Bukoba Mpya Foundation" kwa kushirikana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Imeandaa Kongamano kubwa la kuzitambua na kuzitumia Fursa za maendeleo mkoani kwa vijana, kina mama, kina baba na Wazee wastaafu.
Mada mbalimbali zitatolewa
- Ufugaji wa Kisasa, uvuvi.
- Ufumbuzi wa gonjwa la mnyauko kwa mazao ya chakula.
- Kutambua na kukuza vipaji kwa watoto na vijana.
- Nini kimeirudisha Kagera yetu nyuma kimaendeo.
- Kilimo cha Kisasa.
- Nini kimepelekea mkoa kushuka katika sekta ya Elimu.
- Kukuza utalii na kuifanya kagera kuwa sehemu ya utalii.
- Ujasiriamali wa mtu Mmoja Mmoja au vikundi.
Kongamano hilo litafanyika kwa siku mbili
Lini: Tarehe 15-16 July, 2017
Mahali: Yasira Hotel Bukoba
Sambamba na mijadala kutakuwepo na maonesho ya bidhaa zinazozalishwa
mkoani kagera na nje ya mkoa. Pamoja na shughuli za utamaduni wa Mhaya.

Taasisi mbalimbali zitaonesha namna zitoavyo huduma kwa wananchi.
Kongamano litapambwa na Burudani toka kwa wasanii wazawa na (kina Saida, Kapotive, Maua Bk sande na wengine wengi)
(Watoa Mada. Prof. Aurelia Kamuzora, Dr. Frank Theobald, Dr. Nicholaus Tutuba, Mwl. Gelasio Rweyasiza, Ndg. Dioniz Malinzi, Mh. William Rutta, Natural World Consultants, Ndg. Revocatus Biro, na wengineo)
Kongamano hili limedhaminiwa
KAGERA SUGAR, NSSF, PSPF, MKOMBOZI BANK, CRDB BUKOBA BRANCH, CRDB MULEBA BRANCH , WALKGUARD HOTELS TANICA, KEMIBOS, MWENDO WA SAA PETROL STATION, HALOTEL, COFFEE TREE INN, CHUO CHA KILIMO MARUKU, BUKOBA TOURS COMPANY, KIROYERA TOURS COMPANY. KIMISI HOTEL.
Kwa mawasiliano Zaidi wasiliana na waratibu wa BMF
Ndg. Yunus Kabyemera
(+255 765 977 247)
Dr. Frank Theobald
(+255 629 505 603)
Ndg. Fahamy Mastawil
(+255 745 151 510)
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,383
2,000
Tunahitaji kuandaa hivi vitu kila mara hata kama ikiwa mara tatu kwa mwaka ni nzuri sana, wakati huo huo wadau nasi tunapishana katika hili na lile ili mambo kwenye karatasi yahamishiwe kwenye matendo ardhini
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom