Kondomu Zenye 'Meno' Kwaajili ya Wabakaji Zazinduliwa Afrika Kusini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kondomu Zenye 'Meno' Kwaajili ya Wabakaji Zazinduliwa Afrika Kusini

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Jun 24, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kondomu zinazoitwa "Rape-aXe" ambazo ni maalumu kwaajili ya wanawake kuwakomesha wanaume wabakaji :usa:
  Kondomu mpya kwaajili ya wanawake zenye meno kwaajili ya kuwafundisha adabu wabakaji zimezinduliwa nchini Afrika Kusini. Kondomu hizo zinazoitwa "Rape-aXe" zilikuwa ni ndoto ya miaka 40 ya daktari wa nchini Afrika Kusini, Dr Sonnet Ehlers ambaye wakati akiwa na umri wa miaka 20 akisomea udaktari alikutana na mwanamke aliyebakwa ambaye alikuwa akilalamika sana.

  Mwanamke huyo alimuambia Ehlers "Natamani kama kungekuwa na meno huko chini, ningemfundisha adabu yule".

  Ehlers alisema kuwa alimwahidi mwanamke huyo kuwa siku moja atatengeneza kitu cha kuwasaidia.

  Katika kuthibitisha ahadi yake, Ehlers amezindua kondomu kwaajili ya wanawake zinazoitwa "Rape-Axe" ambazo zimeanza kutumika wakati huu wa kombe la dunia.

  Kondomu hizo zina kitu kama meno kwa ndani. Mwanamke anayeivaa kondomu hiyo anapobakwa, meno katika kondomu hiyo huunasa uume kama pingu.

  Kondomu hiyo inaponasa kwenye uume, huwa haitoki kirahisi na mtu anapolazimisha kuitoa ndivyo inavyozidi kuubana uume kwa meno yake.

  Ni madaktari pekee ndio wanaoweza kuinasua kondomu hiyo hivyo kuwawezesha madaktari kuwagundua wabakaji kirahisi na kuwaripoti polisi.

  "Inasababisha maumivu makali", Ehlers aliiambia televisheni ya CNN katika mahojiano na televisheni hiyo kuhusiana na kondomu hizo.

  "Mbakaji hataweza kukojoa wala kutembea wakati inaponasa kwenye uume wake, kama atajaribu kuitoa kwa nguvu, itaubana zaidi uume wake", alisema Ehlers.

  Ehlers anasambaza jumla ya kondomu 30,000 kwa wanawake nchini Afrika Kusini ili wajilinde na wabakaji wakati wa fainali za kombe la dunia zinazoendelea nchini humo.

  Hata hivyo kondomu hizo zimekumbwa na malalamiko toka kwa watu ambao wanahofia kondomu hizo zinaweza kutumiwa vibaya na wanawake kuwakomesha wanaume.

  Mwanamke mwenye hasira kwa mpenzi wake anaweza kuzitumia kondomu hizo kumuaibisha mpenzi wake.

  Hatari nyingine iliyoelezwa kuhusiana na kondomu hizo ni mwanamke kushambuliwa na mwanaume mbakaji kwa hasira za maumivu atakayoyapata.

  Ehlers kwa upande wake amezitetea kondomu hizo kuwa zinahitajika ili kupunguza idadi ya wanawake wanaobakwa kila siku nchini Afrika Kusini.

  Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa matukio ya ubakaji duniani ambapo asilimia 16 ya raia wa Afrika Kusini wanaishi na virusi vya ukimwi.
  Chanzo NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.

  Inafurahisha Kondomu zenye meno? Natamani na hapo kwetu bongo Zije hizo Kondomu zenye Meno kwa chini,ziwakamate Wabakaji wanawake kasheshe kweli huko South afrika.
   
 2. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Haziwezi kuwang'ata wanawake wenye hahahahaha
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hizi ni maalum kwa wabakaji tu:dance:
   
 4. D

  Diana-DaboDiff JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2010
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii condom itazua balaa nyingine wabakaji watagueka walawiti.
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Jun 24, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Mmmh hizo kondomu kiboko.
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Ilibidi iwe siri, sasa wabakaji watakuwa wanakagua kwanza ma-apple kabla ya kubaka, say, kwa kutanguliza kwanza kidole. Bakaji likishagundua kuwa kuna hiyo kondomu laweza kuitoa na kuigeuza na kumvisha mbakwaji ili imtafune mtegaji!! Hivyo wanawake watakuwa wanaivaa masaa yote?
   
Loading...