Kondomu yavunja ndoa. Huu ni wivu au umakini katika ndoa???

Huyo mwanamke anatakiwa kupimwa akili.... kukuta kondom kwenye suruali ya mumewe ni jambo moja na kutembea nje ya ndoa ni jambo jingine. ni mambo tofauti hayo....LABDA ALIWEKEWA MFUKONI. amtende haki mumewe banaaa..:angry:
 
Hakuna cha wivu hapo,ndo umakini wenyewe,wanaume acheni uzinzi nje ya ndoa zenu,kama huwezi usioe,mnakula viapo mbele ya Mungu then mnaendelea na uchafu wenu ndani ya ndoa......ila bora na huyo anajali,mingine inasahau hata kwamba inahatarisha maisha ya wake zao,inaweza waacha watoto yatima na kuwapa shida wale wote wanaomtegemea na kumtegemea huyo mama.......
The bad thing ni kuwa sasa hivi ni kitu cha kawaida.......halafu mbaya ni pale unapokutana na jianaume linalo-assume na wewe unacheat..:A S 20:

Hapo reaction yako ikoje ndugu? kama ndio yamakukuta ww. :popcorn:
 
Huyo mwanamke anatakiwa kupimwa akili.... kukuta kondom kwenye suruali ya mumewe ni jambo moja na kutembea nje ya ndoa ni jambo jingine. ni mambo tofauti hayo....LABDA ALIWEKEWA MFUKONI. amtende haki mumewe banaaa..:angry:

Sasa nimepigiwa simu kuwa mwanamke kaenda kumtafuta Daktari aliyedaiwa kutoa kondomu hizo. Sijui mambo yatakuwaje huko, na sijui reactipon ya mwanaume juu ya hilo!!! Nitawajuza nikizipata news!!!
 
Hapo reaction yako ikoje ndugu? kama ndio yamakukuta ww. :popcorn:

Mi napenda mtu awe mkweli,in case yamenikuta tuzungumze tu kwanza,manake kuna sababu ya yeye kwenda nje....lakini anapoleta uongo juu ya uongo eti anazuia mimba,akaenda kwa Dr akakuta zimebaki mbili....hapo hatutaelewana kabisa,hapo inaonekana hayuko tayari kukabiliana na tatizo lililopelekea kwenda nje bali yeye anaendelea na uongo wake,kwa minajili hiyo namruhusu aendelee ila atimize majukumu yake mengine,mi naye basi........:coffee:
 
heee!
Kumbe we mwanaume.

grapes_and_glass_image1.jpg

Cheers
 
Kama siyo wivu kwanini usiamini kuwa kweli kazitoa hospitali hizo kondomu????

Kama ishu ni kuzuia uzazi na mhusika ni mimi pia,tungekuwa tumeshirikishana na kuamua namna ya kupanga uzazi,nami hapo wala singeshtuka.........read between the lines ya excuse ya huyo mwanaume utanielewa.
 
kwani kondomu zenyewe zilikua aina gani raha,raffrider,dume, salama au mcd?
 
Kukutwa na condom mbili ni kosa,zingekuwa 3 wife angemuelewa,sasa alitegemea kutumia hizo mbili kwa siku ngapi si za siku moja tu ? Kuna jamaa alikutwa na condom mfukoni na alipoulizwa akadai kuna shindano Clouds radio watangazaji wanazunguka mitaani na anaekutwa na condom mfukoni anapewa laki 1 ndio maana anazo wife akakubali na kuomba akipata hiyo laki amgawie nusu hahaha! kuna watu wabunifu kweli hapa bongo.
 
kuna familia moja hapa niishipo ndoa yao imevunjika baada ya mwanamke kukuta pieces 2 za kondomu ndani ya suruali ya mume wake. Hadi sasa ni mwezi mmoja umepita tokea kizungumkuti hicho kitokee. Juhudi za kusuluhisha tatizo hilo zinaendelea nami nikiwemo, lakini bado mke hajaridhia kurudi. Je, wanajf huu ni wivu au ni umakini wa mwanamke ndani ya ndoa yake??? Nawasilisha!!! Karibu!!!

huyo mwanamke ana mikogo, mumewe anamlinda yeye analeta jeuri, si wanasema eti " ukimpenda utamlinda".

hicho kisa kimenikumbusha zamani kidogo mimi nilienda kwa boyfriend wangu mkoani kwa siku kadhaa, siku mbili kabla ya kuondoka nikiwa nachukua nguo zangu chafu kwenye kapu nifue,enheee chini kabisa nikazikuta ndomu boksi zima la msd,mimi na yeye tulikuwa hatutumii kwa kuwa tulikuwa na utaratibu wa kupima mara 3 kila mwaka as tulikuwa tunaishi mbalimbali, nilipomuuliza akadai ofini kwao walitembelewa na waelimishaji wa ukimwi na kila mtu akapewa boksi zima!???mwisho siku nikamwambia mungu asante ni;ivyoondoka ndio ukawa mwisho wa habari....
 
:clap2::clap2::clap2::clap2::coffee:
 
michelle usinicheke mwenzio!!yalinikuta nikashindwa hata kulia zaidi ya kujuta kilichonitoa kwetu hadi huko maporini then dahhhh

Nailyne wangu sijakucheka,tunapita kwingi,nimekupa makofi kwa kuchukua hatua nzuri.....yaani umenifurahisha sana....

Napenda watu wanaoona jambo then wanachukua uamuzi mapema kabla hayajawakuta makubwa zaidi.:coffee:
 
Back
Top Bottom