Kondomu Ndogo Kwaajili ya Watoto Zaingia Madukani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
4183762.jpg

Kondomu zenye ukubwa wa wastani zinadaiwa kuwa haziwatoshi ipasavyo vijana wenye umri mdogo
Kampuni kubwa ya kutengeneza kondomu ya Uswizi imetengeneza kondomu ndogo sana kwaajili ya watoto kuanzia umri wa miaka 12 kutokana na kile kinachosemwa kuwa watoto wa siku hizi wanaanza kufanya ngono mapema. Kondomu hizo zilizopewa jina la "Hotshot" ni maalumu kwa vijana wa kiume wenye umri mdogo kuanzia umri wa miaka 12 hadi miaka 14.

Kondomu hizo zilitengenezwa kufuatia hatua ya makundi ya uzazi wa mpango kusema kuwa vijana wenye umri mdogo hawapati kinga inayotakikana wakati wa kujamiiana.

Ilidaiwa kuwa vijana wa siku hizi wanaanza ngono mapema na hawatumii kinga na wala hawajui jinsi ya kujikinga na magonjwa yanayotokana na ufanyaji wa ngono zisizo salama.

Kondomu hizo zimeingia madukani nchini Uswizi na kuzua maoni tofauti toka kwa wazazi nchini Uswizi.

Taarifa ya utafiti uliofanyika kabla ya kutengenezwa kwa kondomu hizo ilionyesha kuhitajika kwa elimu ya mapema kwa vijana jinsi ya kujikinga na magonjwa ya zinaa pamoja na mimba zisizohitajika.

Msemaji wa kampuni ya Lamprecht AG iliyotengeneza kondomu hizo, alisema kuwa watakapoanza kuuza kondomu hizo nje ya nchi, Uingereza itapewa nafasi kubwa kutokana na idadi kubwa ya mimba za wasichana wenye umri mdogo.

Katika nchi za ulaya Uingereza inaoongoza kwa idadi kubwa ya wasichana wanaopata ujauzito kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.
 
Looh nimeishiwa maneno. Tunakoenda siko kabisa
 
Na wauze tu, si biashara? Ni kweli watoto wadogo wanaweza kukufundisha style za kujamiiana utashangaa. Sumni sumni wanazoiba kwenda kutizama kideo zinawasaidia kujifunza mambo mengi na wanahamasika kufanya practical. Kuwakataza kwa maneno tu haina tija, wataondoka na ukimwi. Bora kinga kuliko tiba ambayo after all haipo. Kwani watu wazima wangapi hujimegea bila condom ingawa wanajua athari zake? Wengi wakubwa tunaogopa kununua condom dukani, unaangalia kushoto na kulia kabla hujauliza bei ya "karanga" au "pipi" au "hiyo nanii".

Madhara yake tu ni kwamba watoto hawafundishwi shuleni kwa umri huo jinsi ya kuitunza miili yao kuepukana na magonjwa kadhaa. Miaka 12wako darasa la nne. Somo hilo ukiwapa ni kuwapelekea vichekesho tu. Ona nyumbani unashika remote control, DVD yako inapofika eneo fulani unaforward haraka, kisha unamsikia mtoto wako wa miaka mitano anakuambia, "baba, hapo wala sio pabaya sana, lakini mbele yake ndio wanafanya kweli". Unalo tena?
 
Itakuwa ukimtuma mtoto dukani akanunue unga kilo moja atanunua nusu na robo pease inayobaki nipe...'' naniiii ya watoto''. Kazi ipo
 
Kondomu hizo zilizopewa jina la "Hotshot" ni maalumu kwa vijana wa kiume wenye umri mdogo kuanzia umri wa miaka 12 hadi miaka 14.

Kondomu hizo zilitengenezwa kufuatia hatua ya makundi ya uzazi wa mpango kusema kuwa vijana wenye umri mdogo hawapati kinga inayotakikana wakati wa kujamiiana.

Ilidaiwa kuwa vijana wa siku hizi wanaanza ngono mapema na hawatumii kinga na wala hawajui jinsi ya kujikinga na magonjwa yanayotokana na ufanyaji wa ngono zisizo salama.

Kondomu hizo zimeingia madukani nchini Uswizi na kuzua maoni tofauti toka kwa wazazi nchini Uswizi.

Taarifa ya utafiti uliofanyika kabla ya kutengenezwa kwa kondomu hizo ilionyesha kuhitajika kwa elimu ya mapema kwa vijana jinsi ya kujikinga na magonjwa ya zinaa pamoja na mimba zisizohitajika.

Msemaji wa kampuni ya Lamprecht AG iliyotengeneza kondomu hizo, alisema kuwa watakapoanza kuuza kondomu hizo nje ya nchi, Uingereza itapewa nafasi kubwa kutokana na idadi kubwa ya mimba za wasichana wenye umri mdogo.

Katika nchi za ulaya Uingereza inaoongoza kwa idadi kubwa ya wasichana wanaopata ujauzito kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.
 
Wanaume (watu wazima) wa India walilalamika kuwa condoms haziwatoshi (zinawapwaya)
Na wakaomba watengenezaji wa bizaa hii wawapelekee saizi ndogo.
Nadhani hizo zingewafaa zaidi hao wahindi.
 
Madhara yake tu ni kwamba watoto hawafundishwi shuleni kwa umri huo jinsi ya kuitunza miili yao kuepukana na magonjwa kadhaa. Miaka 12wako darasa la nne. Somo hilo ukiwapa ni kuwapelekea vichekesho tu. Ona nyumbani unashika remote control, DVD yako inapofika eneo fulani unaforward haraka, kisha unamsikia mtoto wako wa miaka mitano anakuambia, "baba, hapo wala sio pabaya sana, lakini mbele yake ndio wanafanya kweli". Unalo tena?
sasa mkuu, wakitengenezewa condom ndo watajua?......root couse ni elimu. Kwa nini tunangoja hadi wafanyabiashara wa-take advantage ya kutopanga kwetu?

Nimeona vitabu vya sayansi vya tanzania shule ya msingi siku hizi, vina topics za Reproductive Health na HIV/AIDS kuanzia darasa la pili au la tatu kama sikosei. lakini details zinaongezeka as you progress to higher grades
 
Lkaini zikiletwa huku kwetu tusishangae watoto wakihamasihwa kwamba sasa nao waweza kujumika kwani wameletewa kinga yao! Hapo ndio hatari ya kuua kabisaa kizazi chetu!
 
mmeamua kuidhinisha ngono hadi kwa watoto wadogo? kuwapa zana ni kuwaambia - guys move on but remember the tools!

haya endeleeni ni soko huria ila matokeo yake mtayaona
 
jamani tukumbuke kwamba Africa ndio mdhaifu mkubwa wa ugonjwa wa ukimwi..ni wakati wetu kufunguka sasa na kuwa wazi kwa wanetu kuhusu elimu ya ugonjwa huu...watoto wanafanya mapenzi..tena wa kizazi hiki ndio hatari kabisa...wakati huo huo kuna watoto wanazaliwa na virus vya ukimwi..mzazi ni vigumu kujua mwanao anacheza na nani...cha muhimu mueleze, muelimishe na ikibidi mnunulie condom ili ajikinge...ni wakati wa kuacha utamaduni wa zamani ili kuweza kunusuru taifa letu....Tanzania bila ukimwi inawezekana
 
Back
Top Bottom