Komu aliuza ushindi wa Chadema Moshi Vijijini

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Kuna mazungumzo hapa moshi vijijini kwamba mawakala wa chadema wanaamini kwamba mgombea wao ndugu Komu aliuza ushindi wa chadema akidhani ulikuwa ushindi wake. Mawakala wote wanadai Komu aliongoza katika vituo vyote na wananchi walipigana kufa na kupona. Wanajilaumu kutokumlinda mgombea wao. Wamevunjika moyo sana. Ni usaliti unaokatisha wananchi tamaa
 
Nafikiri siku za usoni mgombea mwanamke wa Chadema asiwemo kwenye orodha ya viti maalum. Pia sheria za uchaguzi zioneshe wazi kuwa jina likiwa kwenye viti maalum basi kwenye majimbo lisiwemo na kinyume chake kwa vyama vyote nchini.
 
Mkuu sioni sababu ya kumtuhumu mtu bila kuwa na solid evidence. Watuambie ni vituo gani Komu alishinda
kwa kura ngapi na ni wapi Dr Chami alishinda/alishindwa tukiweza kupata hiyo idadi tumuiplicate.

Vinginevyo tutakuwa tunamtuhumu bure Komu. Itafurahishwa pia kupata udhibitisho kutoka kwenye chama
kama wanazo speculation zozote
 
Hamjui kilichoshindaniwa Moshi vijijini, hakukuwa na suala la CHADEMA na CCM, suala lilikuwa jingine tofauti kabisa.
 
Nafikiri siku za usoni mgombea mwanamke wa Chadema asiwemo kwenye orodha ya viti maalum. Pia sheria za uchaguzi zioneshe wazi kuwa jina likiwa kwenye viti maalum basi kwenye majimbo lisiwemo na kinyume chake kwa vyama vyote nchini.

Ndugu Mwanamayu angalia bandiko lako vizuri,Habari uliyoandika hapa haina ukweli,ama umeandika kwa bahati mbaya au umeandika kwa makusudi kuwapotosha wasomaji.Aliyegombea Ubunge Moshi Vijijini si Mwanamke.Anthony Calist Komu,ni Mwanaume pia ndiye Mkurugenzi wa Fedha wa Chadema na ndiye aliyegombea Ubunge Moshi Vijijini ,na alishindwa na Dr.Cyril Chami wa CCM.Katika maandiko yako labda umemchanganya Anthony na Anna Maulidah Komu ambaye aligombea Ubunge kwa Tiketi ya Chadema ktk Jimbo la Kigamboni,ambako Mgombea wa CCM Dr.Faustine Ndugulile alishinda.Fanya uhakiki vizuri wa vyanzo vyako vya habari zako kabla ya kutoa shutuma.
 
Kuna mazungumzo hapa moshi vijijini kwamba mawakala wa chadema wanaamini kwamba mgombea wao ndugu Komu aliuza ushindi wa chadema akidhani ulikuwa ushindi wake. Mawakala wote wanadai Komu aliongoza katika vituo vyote na wananchi walipigana kufa na kupona. Wanajilaumu kutokumlinda mgombea wao. Wamevunjika moyo sana. Ni usaliti unaokatisha wananchi tamaa

Source yako?

Evidence? La sivyo hapa si mahali pa majungu!!
 
Mkuu Kithuku, kumbe nini hicho cha sirini ambacho kiligombewa nasi hatukijui? Tujuze mkulu, tafadhali
 
A good case of political anthropology. Kama kuna anayependa hii fani akienda uchagani atapata data hadi atafurahi mwenyewe.

mbona mimi niko uchagani na sielewi inachoongea? kwa nini usisema?
 
Source yako?

Evidence? La sivyo hapa si mahali pa majungu!!

nilichelewa sana kuanzisha hii thread kwa sababu nilidhani ningeweza kupata data. watu walianza kulalamika kidogo kidogo. sasa hivi ni gumzo kila kona moshi vijijjini kwamba Komu aliuza nguvu za wananchi. mawakala 20 ambao nimeongea nao idadi ya kura waliyonayo inaonesha Komu kuongoza kwa zaidi ya kura 2000. lakini hii siyo sababu ya kusema kwamba alishinda, isipokuwa mawakala hao waliwasiliana na wenzao pia na wengi wanashangaa Chami alipata ushindi vituo gani.

chadema moshi vijijini watoe edadi ya kura katika kila kituo cha kupigia kura walizopokea kutoka kwa mawakala. kwa kuwa mawakala wanafahamiana na wanatumia simu, itakuwa rahisi kila wakala kuhakiki kama idadi ya kura zilizotolewa na Ofisi ya Chadema ndizo wakala huyo alizituma alizozituma. Hii itasaidia kurudisha imani kwa wananchi ambao sasa wanaamini wamedhulumiwa.

Hata baba yangu mwenye miaka 70 haamini kama Chami alishinda kwa idadi ya kura
 
Ilshasemwa humu kuna ubaguzi wa grade za uchaga huko kwenu, kuna mchaga wa uru na mchaga mkibosho, ni sawa na kwetu kule ukiwa mpogoro wa ulanga mashariki wewe ndie genuine(mvigoi) na ukiwa magharib unaitwa wa kuchonga (vidabaga)!!!!!!

Hahahaaaaaaaa kazi ipo acha julius kambarage nyerere apumzike kwa amani maana alijua tanganyika na unguja ndani na nje na maono yalimuonyesha kinachofuatia!!!!!!!!

Sasa iko haja ya kuwaangalia watu wa makabila tofauti na mikoa wanayotafutia mamlaka za kisiasa ili tujue kama ni genuine huko kwao au wa kuchonga?? Maana hilo liko kagera, mwanza ,musoma,moro, iringa, mby na n.k

mungu ibariki tanzania
 
ha ha ha hahh shikambaku FDR, umenikumbusha mbali sana!!
 
Ndugu Mwanamayu angalia bandiko lako vizuri,Habari uliyoandika hapa haina ukweli,ama umeandika kwa bahati mbaya au umeandika kwa makusudi kuwapotosha wasomaji.Aliyegombea Ubunge Moshi Vijijini si Mwanamke.Anthony Calist Komu,ni Mwanaume pia ndiye Mkurugenzi wa Fedha wa Chadema na ndiye aliyegombea Ubunge Moshi Vijijini ,na alishindwa na Dr.Cyril Chami wa CCM.Katika maandiko yako labda umemchanganya Anthony na Anna Maulidah Komu ambaye aligombea Ubunge kwa Tiketi ya Chadema ktk Jimbo la Kigamboni,ambako Mgombea wa CCM Dr.Faustine Ndugulile alishinda.Fanya uhakiki vizuri wa vyanzo vyako vya habari zako kabla ya kutoa shutuma.

safi sana, mpashe huyo
 
Nafikiri siku za usoni mgombea mwanamke wa Chadema asiwemo kwenye orodha ya viti maalum. Pia sheria za uchaguzi zioneshe wazi kuwa jina likiwa kwenye viti maalum basi kwenye majimbo lisiwemo na kinyume chake kwa vyama vyote nchini.
Mkuu hapo kwenye RED, fanya homework yako vzr. Huyo Komu mwanamke aligombea Kigamboni.
 
Back
Top Bottom