Komu aliuza ushindi wa Chadema Moshi Vijijini

komu alishindwa kwa kukosa kura za wakibosho anakotokea chami , komu ni muuru alipata kura za uru , old moshi , mbokomu na ukanda wa tambarare hao mawakala wa chadema waliokuwa kibosho waliepa na fomu za matokeo na walikuwa hawapatikani kwa simu ,kwa ninavyomfahamu komu ni mtu wa msimamo
 
nilichelewa sana kuanzisha hii thread kwa sababu nilidhani ningeweza kupata data. watu walianza kulalamika kidogo kidogo. sasa hivi ni gumzo kila kona moshi vijijjini kwamba Komu aliuza nguvu za wananchi. mawakala 20 ambao nimeongea nao idadi ya kura waliyonayo inaonesha Komu kuongoza kwa zaidi ya kura 2000. lakini hii siyo sababu ya kusema kwamba alishinda, isipokuwa mawakala hao waliwasiliana na wenzao pia na wengi wanashangaa Chami alipata ushindi vituo gani.

chadema moshi vijijini watoe edadi ya kura katika kila kituo cha kupigia kura walizopokea kutoka kwa mawakala. kwa kuwa mawakala wanafahamiana na wanatumia simu, itakuwa rahisi kila wakala kuhakiki kama idadi ya kura zilizotolewa na Ofisi ya Chadema ndizo wakala huyo alizituma alizozituma. Hii itasaidia kurudisha imani kwa wananchi ambao sasa wanaamini wamedhulumiwa.

Hata baba yangu mwenye miaka 70 haamini kama Chami alishinda kwa idadi ya kura

Naam hata mimi bado siamini kama JK ni rais wangu!

Sasa kama kulikua na malalamiko ya wazi mbona hatujasikia malalamiko yeyote toka kwa mgombea binafsi au Chama kwa ujumla?
Au ndo tuseme chama bado kinajipanga na kitakuja na solid evidence hapo baadae? ila hayo matokeo hata mimi yalinipa mshangao manake moshi vijijini sio mbumbumbu kiasi cha kuipigia kura ccm:nono::nono::nono::nono::nono::nono: kuna kauchakachuaji kalipita mahali
 
Zengwe hilo linaundwa taratibu. Hakuna evidence yeyote yakuthibitisha Komu aliuza ubunge. Kama ipo toa usibaki kubwabwaja tu pumba
 
Jamani wanainji tuongee kitu kama tuna ushaidi . Kama upo kweli hatua za kijeshi zichukuliwe dhidi yake.
 
Ndugu habari yako.Kabla hujaandika habari nzito kama hizi unatakiwa kwanza ukae chini na utafakari kwa kina.Inawezekana wewe unaona hili ni jambo dogo sana lakini kumbuka uancheza na maisha ya watu hapa.Hivi unamfahamu Komu au umesikia tu?Komu hawezi kuuza jimbo kwa kuwa anafahamu Ubunge is worth than any amount of money.Yaani apigane weee halafu mwishoni auze jimbo,haiwezekani.Jamani sio kila manchokisikia ni cha ukweli muwe mnajaribu kupambanua kwanza.Inasikitisha sana!!!!

MH.Regia[mb]....nimepita huko karibuni na nimesikia huu uvumi kwa watu wa kawaida kabisa.......,niliudharau na sikujuwa kuwa utafika huku....ushauri wangu kwenu ni huu.......lazima mjuwe kuwa ccm inatumia mfumo wa kipropaganda wa old east......kila baada ya uchaguzi huwa wanapenda kueneza propaganda za aina hii na kugombanisha wapinzani.....ili uchaguzi unafuatia wasiaminike......[angalia kazi waliyofanya baada ya mafanikio ya upinzani 1995,mjuwe kuwa tayari wameingia kazini]
wanaeneza uvumi kwa wananchi wa kawaida kuwa komu amehongwa milioni 400 na chami na system.
Uvumi wa aina hii pia ulienezwa wakati wa kampeni kwa Godbless Lema kuwa wananchi wasihangaike kwani hata akishinda atachukuwa pesa.....,kukawa na uvumi mwingine wa kumuhusidha muheshimiwa zitto kabwe na kujitowa kwa mpinzani wa NIMROD mkono.....hata pale mwanza kulikuwa na uvumi kuwa jimbo litauzwa......we have to understand these guys wanataka kuwagonganisha....

Ni muhimu uwashauri wagombea ubunge wote wa chadema wakisaidiwa na nyinyi wabunge na viongozi wengine kufanya ziara za kuwashukuru wananchi na kuwaeleza hali halisi[aidha walioshinda au kushindwa ...wote]...nimeona juzi gazetini Mpendazoe amefanya mkutano.....ni muhimu wote mfanye hivyo.....ili kujijengea imani kwa wananchi....tena kwa hili Komu na wengine wanatakiwa aanze haraka kuondoa huu uvumi ...na pale ambapo mnaona kuna ushahidi wa kutosha kwenda mahakaamani ..ni vema kuwaeleza wananchi hatua zitakazofuatia..na ikibidi kuwaomba michango ya hali na mali kuleta ukombozi wa ukweli....

Pia fuatilieni ...tunaelezwa kuwa wakurugenzi wa halmashauri ambazo CHADEMA mmeshinda wanahamishwa na kufukuzwa kazi....msipowapazia sauti kimataifa na kitaifa .....kura zenu zitaendelea kuchakachuliwa na wakurugenzi ili kulinda ajira zao......mkipaza sauti itasaidia kuwapa watendaji hawa uhuru kwenye utendaji wao...uhamisho na kufukuzana kazi baada ya uchaguzi ni batili....

Kule Arusha wanasema kuwa uhamisho wa Kamanda wao wa POLISI Basilio Matei....ulitokana na msimamo wake wa kukataa kusimamia kutangazwa Batilda kwa mabavu.........akiogopa damu kumwagika ..na aliwaeleza mazingira hayaruhusu......kamanda huyo pamoja na wengine wenye tatizo kama lake wamehamishwa ......pamoja na kuwa kuwa wengine waliostahili....bado nalo linatakiwa lipaziwe sauti ili watendaji wa serikali ...waweze kutenda kazi kwa uhuru siku zijazo........liangalieni hili kwa mapana na uzito wake!

Nawasilisha...
 
Chami na Komu walikuwa pamoja chuo kikuu Dar; inawezekana kabisa kuwa wangeweza kuelewana vizuri tu!! Fanyeni uchungzi kwani Chami was politically venerable this time around!!
 
HESHIMA KWAKO MKUU, Ushauri huu unabidi uzingatiwe sana! Hatua za haraka ni lazima zichukuliwe kama CHADEMA inataka kuendelea kuwa na nguvu ya ukombozi waliyo nayo. Kipindi hiki cha miaka mitano kitakuwa na majaribu makubwa sana. Ninachoogopa sana ni pale ambapo kutakuwa na roho zitakazoteketezwa kwa ajili ya kujaribu ku-achieve udhalimu wao. Mungu awawezeshe watu kuwa kamini sana.
 
kuna ukweli kuwa matokeo ya kata mbili ambazo zilimpa ushindi chami yalichakachuliwa. ushahidi unatafutwa na tunategemea komu ambaye yuko dodoma atakuwa moshi next week tayari kupeleka kesi mahakamani
 
Naam, tunashukuru sana. Hii inatia matumaini na nina imani watu wakiona angalau kuna jitihada kama hizi wataendelea kuwa na imani na chadema. Ukimya uliokuwa umetawala wakati wananchi wamekatishwa tamaa na matokeo ya nguvu zao huku kukiwa na hizo tuhuma za kuuza ushindi siyo haki na wala siyo namna bora ya kuisaidia chadema.

sidhani kama nakubaliana na wale wanaodhani kuwa kutosafisha tuhuma ndiko kuitakia mema chadema. wala sikubaliani na wale wanaotuhumu mtu anayewasilisha hisia za wananchi hapa ili zipate majibu. kumbe afanye nini kama anasikia haya maneno kutoka kila kona na kweli hana data. kuyapuuza siyo namna mzuri ya kuisaidia chadema.

nina imani kabisa Komu ameshasikia haya maneno sana, na uongozi wa chadema mkoa wa kilimanjaro pia wamesikia. kwa wale tunaoishi moshi haya siyo maneno ya kubisha. tulisubiri kwa muda mrefu mno kauli au action ya ama Komu au Chadema lakini hatukupata. Ningefurahi sana kama hali kama hii haitajirudia tena maeneo mengine. Mbona hata Mpendazoe anafurukuta?

tunasubiri hiyo court action na sisi wengine tuko tayari kuchangia gharama, hatupendi hii aibu ya jimbo moja tu la wachaga kuchagua ccm!
 
kuna ukweli kuwa matokeo ya kata mbili ambazo zilimpa ushindi chami yalichakachuliwa. ushahidi unatafutwa na tunategemea komu ambaye yuko dodoma atakuwa moshi next week tayari kupeleka kesi mahakamani

Mkuu Mwikimbi,

heshima kubwa kwako mkuu. wiki zimepita mkuu tunaomba updates angalau
 
Kuna mazungumzo hapa moshi vijijini kwamba mawakala wa chadema wanaamini kwamba mgombea wao ndugu Komu aliuza ushindi wa chadema akidhani ulikuwa ushindi wake. Mawakala wote wanadai Komu aliongoza katika vituo vyote na wananchi walipigana kufa na kupona. Wanajilaumu kutokumlinda mgombea wao. Wamevunjika moyo sana. Ni usaliti unaokatisha wananchi tamaa

Thats a political gonorrhea being spreaded to devalue Mr A.Komu.....Kwa hiyo maneno yaliyojaa mitaani kwamba Halima Mdee alitaka kupokea Rushwa ya Mil 600 ila akaogopa Jeshi la watu lililokaa pale nje kawe ni kweli....Yaliyotapakaa kuhusu Shitambala kwamba kauza ushindi ni kweli?...na wanaodai kwamba wenje alitaka kupewa Mil 800 ili amwachie nafasi mwamba wa vitambulisho ni kweli? Hapa nipo Marangu maeneo ya samanga hakuna UMAJINUNI kama huo.
 
Mkuu Mwikimbi,

heshima kubwa kwako mkuu. wiki zimepita mkuu tunaomba updates angalau
kuna hali ya kutatanisha, mpaka jana kesi ilikuwa bado haijaenda mahakamni, licha ya kwamba draft ilikuwa tayari. kuna mtu anaitwaa akwilini chuwa ni lazima abanwe kisawasawa. kuna ukweli kuwa chami yuko moshi akijitaidi kuzuia kesi hii isiende mahakamani,, eti kuupoteza uwaziri wake ni sawa na kuwapotezea muda wananchi wa moshi . akwilini chuwa alizima simu jana siku nzima, komu ambaye yuko hanang au karatu amerudi moshi haraka kujua kulikoni? akwilini chuwa ni kiongozi wa chadema ngazi ya mkoa, msisahau pia ni mkibosho sawa na chami,sasa ukibosho sijui unaingilia hapa?
 
Duh! nyuzi nyingine bana zinatunyima haki tusio na habari za ndani kuchangia. Hata hivyo bado Watanzania tuna safari ndefu. Wengine tulijua wachaga ni wachaga tena ni watu wa mantiki tu; kumbe kuna makabila mengi ivo na yenye kulinda himaya zake! Mbona kazi ipo?
 
kuna hali ya kutatanisha, mpaka jana kesi ilikuwa bado haijaenda mahakamni, licha ya kwamba draft ilikuwa tayari. kuna mtu anaitwaa akwilini chuwa ni lazima abanwe kisawasawa. kuna ukweli kuwa chami yuko moshi akijitaidi kuzuia kesi hii isiende mahakamani,, eti kuupoteza uwaziri wake ni sawa na kuwapotezea muda wananchi wa moshi . akwilini chuwa alizima simu jana siku nzima, komu ambaye yuko hanang au karatu amerudi moshi haraka kujua kulikoni? akwilini chuwa ni kiongozi wa chadema ngazi ya mkoa, msisahau pia ni mkibosho sawa na chami,sasa ukibosho sijui unaingilia hapa?

Nilipoanzisha hii thread watu walinishambulia sana. Sasa ukweli unajiweka sawa wenyewe. Kama siyo Komu basi kuna mtu au watu ndani ya Chadema walikula. Kwenye magazeti leo Chami anaonekana alikuwa Arusha jana, lakini nilijua tu ni njia ya kuwa karibu na hilo swala ili alidhibiti. Ndiyo maana nikafufua hii thread.

nadhani wanaodai ukabila hapa wanakosea. wakibosho ndio wana hasira kuliko wauru. hawampendi chami, kuna ushahidi wa kimazingira kwamba hawakumchagua.

Pia nadhani ndiyo maana Chami amepewa uwaziri kamili ili kuwaringishia wachaga wa sehemu nyingine ambao wamechagua wapinzani. Lakini inajulikana kwamba uwaziri siyo maisha bora kwa wapiga kura, ni semina tu kwa wanachama wa ccm.

Mkuu Mwikimbi tujuze zaidi yanayojiri please
 
du kwa hili chadema fanyeni kazi ya ziada mimi ni mwanajimbo hilo wiki iyopita mama alikuwa hapa dar nijaribu kumdodosa kuhusu hili haonyeshi kama mr A KOMU kauza jimbo ila wanajiuliza chami kashindaje?Mama ni mtu potential pale kwenye serikal ya kijiji kwa hiyo anavijitaarifa vya kuchoshwa vya wanakijiji wenzake.
 
Nashukuru sana, hii hali ambayo wakibosho wanashitumiwa au kisingiziwa ukabila wakati wao wanajua walichagua Chadema ndiyo ilinifanya nianzishe hii thread bila kuwa na ushahidi wa kisayansi. Wakibosho wameudhika sana na hizi shutuma za uongo. Hawa watu wa vijijini hata hawajui blog ni nini na radio na magazeti hazijawahi kuripoti taarifa zao. Wakibosho wameduwaa kwamba chami kachaguliwa na nani
 
naendelea kmsaka mr. komu kawasili moshi jioni hii, nimemhakikishia kuwa asifanye ajizi. tuko hapa tunafuatilia kulikoni , habari njema kuwa nyimbo yuko busy kufungua matawi ya chadema kule njombe ni fundisho tosha huko moshi vijijini. simu ya komu ni 0713 615603
 
najua chami unasoma hapa, wewe ni kibaraka wa ccm , na haujulikani msimamo wako uko wapi, aidha unaunga mkono mafisadi au hapana, nakumbuka wewe ni kibaraka tangu pale uru seminary, hatukuhitaji katika ukombozi wa pili wa taifa letu. endelea kumwita chenge na lowasa kaka.
 
Back
Top Bottom