Komredi Polepole: Tunahitaji Katiba itakayosimamia Mifumo siyo itakayomtegemea Mtu mmoja

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,532
141,334
Mbunge wa viti maalumu komredi Polepole amesema muda ukifika tutahitaji Katiba inayosimamia mifumo na siyo inayomtegemea mtu mmoja.

Polepole alikuwa akijibu swali la mtangazaji nguli barani Afrika Aloyce Nyanda aliyetaka kujua maoni yake kuhusu katiba mpya.

Polepole amesema ni lazima tuwe na viongozi wanaoheshimu na kuiishi katiba ndipo wananchi watakuwa na furaha ya kweli ndani ya nchi yao.

Polepole amesema kuna nchi duniani katiba zao hazijaandikwa popote lakini viongozi wao wanaziishi hizo katiba

Chanzo: Star tv!
 
Polepole atulie kwenye lengo lake la mwanzo, akitoka nje ya hapo atajichanganya achekwe, anatakiwa ajue aongee kitu wakati gani, vile alivyowahi kuvipinga siku za nyuma kwasasa asithubutu kuvigusa.
 
Slipinga katiba mpya?
 
Mbunge wa viti maalumu komredi Polepole amesema muda ukifika tutahitaji Katiba inayosimamia mifumo na siyo inayomtegemea mtu mmoja.

Polepole alikuwa akijibu swali la mtangazaji nguli barani Afrika Aloyce Nyanda aliyetaka kujua maoni yake kuhusu katiba mpya.

Polepole amesema ni lazima tuwe na viongozi wanaoheshimu na kuiishi katiba ndipo wananchi watakuwa na furaha ya kweli ndani ya nchi yao.

Polepole amesema kuna nchi duniani katiba zao hazijaandikwa popote lakini viongozi wao wanaziishi hizo katiba

Source: Star tv!

Heko kwake, lakini maneno yake kabla ya kuyasema ni vyema atuambie ananyumbulika/undergo factory resetting mara ngapi hasa??
Kwa sababu:

1: Polepole wa katiba mpya si yule wa leo si wa kabla ya katiba mpya.
2: Polepole wa Magu session si huyu pia wa sasa, wala katiba mpya.
3: Polepole wa awamu ya sita, si yule wa katiba mpya, si wa Magu.
4: Je tutarajie mwingine ajaeee!!!??
 
Mbunge wa viti maalumu komredi Polepole amesema muda ukifika tutahitaji Katiba inayosimamia mifumo na siyo inayomtegemea mtu mmoja.

Polepole alikuwa akijibu swali la mtangazaji nguli barani Afrika Aloyce Nyanda aliyetaka kujua maoni yake kuhusu katiba mpya.

Polepole amesema ni lazima tuwe na viongozi wanaoheshimu na kuiishi katiba ndipo wananchi watakuwa na furaha ya kweli ndani ya nchi yao.

Polepole amesema kuna nchi duniani katiba zao hazijaandikwa popote lakini viongozi wao wanaziishi hizo katiba

Source: Star tv!
Wakati wa hayati JPM alisema hamna haja ya katiba mpya.
 
Back
Top Bottom