Kompyuta yenye siri za kikosi cha kumlinda Rais wa Marekani yaibwa

Iyegu

JF-Expert Member
Jun 16, 2014
6,276
12,397
Kompyuta ya kikosi cha kumlinda rais wa Marekani
inayoripotiwa kuwa na michoro ya jumba la Trump
Tower, na taarifa zingine za siri imeibwa kutoka
kwa gari la afisa mmoja mjini New York.
Hata hivyo kikosi hicho cha kumlinda rais kinasema
kuwa kompyuta hiyo huikuwa na taarifa za siri.
Lakini wanasema kuwa ina taarifa kuhus uchunguzi wa aliyekuwa mgomea wa Democratic Hillary Clinton kutumia barua pepe ya kibinafsi.
Kwa sasa polisi wanachunguza kamera za siri kuweza kumnasa mtu aliyeiba
Shirika la ABC lilisema kwa gari la ajenti lililengwa katika eneo la Bath Beach kwenye mtaa wa
Brooklyn.
CBS nayo ilisema kuwa kampyuta hiyo ilikuwa na taarifa muhimu kumhusu Papa Francis
Taarifa za polisi zililiambia gazeti la The York DailyNews, kuwa taarifa zilizo kwenye kompyuta hiyo ni
za siri kubwa.
Kompyuta hiyo inaripotiwa kuibwa kutoka kwa mkoba uliokuwa ndani ya gari. Mkoba huo hata hivyo umepatikana lakini kompyuta yenyewe bado
inatafutwa.

BBC
 
Mkuu huu mwandiko wako na jinsi unavyo elezea mada zako unafanana na jamaa mmoja picha yake anatoa hutuba na ana demu aliyefunga kitambaa.
 
Siri za vatican zitapatikana mtaani sasa, ila atakayezitoa sijui kama atabaki salama
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom