Kombora moja kutoka iran lapiga syria na kuua magaidi 50 kwa mpigo

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,395
2,000
Duru katika medani za vita zimetangaza kuwa zaidi ya magaidi 50 wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) waliangamizwa baada ya kombora moja kati ya sita ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kulenga kamandi ya kijeshi ya kundi hilo katika mji wa Al-Mayadin ulioko kwenye viunga vya Deir Ezzor mashariki mwa Syria.
Kanali ya televisheni ya Al-Alam imeripoti kuwa magaidi sita miongoni mwa walioangamizwa walikuwa raia wa Libya.
Aidha makamanda kadhaa wa kundi la kigaidi la Daesh akiwemo Abu Asim Al-Libi, na Abdulqadir Al-Farani, maarufu kwa lakabu ya Abu Harith nao pia wameangamizwa na kombora hilo.
Hadi sasa hakuna taarifa rasmi zilizotolewa kuhusu maafa yaliyosababishwa na makombora mengine matano yaliyofyatuliwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ambayo yalilenga kwa umakini shabaha iliyokusudiwa kwenye kamandi ya magaidi wa kundi la kitakfiri la Daesh katika eneo la Deir Ezzor nchini Syria.
Siku ya Jumapili usiku, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu liliishambulia kwa makombora sita ya masafa ya kati ya ardhini kwa ardhini kamandi ya kijeshi ya magaidi wa kitakfiri wa Daesh (ISIS) katika eneo la Deir Ezzor mashariki mwa Syria kwa lengo la kuwatia adabu magaidi hao wa kitakfiri.
Makombora hayo yaliyorushwa kupitia anga ya Iraq na kukata masafa ya kilomita 650 yalilenga kwa umakini shabaha zilizokusudiwa katika eneo la Deir Ezzor ndani ya ardhi ya Syria.
Kufuatia jinai ya kigaidi iliyofanywa tarehe 7 ya mwezi huu wa Juni hapa mjini Tehran na kusababisha kuuawa shahidi kimadhulumu watu 18 waliokuwa na saumu na kujeruhiwa wengine 52, jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran lilitangaza kuwa halitoruhusu kumwagwa damu takasifu pasina kutoa jibu kwa umwagaji damu huo...
Source parstoday
 

Dragoon

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
7,027
2,000
Hahahaaaaaaaaaaaaaaa!
Nimeipenda sana hii habari, nilijua tu.
Leo nitakaka unono...
teh teh teh :D:D:D
safi sana
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
14,251
2,000
Nategemea mashambulizi ya kutosha kabisa ndani ya ardhi ya Iran kwa siku za usoni. Iran sio mahali salama tena kwenda; watanzania mchukue tahadhari.
 

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
11,730
2,000
Kitu wasichokijua wengi ni kwamba kunachoendelea kati ya Iran na Marekani ni Drama tu... Marekani ndiye aliyeiweka madarakani hiyo serikali ya kiislam ya Iran na ndiye atakayeiondoa muda ukifika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom