Kombora la Mengi lamtikisa Rostam

Msindima

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,018
33
2009-05-04 17:12:52
Na Waandishi Wetu


Makombora dhidi ya mafisadi papa yaliyofyatuliwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, yamemtikisa Mbunge.

wa Igunga wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rostam Aziz na jana amejitokeza hadharani kumshambulia Mwenyekiti huyo, bila kujibu tuhuma zilizotajwa juu yake.
Rostam ambaye awali alisema amepuuza makombora ya Mengi kwa madai kuwa ni porojo, amedai kuwa baada ya kujadiliana na wenzake ameamua kujibu shutuma hizo.

Katika majibu yake, Rostam alijaribu kuzigeuza shutuma dhidi yake kama malumbano ya kisiasa, pale aliposema kwamba yeye sio fisadi papa, ila Mengi ndiye fisadi nyangumi.

Akifafanua, Mbunge huyo alisema kuwa Mengi amekopa kwenye taasisi mbalimbali za fedha tangu mwaka 1980, lakini amekuwa akikwepa kurejesha madeni kwa njia za kijanja kijanja, zikiwamo za kuua makampuni yake.

Rostam aliendelea kusema kuwa Mengi alikopa fedha nyingi kupitia nchi wafadhili, ambazo zilitolewa kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara nchini ili waweze kuagiza bidhaa nje maarufu kama Commodity Import Support, ambazo hakuzilipa hadi leo.

Hata hivyo, wakati Rostam anamtuhumu Mengi kwamba alikopa, mwenyewe anatuhumiwa kwamba alipora Sh bilioni 40 katika Akauti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kutumia kampuni `feki` ya Kagoda.

Akijaribu kujihami mapema kuhusu ukweli wa Mengi kulipa madeni au la, Rostam alidai Mwenyekiti huyo ameshirikiana na maafisa wa serikali kupitia Hazina `kutengeneza` makabrasha yanayoonyesha kwamba amelipa madeni yote na kwamba hadaiwi.

Mbunge huyo hakuwa tayari kuwataja maafisa wa Hazina walioshirikiana na Mengi, badala yake akaomba ufanyike uchunguzi.

Katika hali ya kushangaza, Rostam alikiri kwamba hata yeye bado hajakamilisha kulipa madeni ya Commodity Import Support.

``Wengi tulikopa na tunaendelea kulipa,, `` alisema Rostam.
Hata hivyo, alishindwa kufafanua kwamba anaposema ``Wengi tulikopa`` alikuwa anawawakilisha kina nani.

Rostam alidai Mengi ametoa shutuma za ufisadi papa dhidi yake kwa vile ni mbaguzi mwenye fitina, ubinafsi, chuki, wivu na uroho.

Katika mkutano huo, Rostam hakuweza kabisa kujibu hoja za Mengi badala yake ameeleza yale ambayo yamekuwa yakiandikwa kwa njia ya upotoshaji na magazeti yanayofadhiliwa na mafisadi akiwamo yeye (Rostam).

Wakati Rostam akitumia muda mwingi kuhoji uhalali wa Mengi kumtuhumu na kumwita fisadi papa, yeye alishindwa kueleza uhalali wake wa kumtuhumu na kumwita fisadi nyangumi.

Baadaye alipoulizwa ni vipi alitumia staili ile ile ya Mengi kujibu mapigo, Rostam alidai nia yake haikuwa hiyo, bali ameamua kufanya hivyo ili kuweka rekodi sawa.

Akijibu tuhuma hizo, Mengi alisema mafisadi wana uwezo mkubwa sana, sio tu kwa kuiba mali za umma, bali hata kwa kutunga uongo kama alivyofanya Rostam.

``Naomba nimpe Rostam Aziz ushauri wa bure, kama kweli anataka kujisafisha ama kuondokana na shutuma zinazomkabili za ufisadi aende Mahakamani, ikiwezekana hata kesho asubuhi (leo),`` alisema Mengi na kuongeza kuwa:
``Hata baada ya kukutana na vyombo vya habari jana, hoja ya kushutumiwa kama fisadi papa inabaki pale pale.

Watanzania wana hamu kubwa ya kusikia Rostam Aziz anakwenda mahakamani kwa sababu wengi hata wanyonge wana hasira nyingi dhidi ya mafisadi.``

Akizungumza katika hafla ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani jijini Dar es Salaam jana, Spika wa Bunge, Samuel Sitta alisema kuna kundi la watu wachache wanaoitafuna nchi.

Sitta alisema lazima Tanzania iachane na mfumo ambao watu wachache wanaitafuna nchi kwa manufaa yao binafsi na kuwaacha wengine wakizidi kuwa maskini.

Alisema bila kupambana na mafisadi nchi haitaweza kuendelea badala yake itakuwa kama mtoto mdogo mwenye utapiamlo (kwashakoo).

Alipoulizwa kuhusu kauli ya Mengi kuwashutumu mafisadi papa, Sitta alisema kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake na kwamba mtu akifichua maovu si tatizo.
  • SOURCE: Nipashe
 
Hakuna Mtanzania asiyejua kuwa ufisadi unaathiri watu jamii na nchi kwa ujumla. sasa nikisikia vikundi vya watu wakitoka hadharani kumtetea mtu amabye dunia nzima inamjua kuwa ni fisadi najiuliza kama kweli hawa watu wanaelewa wanachokifanya yaani usaliti wanaoufanya dhidi ya watanzania wenzao wanaoteseka kwa kukosa huduma muhimu kwa sababu ya wizi unaofanywa na mafisadi! leo hii kweli kuna mtu anaweza kuwatetea kina Manji, Rostam, Tannil Sommaiya na wengine wote waliotajwa na Mengi na wale ambao hawajatajwa? Report za madhambi yao ziko wazi nyingine mpaka Ulaya halafu eti kikundi cahe vijana kinawatetea kisa nini wanapewa posho na T Shirts jamani amkeni mnauza nasfi zenu kwa hawa mafisadi! Fikirieni ndugu zenu!
 
Shukrani sana Mzee Mengi kwa kumfanya bubu asema,sasa akajibu mahakamani alikuwa wapi 1994 asipeleke tuhuma alizotoa juzi.Aeleze biashara zake ni zipi na za kampuni gani.Asituletee maigizo kwa hosea aliyeitetea Richmond hadi hata Mwanasheria kama Slaa akaamua kupeleke mashitaka ya EPA kwa Umma.
 
Back
Top Bottom