Kombe la Shirikisho: Yanga yaanza vibaya kwa kukubali kufungwa 2 -1 dhidi ya Pyramids ndani ya CCM Kirumba

DonDonald

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,528
2,703
Mabingwa wa kihistoria nchini, Dar es Salaam Young Africa al maarufu kwa jina la Yanga wanaingia uwanjani leo kupambana na timu ya soka ya Pyramids ya kutoka nchini Misri katika mechi ya kwanza ya mtoano kutafuta nafasi ya kuingia kwenye hatua ya makundi kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho.

Kila la heri wawakilishi wetu wa Tanzania.

Kikosi cha Yanga

Farouk Shikalo
Juma Abdul
Ally Mtoni
Kelvin Yondani
Alli Alli
Feisal Salum
Mrisho Ngasa
Makame Rashidi
Sadney Urikhob
Pappy Tshishimbi
Mapinduzi Balama

UPDATES

Mpira umeanza

5" Yanga 0 - 0 Pyramids

10" Ally Mtoni anapiga shuti kali, golikipa wa Pyramids anaokoa

12" Pyramids wanashambulia lango la Yanga

15" Yanga 0 - 0 Pyramids ---- hawa Pyramids ni warefu na wana miili mikubwa kuliko wachezaji wengi wa Yanga

20" Yanga 0 - 0 Pyramids ---- Yanga wanapata foul baada ya Juma Abdul kufanyiwa rafu; Yanga wanapoteza

22" Yanga wanakosa goli hapa, Ally Ally anapiga kichwa ila namna gani anapiga nje

25" Yanga 0 - 0 Pyramids ---- Mrisho Ngasa anapewa kadi ya njano

35" Yanga 0 - 0 Pyramids ----- Pyramids wanakosa goli hapa

40" Yanga 0 - 0 Pyramids

42" Goal; Pyramids wanapata goli la kwanza kupitia kwa Eric Traore

45" Yanga 0 - 1 Pyramids (Eric Traore)

Mapumziko: Yanga 0 - 1 Pyramids

Second Half

46" Yanga 0 - 1 Pyramids

50" Yanga 0 - 1 Pyramids ---- Yanga wameanza kipindi cha pili kwa kasi; mchezaji mmoja wa Pyramids anapewa kadi ya njano kwa kuchelewesha muda

53" Yanga 0 - 1 Pyramids --- Fei Toto anapiga mpira lakini kipa wa Pyramids anaokoa na kuwa kona

64" Goal; Pyramids wanapata goli la pili kwa kupitia Mohamed

65" Yanga 0 - 2 Pyramids (Traore, Mohamed)

70" YANGA wanafanya mabadiliko, anaingia Kaseke anatoka Ngasa

68" Yanga 0 - 2 Pyramids ---- Yanga wanafanya mabadiliko anaingia Balinya anatoka Fei Toto

70" Yanga wanafanya mabadiliko anatoka Ngasa anaingia Kaseke

75" Yanga 0 - 2 Pyramids (Traore, Mohamed)

80" Yanga 0 - 2 Pyramids (Traore, Mohamed)

85" Yanga wanafanya mabadiliko anaingia Sibomana anatoka Makame

86" Yanga 0 -2 Pyramids

88" Goal; Tshishimbi anaifungia Yanga goli la Kwanza

88" Yanga 1 - 2 Pyramids

90" Zimeongezwa dakika 5

"92 Red Card; Kelvin Yondani anapewa kadi nyekundu kwa kucheza rafu

95" Yanga 1 - 2 Pyramids

Mpira Umekwisha

Timu ya Yanga imepoteza mechi ya kwanza dhidi ya Pyramids kwa kufungwa goli 2-1, timu hizo zitarudiana ili kupata mshindi atakayeingia kucheza hatua ya makundi

Mashabiki Wanafanya Fujo: Baadhi ya mashabiki wa Yanga wanafanya fujo hapa uwanjani kwa kurusha chupa kuelekea sehemu waliyokaa viongozi wa Yanga
 
Yanga wanacheza hawajui wanataka nn,timu km ya bonanza na mechi kama ya bonanza.Hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom