Kombe la Mataifa ya Africa (AFCON) kutofanyikia tena Cameroon kufuatia tishio la ugaidi

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,260
2,000
Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 iliyopangwa kufanyikia nchini Cameroon, haitofanyika tena nchini humo kutokana na sababu za kiusalama.

Kikao cha Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kimefikia uamuzi wa kuiengua nchi hiyo kuhodhi mashindano hayo makubwa Afrika kufuatia kuwepo kwa mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa kundi la kigaidi la Boko Haram na mgogoro baina ya Jeshi na makundi ya wananchi waliojitenga katika maeneo tofauti nchini humo.

Katika taarifa yake, kikosi cha usalama cha CAF kimesema kuwa kimejiridhisha kwamba hali ya usalama nchini Cameroon hairidhishi na huenda ikatia doa michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Kufuatia uamuzi huo, CAF imetoa fursa kwa nchi nyingine kutuma maombi ya kupewa kibali cha kuhodhi michuano hiyo ambayo imepangwa kufanyika mwezi Juni na Julai mwaka 2019.

Nchi itakayofanikiwa kupata kibali itatangazwa kufikia tarehe 31, Desemba 2018.
========


OFFICIAL: Cameroon will not host 2019 Africa Cup of Nations

  • The hosting of the Afcon was part of the agenda in the Caf Extraordinary Executive Committee meeting held in Accra, Ghana on Friday
  • Caf will now invite countries to submit official bids to host the tournament in June after ruling that Cameroon will not be allowed to appeal
  • The new host will be decided by December 31
It's official! Cameroon has been stripped of the rights to host the 2019 Africa Cup of Nations (Afcon).

"Today, the @CAF_Online Executive Committee met in Accra, Ghana and has decided that @FecafootOfficie could not host the 2019 Total Africa Cup of Nations," read a tweet from the official Confederation of African Football (Caf) Twitter handle on Friday.

The hosting of the Afcon was part of the agenda in the Caf Extraordinary Executive Committee meeting held in Accra, Ghana on Friday.Two reports that were key to the final decision regarding Cameroon were tabled namely; report of inspection visits of the security committee from October 27 to November 1 and a report of the inspection visit from November 11-15.

"After significant debate and having received detailed updates from numerous inspection visits over nearly 18 months, CAF has noted that a number of compliance conditions have not been met. In addition, after having heard from representatives of the governmental and sports authorities of Cameroon, and reviewed the latest progress on preparations, CAF notes the gap between the requirements of hosting the AFCON and realities on the ground," began the statement from Caf.

Cameroon is experiencing a tense security situation with persistent attacks by Boko Haram jihadists in the north and a conflict between the army and separatists in the two English-speaking regions.

"Furthermore, after hearing the conclusions of the CAF Security Inspection Team during their most recent visit to Cameroon, CAF concludes that the Africa Cup of Nations could not be exposed to any issues that could impact on the success of the most prestigious African competition."

After having considered that a simple postponement of the tournament was impossible because of CAF’s contractual commitments, and the importance of maintaining the competition calendar, the CAF Executive Committee decided that the next edition of the 2019 Africa Cup of Nations could not be held in Cameroon," read another part of the statement.

CAF will now invite countries to submit official bids to host the tournament in June 15-July 13 after ruling that Cameroon will not be allowed to appeal. The new host will be decided by December 31.

Source >> OFFICIAL: Cameroon will not host 2019 Africa Cup of Nations
 

Saharavoice

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,244
2,000
East Africa waombe waandae kwa pamoja. Tanzania kuna viwanja vitatu vya kimataifa kabisa ambavyo viko Dar, Kenya nadhani kimoja au viwili, kuna uwanja wa Aman Zanzibar ingawa sina uhakika kama unakidhi viwango kwa uzuri, Uganda pia.

Viwanja vinatosha bana.
 

Mkorintho wa 6

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
270
500
East Africa waombe waandae kwa pamoja. Tanzania kuna viwanja vitatu vya kimataifa kabisa ambavyo viko Dar, Kenya nadhani kimoja au viwili, kuna uwanja wa Aman Zanzibar ingawa sina uhakika kama unakidhi viwango kwa uzuri, Uganda pia.

Viwanja vinatosha bana.
Umesahau Kenya kwamba wanasumbuliwa na Al-shaabab mara kwa mara tena wao hupigwa vibaya mno na wanapenda kupiga makundi ya watu.

Kwa Africa mashariki tusahau kabisa habari za mashindano kuja kwetu.Bongo viwanja havitoshi
 

Saharavoice

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,244
2,000
Umesahau Kenya kwamba wanasumbuliwa na Al-shaabab mara kwa mara tena wao hupigwa vibaya mno na wanapenda kupiga makundi ya watu.

Kwa Africa mashariki tusahau kabisa habari za mashindano kuja kwetu.Bongo viwanja havitoshi
Unadhani wapi hakuna magaidi? maana kaskazini kuna IS, Magharibi Boko Haramu, Centre hali haijatulia kisiasa kukiwa rebels kibao. labda huko South Africa
 

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
4,930
2,000
Tz tuna viwanja vichache sana. Viwanja bora tz ni vinne au vitano ukijumlisha na ule wa mandela rukwa ukiboreshwa uko safi.
Kenya alshabab hakufai kabisa. Haya makundi ya kiislam ni taabu sana.
 

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
16,868
2,000
Tz tuna viwanja vichache sana. Viwanja bora tz ni vinne au vitano ukijumlisha na ule wa mandela rukwa ukiboreshwa uko safi.
Kenya alshabab hakufai kabisa. Haya makundi ya kiislam ni taabu sana.
Acha utani Mkuu Uwanja wa Mandela unatofauti gani na Viwanja kama Lake Tanganyika Kigoma,ule wa Katavi Mpanda, na hata ule Jamhuri Morogoro?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom