Kombe La Mapinduzi 2017: Historia, ratiba za bingwa wa kihistoria.

sembo

JF-Expert Member
May 25, 2011
4,350
3,451
Ikiwa leo Kombe La Mapinduzi ndiyo linakata utepe.. namleta kwenu mbabe wa kombe hili [bingwa wa kihistoria wa Kombe hili].. Simba SC.

Kombe hili mpaka sasa tangu limeanzishwa lina miaka 10. Mabingwa wa hili kombe tangu lianzishwe mnamo mwaka 2007, ni kama ifuatavyo;

ORODHA YA MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI.
2007...1. Yanga SC 2. Mtibwa Sugar
2008...1. Simba SC 2. Mtibwa Sugar
2009...1. Miembeni 2. KMKM
2010...1. Mtibwa Sugar 2. Ocean View
2011...1. Simba SC 2. Yanga SC
2012...1. Azam FC 2. Simba SC
2013...1. Azam FC 2. Tusker FC
2014...1. KCCA 2. Simba SC
2015...1. Simba SC 2. Mtibwa Sugar
2016...1. URA 2. Mtibwa Sugar

Kwa matokeo hayo tunaona, Bingwa wa kihistoria Simba SC katwaa mwali huyu mara 3, anayemfuatia akiwa ni Azam katwaa mara 2.. na wale ndugu zetu Yanga wakiambulia mara 1 tu [kumbukumbu zangu zinaonesha walishinda kimazabe sana].

Katika michuano hii inayoanza tarehe 30.12.2016, Mnyama Simba SC amepangwa kundi A akiwa na timu zifuatazo; URA, KVZ, Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys.

RATIBA KAMILI YA MAPINDUZI CUP kwa Timu ya Simba SC kuanzia hatua ya makundi hadi tutakapokabidhiwa kombe letu mnamo 13.01.2017 ni kama ifuatavyo;

01.01.2017 Simba SC vs Taifa ya Jang’ombe saa 02:30 usiku.

03.01.2017 KVZ vs Simba SC saa 02:30 usiku.

05.01.2017 Simba SC vs URA saa 02:30 usiku.

08.01.2017 Simba SC vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri.

10.01.2017 Nusu fainali ya kwanza.. saa 10:00 [ Simba SC vs .......]

13.01.2017 Fainali.. saa 02:30 usiku. [ Simba SC vs ......]

ANGALIZO: Mnyama yu serious kabisa na hili kombe.. Zanzibar tunakuja kumchukua mwali wetu tuliyempoteza mwaka huu (2016).
 
Wasindikizaji wengine wa michuano hii wapo kundi B.. ambalo lina timu za Yanga, Azam, Zimamoto na Jamhuri.

RATIBA KAMILI YA MAPINDUZI CUP 2017.

30/12/2016 Taifa ya Jang’ombe vs Jang’ombe boys saa 2:30 usiku.

1/1/2017 KVZ VS URA Saa 10:00 alasiri, Simba vs Taifa ya Jang’ombe saa 2:30 usiku.

2/1/2017 Azam vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Jamhuri saa 2:30 usiku.

3/1/2017 Jang’ombe boys vs URA saa 10:00 alasiri, KVZ vs Simba saa 2:30 usiku.

4/1/2017 Zimamoto vs Yanga saa 10:00 alasiri, Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.

5/1/2017 KVZ vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri, Simba vs URA saa 2:30 usiku.

6/1/2017 Taifa ya Jang’ombe vs KVZ saa 2:30 usiku.

7/1/2017 Jamhuri vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Azam saa 2:30 usiku.

8/1/2017 Simba vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri ,Taifa ya jang’ombe vs URA 2:30 usiku.

10/1/2017 Saa 10: 00 nusu fainali ya kwanza , Saa 2:30 nusu fainali ya pili.

13/1/2017 Fainali saa 2: 30 usiku.
 
Eeeh kama kawa..wapinzani lazima waelewe kwamba simba ni maji ya shingo, na huu mwaka pia watatusoma kwa sana hah hah time will tell!
 
Kesho kikosi cha Simba SC kinaanza safari ya kuelekea Unguja.. kikiwa na wachezaji wote waliosajiliwa kumtumikia Mnyama katika msimu huu wa 2016/2017. Pia wameongezwa baadhi ya vijana toka Simba B.
 
Mwangalingimungu njoo na huku uendeleze ligi yako ya ubishi wa takwimu.

Nasikia miamala huwa haisomi kwa marefa wa visiwani. Ni haki bin haki ndio maana timu zinazopenda mbeleko zimekuwa wasindikizaji wazuri miaka nenda miaka rudi.
 
536f91ec1f87502ffc4193ba59089825.jpg
 
Kesho kikosi cha Simba SC kinaanza safari ya kuelekea Unguja.. kikiwa na wachezaji wote waliosajiliwa kumtumikia Mnyama katika msimu huu wa 2016/2017. Pia wameongezwa baadhi ya vijana toka Simba B.
Mtani hilo kombe tuliisha wabinafsishia wala hatuna matatizo nanyie ni la kwenu kiukweli na huona vibaya kama mwaka jana wale waganda walilichukua waliwadhulumu haki yenu ya msingi kila la kheri mtani
 
Shukrani Mkuu kwa kulitambua mapema.. Natamani sana hata wale ndugu zako, wangekua na wepesi wa kuelewa kama wewe.
 
Mwangalingimungu njoo na huku uendeleze ligi yako ya ubishi wa takwimu.

Nasikia miamala huwa haisomi kwa marefa wa visiwani. Ni haki bin haki ndio maana timu zinazopenda mbeleko zimekuwa wasindikizaji wazuri miaka nenda miaka rudi.
 
Mambo ya aibu sana kwa mchezaji mkubwa!

Kwa mashabiki wastaarabu hata wa timu yake walipaswa kukemea upuuzi huu. Ndio maana wengi wamenyaa kuonesha kutofurahia jambo hili, lkn hiyo haitoshi, linapaswa kukemewa hadharani
 
Full Mziki uliopo Zenji kwa kazi moja tu, kumrejesha mwali wetu ni;

MAKIPA; Peter Manyika, Dennis Richard na Daniel Agyei.

MABEKI:Hamad Juma, Janvier Bokungu, Novaty Lufunga, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda na Method Mwanjali.

VIUNGO: Said Ndemla, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mwinyi Kazimoto, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Muzamil Yassin, James Kotei

WASHAMBULIAJI: Pastory Athanas, Juma Luizio, Mavugo na Blagnon.

NB: Leo mida ya saa 2 usiku mnyama atakua dimbani kuchukua pointi zake 3 toka kwa Taifa ya Jang'ombe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom