Kombe la Dunia Urusi: Fahamu mataifa yaliyofuzu hadi sasa

1. Afrika yenye mataifa wanachama wa FIFA 53 ina nafasi 5 kwenye kombe la dunia. Hadi sasa,timu mbili za Misri na Nigeria zimeshafuzu. Bado zasubiriwa tatu.

2. Asia yenye timu wanachama wa FIFA 46 ina nafasi nne na nusu/tano kwenye kombe la dunia. Yaani mshindi wa tano wa Asia ambaye alikuwa Syria ilipambana na Australia.Tayari Iran,Korea ya Kusini,Saudi Arabia,Japan na Australia zimeshafuzu

3. Ulaya yenye timu wanachama wa FIFA 54 ina nafasi 13. Kwakuwa michuano itafanyika Ulaya,kutakuwa na timu 14. Tayari mataifa 10 yameshafuzu: Ubelgiji,Ufaransa,Iceland,Ureno,Serbia,Uingereza,Ujerumani,Poland,Urusi na Hispania. Nafasi nne zinasubiri play-off za washindi wa pili wa makundi wakiwemo Italia na Sweden.

4. Amerika ya Kaskazini,Amerika ya Kati na Karibiani ina mataifa 35 na ina nafasi 3 na nusu. Tayari Costa Rica,Mexico na Panama zimeshafuzu. Mshindi wa nne ambaye ni Honduras atacheza play-off kusaka kufuzu.

5. Oshenia ina timu 11 na ina nafasi nusu,yaani mshindi wake hucheza na mshindi wa 5 wa Amerika ya Kusini kusaka nafasi. Tayari New Zealand ameweka miadi na Peru.

6. Amerika ya Kusini yenye timu 10 ina nafasi 4 na nusu. Tayari mataifa manne ya Brazil,Uruguay,Colombia na Argentina yamefuzu. Peru atasaka nusu na New Zealand.

Siku njema waungwana!

Mkuu petro. Samani aise. Kwa timu za ulaya,,,ktk kila kundi huwa ni timu ngapi zinacheza???? Na kati ya izo ni ngapi zinashiriki kwenda russia? Ni mbili ama ni tatu?
 
Mkuu petro. Samani aise. Kwa timu za ulaya,,,ktk kila kundi huwa ni timu ngapi zinacheza???? Na kati ya izo ni ngapi zinashiriki kwenda russia? Ni mbili ama ni tatu?
Mshindi wa kwanza hufuzu moja kwa moja. Wa pili hucheza play-off na mwingine mechi mbili. Kundi huwa na timu tano.
 
Back
Top Bottom