Kombe la Dunia Urusi: Fahamu mataifa yaliyofuzu hadi sasa

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,195
25,513
1. Afrika yenye mataifa wanachama wa FIFA 53 ina nafasi 5 kwenye kombe la dunia. Hadi sasa,timu mbili za Misri na Nigeria zimeshafuzu. Bado zasubiriwa tatu.

2. Asia yenye timu wanachama wa FIFA 46 ina nafasi nne na nusu/tano kwenye kombe la dunia. Yaani mshindi wa tano wa Asia ambaye alikuwa Syria ilipambana na Australia.Tayari Iran,Korea ya Kusini,Saudi Arabia,Japan na Australia zimeshafuzu

3. Ulaya yenye timu wanachama wa FIFA 54 ina nafasi 13. Kwakuwa michuano itafanyika Ulaya,kutakuwa na timu 14. Tayari mataifa 10 yameshafuzu: Ubelgiji,Ufaransa,Iceland,Ureno,Serbia,Uingereza,Ujerumani,Poland,Urusi na Hispania. Nafasi nne zinasubiri play-off za washindi wa pili wa makundi wakiwemo Italia na Sweden.

4. Amerika ya Kaskazini,Amerika ya Kati na Karibiani ina mataifa 35 na ina nafasi 3 na nusu. Tayari Costa Rica,Mexico na Panama zimeshafuzu. Mshindi wa nne ambaye ni Honduras atacheza play-off kusaka kufuzu.

5. Oshenia ina timu 11 na ina nafasi nusu,yaani mshindi wake hucheza na mshindi wa 5 wa Amerika ya Kusini kusaka nafasi. Tayari New Zealand ameweka miadi na Peru.

6. Amerika ya Kusini yenye timu 10 ina nafasi 4 na nusu. Tayari mataifa manne ya Brazil,Uruguay,Colombia na Argentina yamefuzu. Peru atasaka nusu na New Zealand.

Siku njema waungwana!
 
World cup bila Argentina, and uwepo wa King Messi c chochote__ni sawa sawa na mbagala cup.

Asante sana chama langu la wanaARG___
 
MKuu naomba kujua kwaNini ulaya wawakilishi ni wengi kuliko afrika wakati wanakaribia idadi sawa ya mataifa wanachama wa FIFA
Kiwango cha mpira ndio sababu.
Idadi ya washiriki kwa michezo ya mabara huangalia kiwango.
Infantino ameshapendekeza Africa ipeleke timu saba kwa mashindano ya 2022 nadhani kama kutakuwa na mabadiliko ya idadi kutoka timu 36 hadi 48
 
Asante mkuu ila naomba kuuliza ni kigezo gani kinatumika kuipa ulaya timu 13/14??
 
Kiwango cha mpira ndio sababu.
Idadi ya washiriki kwa michezo ya mabara huangalia kiwango.
Infantino ameshapendekeza Africa ipeleke timu saba kwa mashindano ya 2022 nadhani kama kutakuwa na mabadiliko ya idadi kutoka timu 36 hadi 48

Kutoka 32 mpaka 48. Hivyo zimeongezeka 16 + 32= 48
 
Back
Top Bottom