Kombe la dunia: Kocha anapo nuna na kukataa kupongezwa baada ya timu yake kushinda

Tall

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
1,425
165
1.SIKUAMINI BAADA YA KUONA KOCHA HATAKI KUPONGEZWA NA WACHEZAJI WALIOMVAMIA KUMPONGEZA BAADA YA MECHI KATI YA GHANA NA SERBIA.
2.JE NI KWELI YULE NI KOCHA WA GHANA? AU MACHO YANGU?
3.NASIKIA JAMAA HUYO NI MSERBIA.....SASA EEEH,UNAIFUNGA TIMU YA HOME?
.......KAMA NI HIVYO itabidi aombe uraia GHANA.
4.NAOMBA MAONI YENU WANA JF? NI SAHIHI NILIVYOONA?
 
Hakika alilofanya si uungwana. Kwa mtazamo huo alikuwa anategemea/anapenda Ghana kufungwa. Ajiuzulu kulinda maslahi ya taifa lake ili tujue moja.
 
Aliposign contract hakujua kuwa hayo yaweza kutokea? Ingawa hata mimi nilimuona muda wote kasimama kama vile hana raha vile? Shauri lake alishawapa vujana ujanja na hawezi tena kuutoa!! kwikwi kwi. Na hao serbia wasimlaumu!!
 
Hakika alilofanya si uungwana. Kwa mtazamo huo alikuwa anategemea/anapenda Ghana kufungwa. Ajiuzulu kulinda maslahi ya taifa lake ili tujue moja.

...Na kwa hakika alitakiwa aachie ngazi hapo hapo maana ikitokea timu hizo zikikutana Nusu fainali ama Fainali (Inawezekana!) atafanya nini ili kuhakikisha timu ya alikozaliwa inaishinda ile ya anakofanyia kazi!!!
 
Ifikie mahali Afrika tutegemee makocha wetu wazalendo..
Mbona Algeria wameweza...
 
Ilifika mahali nikawa nashindwa kutofautisha kati ya Kocha wa Ghana na kocha wa Serbia maana wote walikuwa wana Huzuni
 
We are happy that an African team has beaten a good European team and we hope that the whole of Africa is celebrating the continent's first win in the 2010 World Cup," Rajevac told a post-match news conference.

"It was a very difficult match and a clash of contrasting styles, so I have to congratulate my players for a valiant effort because they kept going until the end," he added.

But Rajevac also had mixed emotions about beating Serbia in their opening Group D match and said he hoped both teams would qualify for the last 16.

"This is the greatest win of my career but I also feel sorry for Serbia, I saw the anguish on the players' faces after the final whistle.

"I had a job to do and I did it professionally but I hope my countrymen win their next two games against Germany and Australia, I wish them the best of luck."
Source

Jamaa alionesha uzalendo fulani kwa nchi yake,ni kama vile tunavyomlalamikia Maximo kutuwekea kipa mbovu katika pambano la Taifa stars na Brazili
 
Kusema kweli msione ajabu huyu jamaa kocha wa Ghana amesikitishwa! Hawa wa-Serbia ni wa-fanatics, yaani wote hawa watokao BALKANS countries au SLAVIAN countries....chukueni mfano miaka ya 90 walivyokuwa wakiuana kule Bosna. Yaani si mchezo wala msione ajabu huyu jamaa baadae akiona Serbia inkaribia kutolewa akafanya mambo yake ili awezeshe Serbia iendelee. Ktk statistics inaonyesha kwamba kocha wa Zaire miaka ya 70 ilifungwa mabao kibao 9 kama sikosei, wakiwa na kocha wa kiYugoslavia(Serbia hao hao tu) wakati walivyocheza nao.
 
Source

Jamaa alionesha uzalendo fulani kwa nchi yake,ni kama vile tunavyomlalamikia Maximo kutuwekea kipa mbovu katika pambano la Taifa stars na Brazili

Hilo Neno Inawezekana kabisa Mwarami aliwekwa pale kama Shati golini ili wakina Binyo wajifungie migoli tu! hakuna cha JABULANI wala nn!.
Jana Kweli yule MSERBIA hakuwa na raha kabisa Ajira na Utaifa kipi zaidi
?
 
Hata mimi niliona baada ya mpira kwisha wachezaji wa akiba na bench lote la Ghana walimvamia kumpongeza jamaa akatimua zakje huko as if hakufurahia kitendo cha Ghana kupata lile goli. Nadhani yeye anatakiwa kufanya kazi yake hayo ya uzalendo mbonanchi yake mwenyewe haikumpa jukumu la kufundisha timu yao ya Taifa??:sick:
 
ndio aruke-RUKE sana tu,sasa alifata ajira ghana ya nini?au nje ya nchi yake?nyambaf
aliniboa sana,tungekuwa sie timu si katukwepa?angeshangaa mchuno wake kuazia hapo adi aombe msamaha
izi ngozi nyeupe(% kubwa) ovyooo ovyoo wanaboa kinoma unaweza chapa mtu kofi
 
Ni kawaida sana hii kutokea kwenye soka. Hilo tukio linanikumbusha Carlos Tevez alipowafunga Westham United timu yake ya zamani hakushangilia lile goli kabisa. Ni nzuri kwa mtu mwenye mapenzi ya kweli na kule alikotoka
 
it was fair jamani mlitaka aruke ruke kushangilia?
kwa hiyo Ghana ingeshindwa angeshangilia mkuu?
Nasita kusema huyu jamaa hatufai waafrica.ghana ni wazuri lakini kocha wao bomu anaweza hata kuuza mechi huyu,mpira hauchezwi kiwanjani tu
 
Nakumbuka siku moja nilipocheza mpira against timu ya mwajiri wangu.siwezi kusahau,ni mauzauza matupu.tulishinda na mimi ndie nilikuwa nguzo ya ushindi ule, ,pamoja na kuwa niliruhusiwa na uongozi/mwajiri kuchezea kule lakini wafanyakazi wote hawakunielewa.
 
Makocha wa kizungu tunaowaamini ndio wanao tuangusha timu zetu za Africa kufanya vibaya kwa kuwachezesha wachezaji nyota duniani nafasi amabazo hawajazizoea wewe umeona wapi Mzungu achekelee mwafrika ashinde kombe la dunia??
 
Back
Top Bottom