Kombe la Copa Coca Cola laenda Zanzibar kwa kuifunga Tabora 2-1 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kombe la Copa Coca Cola laenda Zanzibar kwa kuifunga Tabora 2-1

Discussion in 'Sports' started by bnhai, Jul 18, 2009.

 1. b

  bnhai JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  RAIS Jakaya Kikwete jana aliongoza Watanzania kushuhudia fainali ya kuvutia ya michuano ya Copa Coca-Cola ambayo ilishuhudia Mjini Magharibi ikitwaa taji hilo baada ya kuilaza Tabora mabao 2-1.

  Kikwete, ambaye ni mpenzi mkubwa wa soka aliwasili uwanjani hapo saa 9. 20 bila kutarajiwa na wengi huku mawaziri wake, George Mkuchika (Habari) na Margaret Sitta (Maendeleo ya Jamii) na uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ukiongozwa na rais wake, Leodegar Tenga wakiwa tayari wameketi.

  Ujio huo wa Rais Kikwete ambaye aliinuka na kushangilia bao la Tabora dakika chache kabla ya filimbi ya mwisho na lile la ushindi la Wazanzibari uliwachangamsha mashabiki wengi waliojitokeza kutazama mchezo huo.

  Katika mchezo huo uliochezwa kwa dakika 120, kasoro pekee ilikuwa kipa chipukizi wa Tabora, John Protase ambaye alicheza vizuri, lakini kwa muda wote alidaka michomo mikali bila glovu mikononi.

  Baada ya mchezo huo, Mohammed Abdulkarim wa Mjini Magharibi aliiongezea tuzo timu yake kwa kuibuka mchezaji bora wa michuano ya mwaka huu na kutwaa Sh500,000 huku Kigoma ambayo ilimaliza katika nafasi ya nne ikitwaa taji la timu yenye nidhamu.

  Mgeni rasmi, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Kapteni, George Mkuchika aliwashukuru wadhamini, Kampuni ya Coca- Cola kwa kuiwezesha michuano hiyo kuwa yenye mafanikio na kuwataka wajikite zaidi katika michuano hiyo kwa muda mrefu zaidi.

  Maelfu ya mashabiki waliofurika Uwanja wa Uhuru walijionea mchezo wenye ushindani mkubwa na vipaji kutoka kwa timu zote mbili, ingawa Mjini Magharibi walionyesha kuwa hazina kubwa kwa siku za usoni katika soka.

  Kwa ushindi huo, Mjini Magharibi waliondoka na kitita cha shilingi milioni 4.5 huku washindi wa pili, Tabora ambao walikabidhiwa zawadi yao na Waziri Sitta wakinyakua shilingi milioni 3 na Morogoro waliomaliza katika nafasi ya tatu wakilamba milioni 2.

  Washindi hao pia wameahidiwa zawadi, zikiwamo za kupokewa na kuenziwa kishujaa na wabunge wa Zanzibar waliomo katika kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano mjini Dodoma, walidhihirisha umahiri wao wa kusakata kandanda la kisasa.
  Wabunge wa Zanzibar wakiongozwa na Hafidh Ally Tahir (Dimani- CCM) walitoa ahadi hiyo mjini Dodoma juzi wakieleza dhamira ya kuwafikisha mashujaa hao bungeni muda wowote kuanzia kesho, Jumatatu.
  Source; Mwananchi
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hureeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!
  Kudadadeki............Maximo upooooooooooooooooooo!!!! siyo una'nga'ngania vifuu tundu tu, watoto haoooooo!!!!
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  TFF....mpo?
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ngoja nisherehekee kwa Urojo, Pweza na vibibi hapa, bila kusahau kushushia na sharubati.
   
 5. T

  TX Member

  #5
  Jul 19, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ndio zenj. NA hUYO mximo anangangania tanzania bara huku akiacha wa zENJ. mAximo chukua vijana hao
   
 6. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nafikiri hii wataiondoa kwenye kero za Muungano kidogo kwa sasa angalau tupumue
   
Loading...