Kombani: Sifikirii kujiuzulu wala Sitegemei kufukuzwa kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kombani: Sifikirii kujiuzulu wala Sitegemei kufukuzwa kazi

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Diehard, Jan 4, 2011.

 1. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Katika hatua ya kuweweseka Celina Kombani amejigamba hategemei kufukuzwa kazi sijui alimpa limbwata JK CHEKI ZAIDI source Mwananchi:
  SIKU moja baada ya CUF, kumshauri Rais Jakaya Kikwete amfukuze kazi Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani kwa madai ya kutoa kauli inayowachanganya wananchi kuhusu Katiba, Waziri huyo ameibuka na kusema "Sifikirii kujiuzulu, wala sitegemei kufukuzwa"
  Juzi CUF kilimshauri rais Kikwete kuwapumzisha Waziri Kombani na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema kwa kile ilichoeleza kuwa wamekuwa wakiropoka kuhusu suala la Katiba na kuwachanganya wananchi.

  Wakati mjadala wa Katiba ukiwa umepamba moto, Waziri Kombani ambaye ndiye waziri mwenye dhamana alisema, "Katiba mpya kwa sasa haiwezekani kabisa kwani sio muhimu na kuwa Serikali haina bajeti ya kushughulikia katiba mpya".

  Waziri huyo aliyepewa dhamana ya kuongoza wizara hiyo kwa mara ya kwanza, alisema Serikali itaendelea kufanya marekebisho ya sheria hiyo mama wakati wowote inapolazimika.

  “Wachache waje na kitu chenye mashiko na katika maandishi, wakionyesha ni vifungu gani vyenye upungufu, kwa nini vina upungufu na wapendeekeze mbadala wake. Serikali haiwezi kufanyia kazi vitu muhimu kama hivi kwa kupata taarifa kupitia magazetini tu,” alisema Kombani.

  Naye Mwanasheria Mkuu wa Seriakali, Jaji Frederick Werema alisema, "Kuandika Katiba mpya hapana, lakini kufanya marekebisho kwa kuondoa au kuongeza mambo fulani kwenye katiba, ruksa.” Jaji Werema alisema hayo Desemba 27 mwaka jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa hafla ya kumwapisha Jaji Mkuu Mpya, Jaji Mohamed Othman Chande.

  "Suala la kubadilisha ibara zinazoonekana kutokidhi haja na kuingiza mambo mapya kwenye katiba, linakubalika na kwamba hayo yamekuwa yakifanyika," alisisitiza Jaji Werema na kutolea mfano mabadiliko ya katiba yaliyoruhusu kuingizwa kwa haki za binadamu. Lakini alipotakiwa kuzungumzia kauli hiyo ya CUF jana, Waziri Kombani alisema hafikirii kujiuzulu wala hajui kama atafukuzwa. “Mimi sijui kitu.

  Nimesema sijui chochote na wala sifikirii kujiuzulu hata suala la kufukuzwa silielewi,”alisema Waziri Kombani. Wakati Waziri Kombani akisema hivyo, Jaji Werema jana aliliambia gazeti hili kuwa "Sitaki usumbufu, mimi niko likizoni." Aliendelea ‘Sitaki usumbufu wowote kuhusu hilo na sitaki kusikia habari hizo kabisaaaa.”
  Lakini Mwanasheria Mkuu huyo wa Serikali aliwahi kuliambia gazeti hili kuwa hawezi kujiuzulu kwa kauli alizotoa kuhusu Katiba na Dowans.

  "Sijiuzulu ng'o," alisema Jaji na Werema na kuongeza: ''Wanaotaka nijiuzulu ni wale wasiofikiria, kwani kila mtu ana nafasi yake ya kuongea kuhusu katiba. Mimi nimetoa mawazo yangu na wengine wakitaka watoe ya kwao."
  Aliendelea, ''Kunitaka nijiuzulu ni fikra za kichanga sana na potofu. Mtu mwenye upeo mpana hawezi kusema Mwanasheria Mkuu ajiuzulu kwa hili,"alisema.

  Juzi, CUF iliitisha mkutano na waandishi wa habari na kueleza kuwa kauli hizo watendaji wakuu wa Serikali kuhusu katiba zinawachanganya wananchi hivyo Rais anapaswa kuwafukuza kazi kwa maslahi ya Serikali yake.

  "Kama Rais Kikwete atakuwa makini, anapaswa sasa kuwapumzisha Kombani na Werema ili wasiendelee kutia doa jeusi Serikali yake ambayo tayari imejaa kila aina ya matatizo," alisema Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
   
 2. Lisa Rina

  Lisa Rina JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 1,768
  Likes Received: 2,021
  Trophy Points: 280
  Hawa watu wajeuri sana kwa kweli!hii jeuri wanaitoa wapi?
   
 3. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kombani uwezo wa kufikiria ni mdogo pia katiba iliyopo haiwalazimishi kujiuzulu!! Katiba mpya itawakomesha tu
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Siri ya mtungi aijuae kata
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,831
  Trophy Points: 280
  Kwa anaewateua....na mifukoni mwao
   
 6. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Tanzania tuna tatizo la MANAGEMENT PRINCIPLES. Viongozi wengi hawana taaluma hii ndio maana kila mmoja anakurupuka kivyake vyake. Principally there should be a Government spokesman on all sentitve issues like Katiba. Hili sio jambo la Wizara hata kidogo. Waziri anapolisema kama vile ni agenda yake anakiuka taratibu na behind the curtain anamsema Rais ambaye hakumruhursu afanye Hivyo . Kimsingi wanatakiwa Mawaziri na Viongozi wote wa Serikali waliojaidai kutoa msimamo wa Serikali waadhibiwe kisheria kufuata kanuni za utumishi.

  Jinsi walivyokuwa mbumbumbu eti wanakuja tena hewani kujigamba hawajiuzulu na machinery inakaaa kimya tu icluding Rais ambaye in simpler terms amekuwa insurbodinated. Haki a nani hata bar Bar maid au meneja hawezi kuzungumzia suala ambalo bosi wake ndio mhusika.Sembuse IKILU? Upuuzi.
   
 7. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Serikali za kishikaji mtu hujiuzulu akiwa ameshindwa kutetea maslahi ya mtu binafsi ya aliyemweka madarakani na wala sio anapopotoka katika kutimiza wajibu wake kwa wananchi. Kwa hiyo tusitegemea Kombani ajiuzulu kwani hawajibiki kwetu ila kwa mwenye maslahi yake binafsi. Haya ndiyo yakuzingatia tutakapotunga katiba mpya: Serikali iwajibike kwa walioiweka madarakani na sio kwa maslahi ya rais
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Anaposema hategemei kufukuzwa kazi manake ata kuteuliwa alishaambiwaga kabla.
  Iyo stm inaleta maswali mengi sana kuwa labda kuna mtu amewekwa kiganjani na hafurukuti
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Wana kiburi toka kwa bosi wao kmanake washamteka na hawezi kikwamua kutoka mtegoni!
   
 10. Q

  Quick Senior Member

  #10
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kitaeleweka tu,watatoka tu,time will tellllllll:angry::angry::angry::angry::angry:
   
Loading...