komba awaponda na kuwatishia wapinzani live leo bungeni.

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Mh kapteni Komba ameshauri wabunge wote wanaoipondea CCM badala ya kuijadili bajeti wakapimwe akili mirembe then ndo waruhusiwe kuingia bungeni.Pia ametoa tahadhari kwa wabunge wa upinzani wanaotamani milango ifungwe ili ngumi zitembee kwamba wasiombee hilo kutokea kwani watachakazwa vibaya sana kwasababu wabunge wa C.C.M ni wengi zaidi.
 
yeye na tumbo lake anaweza pigana?uwezo wake wa kiakili unaadhiriwa na tumbo lake kubwa kama mimba ya mapacha sita na aache unafki 2015 tupa kule huyu kahaba wa mtoto mdogo lulu
 
mimi napita namsubiri Mbunge wangu Livingstone Lusinde kesho maana leo nimeona katika TV matusi kila upande hadi mwenyekiti kidogo bunge limshinde.

Kwa ngumi zitajatokea tu maana kuna vibunge vinaporomosha mitusi mikubwa kuliko, sokwe mtu, akili km kukalia ******,mara mapepo nk
 
Wakiendelea na mtindo wa leo watadundana kweli. Hakuna haja ya CCM kujitutumua, wananchi wenye akili wanaelewa cha kufanya 2015. Uzuri wa bajeti ni utekelezaji wake na siyo maneno mengi.
 
Kwa hisani kubwa ya walipa kodi wa nchi hii, wawakilishi baada ya kuumiza vichwa kutafuta njia mpya kabisa za kuondoa umasikini wao wanataka kudundana.
 
Sijawahi kumsikia Komba akiongea points ndani ya Bunge zaidi ya maneno kama hayo aliyoropoka.
Hata sijui wananchi wa jimboni kwake wanajisikiaje wanapomsikia.
 
Kwa kweli CCM imekosa wazee wa kukemea mijitu Kama Komba!!?? Angebaki kuimba mapambio huko TOT.....Nafikiri imefika Muda sasa kwa Mbunge akichafua hali ya hewa apigwe viboko 12 hadharani bungeni. Mijitu Kama Komba itakaa kimya , maana linaonekana linaogopa sana fimbo! Tena unalichapa fimbo kwenye mtumbo wake.
 
Sijawahi kumsikia Komba akiongea points ndani ya Bunge zaidi ya maneno kama hayo aliyoropoka.
Hata sijui wananchi wa jimboni kwake wanajisikiaje wanapomsikia.

Hapa kuna mawili: moja,mfumo mbovu wa uchaguzi ndiyo umeingiza mbunge mbovu kama Komba. Pili,wapiga kura nao yawezekana wakawa na akili sawa na mbunge wao;pengine tena unaweza kukuta jana waliona mbunge wao kachangia hoja zenye manufaa kwao!

Tukijua ni kipi kati ya hivyo kinapelekea kuwepo na wabunge kama Komba,ndipo tutafute suluhu.
 
Dawa yake inaitwa PIRITON........akisikia CHADEMA wanaongea halali..........wakiongea magamba wenziye analala

mh%2Bkomba.jpg
 
Huyu jamaa akaimbe kwaya aachane na siasa..japo kuna uhuru wa kidemokrasia wa kila mtu kuchagua au kuchaguliwa ila siasa ni proffesiional si kila mtu anaweza kuwa mwanasiasa
 
Mimi niliangalia jana matukio haya kupitia Luninga na sikuweza kuamini machoni mwangu.
Ni Tanzania pekee ambako Mbunge wake anaweza kusimama na kutetea Bajeti isiyo na tija kwa Watu anaowawakilisha kisa eti imetayarishwa na Serikali inayoongozwa na chama chake.Mimi naijua Iramba ya Mchemba na Mbinga ya Kombo jinsi zilivyo hoi kimaendeleo katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru hivyo si sahihi kwa Wabunge hao kutetea Bajeti ya Mwaka 2012/2013 kama ilivyowasilishwa Bungeni.Niwaombe wananchi wa maeneo hayo watueleze kama na wao kwa ujumla wao wanafaidi ulaji wanaopata akina Mwigulu na Komba umbao unawasukuma kutetea kwa nguvu zao zote kile ambacho hakina tija bila kujali maslahi yao.
 
Kwanza utapozuka ugomvi hofu yangu ni yeye kufa kwa BP kabla hata ya kupigwa.
 
Hapa kuna mawili: moja,mfumo mbovu wa uchaguzi ndiyo umeingiza mbunge mbovu kama Komba. Pili,wapiga kura nao yawezekana wakawa na akili sawa na mbunge wao;pengine tena unaweza kukuta jana waliona mbunge wao kachangia hoja zenye manufaa kwao!

Tukijua ni kipi kati ya hivyo kinapelekea kuwepo na wabunge kama Komba,ndipo tutafute suluhu.

Sio wote mjomba tulimpigia kura huyu Komba bali hapakuwa na mgombea wa upinzani kuweza kusimama dhidi ya hili jitu. There4 wananchi wa Mbinga magharibi hatukumtuma atukane balimawe sauti yetu kusemea kero zinazotukabiri. Jimbo limelala sana kuanzia vijiji Lituhi, mbaha, lundu, hinga, ngumbo, mkili, liwundi, njambe, tumbi, liuli, lundo, mbambabay, etc watu wana ari ya kuona jimbo lao likipiga hatua ya kimaendeleo.
 
Back
Top Bottom