Komandoo Dk Salmin Amour atua Dodoma na Siri moyoni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Komandoo Dk Salmin Amour atua Dodoma na Siri moyoni!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mdondoaji, Jul 8, 2010.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  WAKATI hatima ya kumpata mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM inaelekea ukingoni mwishoni mwa wiki hii, makundi ya ushabiki yanahaha kuwapigia debe wagombea watatu ambao ni Dk Ali Mohamed Shein, Dk Ghalib Bilal na Shamsi Vuai Nahodha.

  Jana rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk Salmin Amour (Komando) aliwasili mjini Dodoma akiwa katika ndege moja na Waziri wa Kiongozi Vuai Nahodha ambaye ni mmoja wa wagombea.


  Kwa muda mrefu sasa Dk Salmin haudhurii mikutana na vikao vya chama kutokana na kusumbuliwa na macho, hali inayoonyesha kuwa hatua ya sasa ya kumpata mgombea urais wa Zanzibar kupitia CCM ina unyeti wake.


  Makundi hayo yameunda ushindani mkubwa miongoni mwa wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM itakayofanyika kesho, mjini Dodoma.


  Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata kutoka Dodoma wakati wajumbe na wagombea wanaendelea kuwasili, kuna mchuano mkali miongoni mwa makundi ya wapambe wao.

  Fununu zaidi kutoka muongoni mwa wajumbe wa CCM zinasema kuna utofuati kati ya wajumbe wa Zanzibar na wa Bara kuhusu uungwaji mkono wa wagombea hao.
  Uchunguzi umebaini kwamba, wafuasi wa vigogo hao wamekuwa wakitambiana na kuelekeza kampeni kwa wajumbe wa Halmashauri ya CCM (Nec), ambao ndio watakaopiga kura kumchagua mtu mmoja atakayeshindana na wapinzani katika kinyang'anyiro hicho.

  Taarifa zinaeleza kuwa ingawa Dk Bilal anatajwa kuwa mshindani mkubwa katika kinyang'anyiro hicho, nafasi yake kuingia tatu bora ina utata kutoka na tuhuma za wafuasi wake kuendeleza kutoa lugha isiyonzuri.


  Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amedokeza kuwa katika uteuzi huo chama hakitafanya makosa kwa kumteua mtu ambaye watu watamguna na kugoma kumchagua.


  Akizungumza na waandishi wa habari jana jioni, Makamba alisema Kamati Kuu ya CCM itakutana kesho sambamba na Halmashauri Kuu ambayo itaanza kikao mara baada ya kumaliza kamati ili kuzuia kuvuja kwa maamuzi yaliyofikiwa.

  Akizungumza katika mahojiano maalum na TBC1 juzi, Makamba alisema mgombea urais wa Zanzibar atapatikana kwa sifa zake na jinsi atakavyojieleza mwenyewe mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC).


  “Hapa hakuna cha mgombea kupita kwa kupigiwa debe wala nini, CCM haiwezi kufanya makosa katika hili kwa kuwa tukimpitisha asiyefaa, watu wataguna na wakiguna ina maana tutashindwa katika uchaguzi; hivyo mgombea atapatikana kupitia sifa tulizozianisha na atakavyojieleza,”alisema Makamba.


  Hata hivyo wakati Makamba akitoa kauli hiyo juzi asubuhi, wasomi na wachambuzi wa masuala ya siasa walisema kulingana na mfumo wa utawala uliopo nchini, rais hawezi kutoka nje ya Baraza la Mawaziri.


  Wasomi hao waliwatabiria kwamba, Dk Shein, Vuai na Bilal kuwa ndio wenye nafasi kubwa ya kuteuliwa na Kamati Kuu.


  Hata hivyo, walionya kuwa kulingana na siasa za visiwa vya Zanzibar, anahitajika kiongozi imara atakayeweza kuimarisha mshikamano baina ya Wazanzibari.

  Mhadhiri Msaidizi wa Kitivo cha Siasa ya Sayansi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally alisema CCM inakabiliwa na changamoto kubwa na kwamba kati ya waliojitokeza kutaka kuteuliwa wapo ambao hawaaminiki kutokana na rekodi na misimamo yao katika uongozi.


  “Lakini katika kinyang’anyiro hiki natoa nafasi kwa Dk Shein, Vuai na Dk Bilal,” alisema Ally.


  Profesa Mwesiga Baregu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augostine alisema Zanzibar wamezoea michuano mikali ya kisiasa na kwamba, si mara ya kwanza kujitokeza wagombea wengi katika nafasi hiyo.


  “Mtu ambaye hakuhusika katika mitafaruku hiyo ni Dk Shein na inaonekana ataweza kuwaunganisha Wazanzibari na hata maamuzi ya kumteua yanaweza yasiwagawe Wazanzibari,” alisema Profesa Baregu na kuongeza:

  “Pia Dk Shein hayuko kwenye kambi ya akina Karume wala Dk Salmini, au CCM Asilia na CCM Mtandao, hivyo haya ni mambo yatakayomfanya achaguliwe,” alisema Profesa Baregu.


  Mhadhiri wa Sheria wa UDSM, Dk Sengondo Mvungi alisema idadi kubwa ya wanaowania urais wa Zanzibar imeonyesha kiwango cha juu cha uelewa wao wa katiba ya nchi na haki zao.


  Mwenyekiti mwenza wa Mpango wa Utafiti wa Elimu ya Demokrasia (Redet), Dk Benson Bana alisema: “Kwanza tuwapongeze tu wametambua haki yao na wameonyesha ukomavu wa demokrasia.”


  Wanachama 11 waliojitokeza kuwania urais kumrithi Amani Abeid Karume ambaye amemaliza muda wake ni Nahodha, Ali Juma Shamhuna, Dk Shein, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar, Haroun Ali Suleiman, Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mohamed Aboud na Dk Gharib Bilal.


  Wengine ni balozi wa Tanzania nchini Italia, Ali Karume, Hamad Bakari Mshindo, Omar Sheha Mussa, Mohamed Yusuf Mshamba na Mohamed Raza Dharamsi.


  Wachambuzi wengine wa siasa wanasema sio rahisi kwa Haroun na Shamsi kuingia wote katika tatu bora kwa vile wanatoka katika jimbo moja la Makunduchi.

  Ali Karume ambaye ni mdogo wa Rais Amani Karume amekuwa akitamba kwamba, kutokana na elimu yake na uzoefu katika siasa, ana nafasi kubwa ya kuteuliwa na chama chake kama vigezo vilivyowekwa na vitafuatwa.

  Mohammed Aboud ambaye katika kikao cha kamati maalumu kilichofanyika Zanzibar wiki iliyopita kilimjadili na baadhi ya wajumbe kutoa tuhuma za kughushi vyeti, amekuwa akijitetea kuwa madai hayo hayana msingi na kuwa yuko tayari kutoa ufafanuzi mbele ya vikao vya juu vya chama vyenye maamuzi ya mwisho.


  Mohammed Raza amelalamikia kutoalikwa katika kikao cha CC kinachofanyika kesho na kudai kwamba kutoonekana kwake Dodoma hakumaanishi kujitoa katika kinyanganyiro hicho.


  “Mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM nilikwenda katika ofisi zetu za chama kutaka ufafanuzi nikaelezwa niende katika ofisi ya masjala ili kupata utaratibu zaidi kuhusu kwenda katika kikao cha NEC Dodoma," anasema Raza katika barua yake kwa Rais Kikwete.


  Dk Salmin akilitua mjini Dodoma saa 8:10 kwa ndege ya Shrika la Ndege la Precision akiwa ameongzana na mgombea wa Urais, Nahodha pamoja na Asha Abdalah Juma ambaye ni Waziri na Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala bora, Ramadhani Abdalah, baadhi ya wabunge na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.


  Komandoo Salmin, alikuwa wa kwanza kushuka na kufuatiwa na Nahodha na viongozi mbali mbali wa serikali na CCM walifika kuwalaki.

  Mgombea mwingine wa Urais wa Zanzibar, Dk Shein aliwasili jana majira ya saa tano asubuhi akifuatiwa na mgombea mwingine, Mohamed Aboud ambaye ni Naibu Waziri wa Afrika ya Mashariki.

  Hata hivyo hadi jana mchana ilikuwa haijafahamika kama Bilal amefika Dodoma ingawa wapiga kampeni wake wameuteka mji wa Dodoma.


  Wakati viongozi hao wakitua, makundi ya wapiga kampeni wa Urais wa Zanzibar kutoka maskani mbali mbali, wamewasili mjini hapa tangu juzi usiku na jana walikuwa wametanda ofisi za CCM na kwenye nyumba za kulala wageni.


  Wengi wa makada hao wa CCM kutoka Zanzibar walikuwa ni Gharib Bilal toka maskani za mikoa mitano Zanzibar wakiongozwa na wajumbe wa maskani kubwa ya Kisonge, ambao walionya kuwa kamwe hawatakubali kusikia vikao vya juu ya CCM vimemwengua.


  Kada maarufu wa CCM Zanzibar na mmoja wa waasisi ya jumuiya ya vijana wa Afro-Shiraz, Baraka Mohamed Shamte, alisema chaguo la Wazanzibar wote ni Bilal na kama CCM Bara ikilazimisha kumleta mwingine kitakachotokea watajuta.


  Shamte alikuwa Katibu wa CCM katika wilaya mbali mbali, ikiwepo Wete Pemba, Unguja Mjini na Pangani mkoani Tanga, kabla ya kurejea Zanzibar.


  “Tangu mwaka 2000 chaguo la Wazanzibari ni Bilal na hadi sasa na kama wanataka CCM iendelee kuwepo Zanzibar waturejeshee Bilal kuwa mgombea wa Urais,”alisema Shamte.


  Wajumbe wengine, Ally Mzee na Mohamed Issa Ramadhani ambao walisema wanajua CCM bara wanamtaka Makamu wa Rais, Dk Shein, lakini wajuwe Zanzibar wanamtaka Bilal au Nahodha.


  Kada Mwingine wa CCM toka Zanzibar, Jamal Ramadhani ambaye alikuwa anaongoza ujumbe wa watu 200 toka Zanzibar alisema, CCM isifanye mzaha katika suala la uteuzi wa mgombea wa Urais Zanzibar.


  Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM Zanzibar, Vual Alli Vuai alimweleza mwandishi wa habari hizi mara baada ya kufika jana kuwa kamati maalum iliyopitia majina ya wagombea Zanzibar imemaliza kazi yake sasa imebaki kazi ya CC na Halmashauri Kuu.


  Habari hii imeandaliwa na Salma Said, Zanzibar, Mussa Juma, Dodoma,
  Sadick Mtulya na Salim Said, Dar  Source: Mwananchi.

  Kazi ipo kesho
   
 2. M

  MLEKWA Senior Member

  #2
  Jul 8, 2010
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa makachero wa Bilali watarudi ZNZ na vilio kama ilivyotokea mwaka 2000. Hatuwezi kuendelea kuchagua kundi la wana CCM wanaowabagua wana CCM wenzao kwa vile tu wanatoka kisiwa cha Pemba. DR Shein yuko na uwezo zaidi hasa ukizingatia amefanya kazi kwenye serikali zote mbili na Ameshika Nafasi kubwa zaidi kuliko Bilali na Nahodha , huu ndio ukweli Bilali hajakomaa kama Kiongozi kwani Kiongozi hawezi kuwa na makundi.
   
 3. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mazingaombwe ya Zanzibar, tusubiri tuone.
  Ni bora wakifarakana maana Upinzani unaweza kushinda sasa kwa margin kubwa
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hapa mteule ni Dr. Shein na sababu ni kwamba wanabadilishana post na rais Karume. Hii ni kwa mujibu wa muafaka uliofikiwa kati ya Karume na Seif wa kutaka Karume aongezewe muda na muda huo ataongezewa wa kwa kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Hivi vitisho vyote ni woga wa wala urojo ila CC ndiyo itaamua nani awe rais whether anachagulika au hachaguliki kwa CCM haijawahi kushinda Zanzibar so wembe ni ule ule uwizi wa kura.
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Mambo ya ngoswe mwachie ngoswe
   
 6. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tutahangaika na njia ndefu wakati formular ni ile ile tuliyotumia mwaka 2000 tukiwa form one haibadiliki and in maths the value of Pie is always 3.1416..... akili kichwani
   
 7. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  ccm bara wanamtaka shein hili wamburuze wanavyotaka na wazanzibari wanamtaka vuai au bilal hili walete mabadiriko kazi hipo.
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sijaelewa mantiki ya wabara kujitia katikati ya uchaguzi wa Wazanzibari..Huu ni ujinga wa ajabu sana unaokumbatiwa.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jul 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Sielewi kwanini NEC taifa ihangaika na uteuzi wa mgombea wa Urais Zanzibar? CCM Zanzibar ingekuwa na uwezo hadi hatua ya mwisho ya kumchagua mgombea wao.. watu wa bara kumpigia kura ni ukiukwaji mkubwa sana wa haki za Wazanzibari... ingekuwa mgombea huyo anapiga na kura na bara kwenye uchaguzi mkuu basi wana NEC wa bara wangekuwa na sababu ya kupigia kura.
   
 10. Yombayomba

  Yombayomba JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2010
  Joined: Aug 23, 2006
  Messages: 818
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wandugu,
  Ni wazanzibari wenyewe ndo waliotaka iwe hivyo, kama CCM Zanzibar ingelikataa nina uhakika CCM bara isingeingilia, swala ni kujiuliza ni kwa nini wagombea wa Zanzibar wasipigiwe kura na mkutano mkuu, angalau uwe na wajumbe wa zanzibar tu? kwa nini kikundi kidogo cha wazanzibar waamulie wamilion moja?
  matatizo mengi ya zanzibar ni ubinafsi wa wao wenyewe na ufinyu wa kuona mbali

  Yombax2
   
 11. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni vema wabara wakiweka mkono wao visiwani kwa sababu kule visiwani bado wanachaguana kwa kurithishana ili kundi fulani lisipoteze ulaji na mamlaka zao. Kwa kufanya hivyo wabara wanatemewa mate usoni na makelele meeengi hata vitisho visivyo na maana ilhali huku bara kuna wazanzibari kila mtaa wakitanua na hawataki mbara naye akatanue visiwani. Umimi wao wajue kwamba ni mwiba kwao wenyewe. Ina maana haki wanayo zaidi watu wa visiwani kuliko wabara katika matunda ya uhuru wetu? Labda kama Tanganyika itafufuka ambapo watanganyika waendelee na mambo yao na wavisiwani nao waachiwe mambo yao. Mbona wabara wanapofanya mambo yao wazanzibari nao wanashirikishwa? Kwa nini wabara wasishirikishwe kuhakikisha mdogo wao anakaa salama?

  Tusiongee kishabiki, sababu zilizowafanya Karume na Nyerere waamue kuunganisha nguvu zinabaki palepale, tena labda kwa sasa ni kubwa zaidi. Wakiachiwa wazanzibari wafanye mambo yao bila mkono wa bara watatoana macho kila siku na shughuli za maendeleo kamwe hazitafanyika. Siasa za visasi hazina tija, ndio hizo zinaepushwa. Sio lazima raisi awe mccm any way, mtu yeyote mzanzibari anaweza kuwa raisi kwani hiyo ni taasisi na sio mtu.
   
 12. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ndo uchakachuaji wa Demokrasia huu
   
 13. J

  Jafar JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kosa lilianzia kule kutokuwepo na serikali tatu. Kwa sasa vyetu vyetu (tanganyika), na vyao (Zenji) vyetu (tanganyika).
   
 14. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  tatizo hili litaendelea kuwapo madhali serikali ziko mbili.

  zanzibar ilitakiwa kuwa na uhuru wa kuchagua kiongozi wake............na tanganyika ikachagua kiongozi wake.............na muungano ukachaguliwa pamoja.

  kwa hali ilivyo sasa mpaka wa madaraka haupo wazi, na kwa 'ustawi' wa tanzania, ccm imeamua kuwachagulia wazanzibari viongozi wao
   
 15. Companero

  Companero Platinum Member

  #15
  Jul 8, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwa nini huelewi hili suala la kihistoria na kisiasa lililosimikwa kiimla toka enzi za Itikadi ya Chama kushika Hatamu? Siku Rais wa Zanzibar atakapoacha kuchaguliwa Dodoma ndio itakuwa mwisho wa ASP + TANU = CCM! Na mwisho wa ASP + TANU = CCM = ?
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mchaguliwa ni Shein hilo halina ubishi ,na ipo sababu ambayo sitoweza kuitaja hapa wala pengine ,yaani kwanini achaguliwe yeye ,zipo sababu labda kwa hali ya kisiasa inavyoendelea kwa hapa tulipo ,mwenye upeo wa kuchambua anaweza kuziona ssababu hizo ambazo hazitaki elimu kubwa wala usumbufu wa kivuvuzela.
  Ipo genune reason why is going 2b Shein ,watabiri kama mupo mnaweza kubashiri hilo.
   
 17. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160

  Usemayo yana ukweli, sioni mtu akipitishwa hapo zaidi ya Shein. Ila kitakachotokea baada ya hapo kwangu ndio itakuwa news.
   
 18. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kutokana na muundo wa Muungano halisi, sio rahisi kutenganisha uteuzi wa viongozi wajuu wa serikali hizi mbili. Japokuwa vipengele vingi vya muungano vinakiukwa.

  Katika hali sahihi kabisa, Rais wa Zanzibar alitakiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ila kuna uhuni uliofanyika wakamtoa Rais wa Zanzibar katika madaraka ya Jamhuri ya Muungano bila kuondoa namna ya kumteua. Mabadiliko yaliyofanywa na Bunge hayakuakisiwa na mikutano ya CCM.

  Kinachotakiwa kufanywa ni kumrudishia Rais wa Zanzibar mamlaka yake katika Jamhuri ya Muungano. Ikiendelea hivi, itabidi siku moja Zanzibar ijitoe katika Muungano kwasababu ya kukiukwa kwa makubaliano ya Muungano kuliko fanywa na viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
   
 19. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Inashangaza wanaibuka watu kujustify huu upupu..Inashangaza. Ndio maana waZnz wanasema wabara ni wakoloni kule wanalaotaka huwa kwa kupitia muhuri wa CCM..kazi kulazimisha tu waweke 'gavana' wao kuendeleza utawala wao wa kimabavu..
   
 20. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Kinachonifurahisha kwa wazanzibar ni kuwa pamoja na tofauti zao, linapojitokeza suala la maslahi ya zanzibar basi tofauti zao huziweka pembeni na kuwa kitu kimoja-angalia suala la zanzibar ni nchi au si nchi; suala la mafuta nk.
  Kwa hiyo tofauti zao zinakuwa za kisiasa tu lakini kimaslahi ya nchi yao hakuna tofauti.
   
Loading...