Malaika Mkuu
JF-Expert Member
- Nov 5, 2014
- 902
- 909
MUDA UMEBADILIKA
Leo Arnold Schwarzenegger amepost picha hii na kusema Time Has Changed. akimaanisha kwamba Muda Umebadilika. Hakuweka picha hii ili mradi tu, aliondoka nyumbani kwake akiwa na mablanketi yake, akayapakiza kwenye gari na kwenda kupiga picha katika moja ya sanamu zake ikiwa imechongwa jinsi alivyokuuwa akitunisha misuli zamani.
Utajiuliza ni kwa nini! Anajua kwamba muda umebadilika, zamani, alikuwa kijana, muda mwingi alitumia akiwa gym, ila leo hii, muda umebadilika na inawezekana kuna baadhi ya vyuma hawezi kuvibeba.
Ana miaka 68 mpaka sasa hivi! Kila kitu kimebadilika, si yule wa kipindi kile, huyu ni mwingine kabisa, inawezekana sasa hivi hata kutembea kilometa 20 hawezi. Anatukumbusha kwamba muda unabadilika, unapopata nafasi ya kufanya jambo katika kipindi cha ujana wako, fanya kwani baadaye utakuwa umechoka, hautoweza kufanya biashara zako na kuzunguka huku na kule.
Ndugu yangu! Hakuuna muda ulio sahihi, muda wako ni sasa hivi, siku inayoitwa leo ndiyo ya kufanya mambo yako yote huku ukimtanguliza Mungu! Kumbuka kwamba, hata Arnorld alikuwa na nguvu, tena zaidi yako ila leo hii, hana nguvu, ila nyuma ya pazia, alitengeneza maisha yake, tena amefanikiwa zaidi.
JE UPO TAYARI KUTENGENEZA MAISHA YAKO SASA HIVI?
SHARE NA VIJANA WENGINE WAJIFUNZE KITU.