Komaa na kinachotoka zaidi kwenye biashara yako

Ahsante SNA kKa hata Mimi nimepata somo nzuri sana,Mimi nina biashara ya steshenary lakini changamoto yake no mzunguko mdgo,japo kuna taasisi za serikali ya mtaa, shule Ila napata wateja wengi was kopi za vitambulisho na barua za serikali ya mtaa na picha. Naomba ujuzi zaidi ndugu yangu.
Jibu ni 1 mkuu..Komaa na kinachotoka zaidi ofisini kwako

Piga Picha nzuri,ongeza matangazo kuhusu copy na passport Brand ofisi yako upya ijulikane Kuwa Copy na passport hapo ndio nyumbani kwake..

Si kwamba hutofanya vitu vingine,hapana ila nachosema ni kwamba Ongeza matangazo ongeza vitu vyakufanya akiwaza kutoa copy aje kwako akiwaza passport aje kwako.

Wapga passport ni wengi ila wanaopga PASSPORT nzuri na kwa ubora "wanahesabika"

Mfano mzuri ni mimi... Nina passport zangu hizo nazielewa kinoma nilipga sehemh hao majamaa walijua nitengenezea passport nzuri,yani nilisafisha passport kibaooo niko nazo tu ndani...

na nikifikiria kupga tena passport ntaenda kule maana najua wanajua... nilishapga passport sehemu kibao ila kilaninapopgwa wanananitoa nasura kama Napuliza moto...

hivyo na wewe mkuu Komaaa tangaza kinachotoka zaidi...
 
Biashara ni mchezo wa kubahatisha ni mchezo ambao hauna Ninja, yeyote bahati itaemdondokea ndio mshindi,Hiyo ndio biashara sasa. Watu wengi tunapofungua biashara tunakua na idea zetu vichwani tunazotamani ziende kwa namna tumeziwaza na kutaka iwe, lakini katika waanzilishi wabiashara 100 watakaobahatika kufungua biashara zikaenda kama walivyopanga ni 10% tu.

Wengi biashara haziendi tunavyotaka,na mwisho mtu anaamua kufunga biashara kisa tu biashara yake haijaenda anavyotaka yeye (makosa hayo) biashara ukiona haiendi ulivyotaka basi iendeshe inavyotaka kuna mambo mawili tusichanganye.

1. Biashara kwenda unavyotaka
2. Biashara kwenda inavyotaka

Leo nataka tuongelee no.2 biashara kwenda inavyotaka, Idea zetu zimeshafeli tulitaka kufungua mama ntilie tuuze vyakula vyote lakini matokeo wateja wanakuja asubuhi tu kunywa chai ikifka mchana hamna mteja,usiku hamna mteja.. (usiseme biashara mbaya) si kweli.

Ukisema biashara mbaya kisa wateja wa chakula hawaji maana yake unataka kuifunga hiyo biashara kwasababu "haijaenda unavyotaka" ukishaona biashara imegoma kwenda unavyotaka sasa tuje PLAN B, Tuifanye biashara hiyo hiyo ya mama ntilie kulingana na "biashara inavyotaka" sio unavyotaka wewe.

Tena tunaifanya biashara hiyo hiyo eneo hilo hilo bila kuhama wala kusogea kwenda popote pale,Tunafanyaje sasa?!

Biashara yetu tulitaka iuze asubuhi mchana jioni,imekataa matokeo yake inauza asubuhi tu...Kwa maana hiyo biashara yetu inataka Tuuze asubuhi TU. Kama ni hivyo sasa tunachofanya na tumeshalijua hilo ni kukomaaa na Asubuhi kwa nguvu zote.. Mchana na usiku si kwamba hutopika La hasha! kupika utapika lakn utapunguza kipimo,Kuna haja gani ya kupika Wali kilo 4 na bado hauishi? tunapika kilo 1 tu mchana na usiku kilo 1, kwisha.

wasipomaliza hata hiyo kilo tunapika Nusu kilo,tutaenda hvyo hata ikibidi kupka robo tutapka au hata kwa order tutapka ila hatutoacha kupika maana bado wateja wa chakula wapo,sasa basi baada ya kupunguza kipimo cha wali, hela uliyokua unaipotezea kwenye wali na makorokoro mengine ya chakula Tunaileta ASUBUHI.

Yes biashara yetu si inataka tupike asubuhi sana,tunachofanya ni kukomaaa na asubuhi Kama ulikua unapka chapati tu na chai,tunaongeza mtori na uji na supu, Kwakua asubuhi ndio kuna JAM sana tunaongeza Mihogo ya kuchemsha na viazi mchemsho, yani Asubuhi mtu akija ofisini kwako anapata SUPER BREAKFAST.

vile vilivyokua hamna asubuhi Ongeza,Kaanga mayai asubuhi,chemsha mayai asubuhi, Hela ya kununua mchele kilo 4 umeipunguza mchana unaileta asubuhi kwahyo ongeza vitu tofauti tofauti ili uweze kupata super profit, asubuhi ikiiisha utajikuta una faida ile ile ambayo ulikua ukiilenga kama ungeuza asubuhi mchana na usiku ila utaipata kwa asubuhi TU... kwahyo waliodhani utafunga Watasubiri sanaaaa...

Una DUKA LA COMPUTER
Mimi ni mfano hai acha niwape kidogo hii,unajua unapokua IT halafu huna hata duka la vifaa vinavyohusiana na IT huo ni ushubwada,unaitiwa kazi ukafaye vifaa unaenda nunua maduka ya watu halafu vifaa vyenyewe ni vidogo vidogo unavimudu,Basi bana nikaonaga ni ujinga nikasema acha nifungue duka la computer na vifaa vyake.

Target yangu niuze computer kwa sana maisha yaende mana nilikua napata tenda ofisi inahtaji pc 5 za cpu,pc 10 za monitor nikachoka kuwaungisha watu nikaleta ili tenda zikija nakula hela kote kote... Maisha yakawa yanaenda hivyo.

Sasa biashara zikanitinga,mambo ya IT nikayaweka pembeni nikaingia kuuza chipsi na maandazi na vibiashara vingine, duka likawa bado lipo lakini ila wateja wa computer sina,duka kwa miezi miwili unauza laptop 1 au cpu 1 hapo kati kati kinachouzika sana ni Vifa vya computer na vifaa vinavyouzika sana ni mouse na keyboard,Duka kubwaaaa ila linaendeshwa kwa faida ya mouse na Keyboard... (nikaona huu ujinga)

Sinaga option yakufunga biashara na nikifanya hivyo hapo jua ni kweli nimeshajaribu mbinu zote zikagoma,basi baada yakuona Kinachouzika sana ni keyboard na mouse,nikaona nikomae humo humo kwenye keyboard na mouse.

Nikiuza Laptop siendi fata tena laptop nafata mizigo tofauti ya keyboard,ntaleta multmedia keyboards,Game Keyboards,Za kawaida,wireless,wired zotee zipo, Nikaleta mouse pia zoteee nikajaza Duka nikalibakisha na Laptop za kulindia Heshima na hadhi ya ofisi tu..

Duka likageuka la mouse na Keyboard,hiyo haitoshi nikaongeza na bango pale juu nikaandika MR.KEYBOARD nikakomaa na vinavyotoka ofisini,hakika faida nili iona maana kila mteja na anaejua duka langu akiwaza mouse anawaza kuja kwangu,akiwaza keyboard anawaza kuja kwangu,nikajulikana kwa sifa hiyo... lakini duka halikuaga la keyboard na mouse ni duka la computer na lilijulikana hivyo.

lakini kuna faida gani kujaza ma computer ya gharama wakati hayaingizi pesa,hatufanyi biashara ili tuonekane ila tunafanya ili tupate faida,Biashara yangu haikwenda nilivyotaka,ikabidi ni iendeshe inavyotaka yenyewe,wao si wanataka keyboard na mouse basi acha niende wanavyotaka wao,hivyo ndio biashara inavyotakiwa kwenda.

Una TIGO PESA NA MPESA
Unafanya miamala yote lakini wateja wako 90% ni wa tigo pesa, usikubali wateja wa airtel/halopesa wakumalizie cash,umeshajua wateja wako wengi n wa tigo pesa hakikisha pesa yako yote umewaekea wateja wako wa tigo pesa, akija mteja wa halopesa au airtel money kama unajiona una laki 3 mkononi halafu anakuja mteja wa airtel anakwambia "naomba kutoa laki mbili" usimruhusu,mkatalie mwambie huna cash.

Hudumia wateja wa tigopesa sana maana ndio walio wengi,usije ukajikuta huna cash hata sh kumi halafu float halopesa ina mihela kibao, mteja wa tigo anakuja anakosa huduma,usiruhusu hilo litokee. Komaa na kinachotoka na jihakikishie unapata faida zaidi kuptia hapo panapotoka zaidi.

Usitapanye pesa sehemu huna uhakika,umeshajua biashara yangu wateja wengi ni wa mtandao flani basi jiimarishe upande huo TU maana ndio penye faida.

Kila biashara tunayofanya lazima kuna kitu kinatoka sanaaaaa, basi kiangalie hicho kitu na kifanye kwa ubora zaidi na zaidi yawezekana kikakutoa kuliko hivyo vikubwa ulivyokua ukiviwaza mwanzo, usione haya mabiashara makubwa makubwa ukafikri wanapata faida sana kuptia hayo mabiashara,si kweli kama ufikiriavyo.

Unaweza ukaona showroom ina magari kibao kila ukipta unayaona magari yale yale mwezi mzima ushawahi jiuliza wana survive vipi? ukute ile showroom inaendeshwa na faida ya kuagiza spear za magari tu, kuptia faida za spear na vtu vdg vdg showroom ina dunda...

sasa wewe kaige na wewe fungua showroom ulete ma range rover ma ist uhisi unamkomoa jamaa uone kitakachokukuta,Biashara unatakiwa ukomae na kinachotoka sana kivalie njuga hakikisha unakisimamia mpk kikutoe.

Kufunga biashara iwe option ya mwisho kbsa kbsa maana kweli kuna sehemu sijui zimelogwa yani hata uwauzie mchele klo jero Hawanunui asee, yani hata useme ufanye nn wao wamekaa tu kuna sehemu za hvyo kwahyo ukiona ushajarbu option zote ikagoma Jikatae hama hilo eneo kabla hujala mtaji.

Acha kuogopa watakuchukuliaje.

Mtu ni msusi, anasuka mitindo yote ila wateja wake wengi ni wa twende kilioni,anasuka twende kilioni 2000 mtu akikaa chini anamsuka ndani ya nusu saa mpk dk 45 kamaliza,ana wateja wa namna hyo kwa siku zaidi ya 10.

Ajabu ni kwamba anatokea siku mteja anataka kusuka Vitunguuu, au anakuja na nywele zake huko zina midawa zina teleza konokono akasome ukipga hesabu za kumsuka ni lazima uchukue sio chini ya masaa 6 mpk siku nzima, Faida ukimaliza kumsuka ni 15,000 to 20, 000.

Unamkubali aje asuke unasahau wateja wako wengi ni wale wa twende kilioni, akija wa kwanza anakukuta una msuka mtu,wapili hvyo hvyo,watatu hvyo hvyo, wanakuja wateja wa misuko ya 2000 wengi unawakosa kisa kugandana na msuko faida kubwa,mteja wa twende kilioni akija anaweza akataka kuosha nywele kwanza kisha ndio umsuke,unapata faida ya kuosha na kusuka,anakuja mwingine anataka tu kubanwa style, nk nk

unakosa hela zote kwa sababu ya msuko m1,unarudi home unasema biashara mbaya wakat ni wewe mwenyewe umejisababishia biashara mbaya,mteja akija kusuka msuko wake unaona huu akikaa sasa hv kuinuka ni mpk wakati nafunga...Mkatae. Umekuja kazini kufanya biashara na sio kuonea mtu huruma, mwambie hutoweza msuka Komaa na buku mbili mbili zako za twende kilioni kufka jion ukijumlisha za kuosha,kusuka unajikuta na mpunga mrefu tu.

Kila mahali kupo hivyo hakuna biashara isiyo na kitu kinachotoka zaidi, basi kama ni hivyo ni kazi yako kuhakikisha unawaridhisha wateja wa hiyo bidhaa/huduma.

Ukienda k.koo unakuta duka linauza simu za nokia ya tochi na viswaswadu tuuuuu,hv unafikiri kashndwa uza smartphone au simu kubwa? mtaji anao ila kaamua kukomaaaa na kinachotoka zaidi,hata wewe anza leo Komaaa na kinachotoka zaidi acha kupoteza pesa kila siku kwa kujipa matumaini hewa. Sijui kama nimeeleweka leo.

Naishia hapo kwa mliopata kitu Asanteni kwa wale ndugu zangu wengine "wapinzani" kwa kila jambo Najua mnanijua huwa siwajibu hata kwa bahati mbaya kwahyo wote karibuni kukosoa na kuongezea palipopungua.
Mkuu uzidi kubarikiwa zaidi katika utafutaji wako, asante sana kwa ujumbe mzuri.
 
Kwenye swala la Tigopesa usi mkatalie mteja ndugu....

Mteja naweza kua amekataliwa uko alipotoka pia kumuhudumia ni kumuakikshia huduma na atakua mteja wako zaid.... Hasa kwa mitandao isiyokuwa na wateja wengi....

Mfn... Nilianza. Na kamishen ya Halotel 15000 Lakin baada ya miezi 6 nkawa napokea 90k kwa mtaji ule ule waku unga unga mpaka kuna watu wanashangaa....

Kwenye Biashara hii ya kifedha akikisha unatafuta mawakala wakuu wengi wale wa online maana unaweza mtumia ya tigo akakuekea Voda, na wale wanao tembeza cash na float mitandao yote....
Pia unakua na ukaribu na majiran zako(washindan wako) na ata mawakal wa mbal ili mbadilishane cash na float au float kwa float....
Umeongea ukweli kwani kwenye huduma hizi bila kuwa na marafiki unao fanya nao kazi kiukweli huduma itakuwa ngumu sana
 
Nakomaa na kukopesha fedha. Naona biashara inasonga vizuri.

ikifika milioni moja nasitisha huduma naanza biashara ya kunipa faida ya 30,000 kwa siku kwa mtaji wa milioni 1
 
Back
Top Bottom