Kohler utatufanya wana wa Arusha tuichukie CHADEMA

Jasho la Damu

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
956
120
Sitaisahau Jan, 5 nilipokoswa koswa na Risasi za moto, Mabomu ya machozi na Virungu vya FFU nilipokuwa kwenye Maandamano ya kupinga Uchaguzi batili wa Meya wa Arusha. Sitaisahau pia ile siku niliyoacha shughuli zangu zote na kwenda kwenye mazishi ya tulioamini ni mashujaa waliokufa wakitetea haki ya wananchi wa Arusha. Tuliimba nyimbo nyingi za kishujaa bila kujali manyunyu ya mvua yaliyokuwa yakitudondokea na kufuatia na jua kali likituchoma. Tulikusanyika kuanzia saa mbili asubui lkn viongozi
 
Kwa hiyo wewe ulikuwa hutaki mwafaka upatikane!!basi kama ni hivyo basi wewe ni shetani na inabidi uogopwe kama ugonjwa wa ukoma!!
 
walifika saa nane mchana huku tukiwa na shauku kubwa ya kutoa heshima ya mwisho kwa mashujaa wetu. Walipanda jukwaani viongozi mbali mbali wa chama na dini wakituhamasisha hatutaacha kuandamana mpaka uchaguzi urudiwe, nasi tulishangilia tukiamini saa ya ukombozi imefika. Wengine walidiriki kusema ni Heri kufa ukiwa umesimama kwa miguu yako kuliko kuishi miaka mingi ukiwa umepiga magoti. Leo inasikitisha kuona Cdm wakikubali matokeo kwa kafara za wana Arusha coz wameshauriwa na KOHLER???!.
 
Mkuu kwa iyo we ulishanoa panga na mkuki ili vita iendelee au? Unawashauri nini wakenya na waziri mkuu wao mpya? Au tsvangrai na mugabe pale zbambwe? Kweli nimeamini kuna watu amani kwao si kitu.
 
Nasikitika sana kuona jinsi wanadamu tunavyoshabikia njia za kibabe katika kudai tunachofikiri ni haki ilihali njia za kiungwana zipo!
 
Sitaisahau Jan, 5 nilipokoswa koswa na Risasi za moto, Mabomu ya machozi na Virungu vya FFU nilipokuwa kwenye Maandamano ya kupinga Uchaguzi batili wa Meya wa Arusha. Sitaisahau pia ile siku niliyoacha shughuli zangu zote na kwenda kwenye mazishi ya tulioamini ni mashujaa waliokufa wakitetea haki ya wananchi wa Arusha.
Tuliimba nyimbo nyingi za kishujaa bila kujali manyunyu ya mvua yaliyokuwa yakitudondokea na kufuatia na jua kali likituchoma.
Tulikusanyika kuanzia saa mbili asubui lkn viongozi

Wacha fix za kijiweni wewe jua kali likuchome na wakati huo huo mvua ikunyee manyunyu yake?
 
hujaeleweka....

Hata sahau wanasiasa walivyotumia damu za wanaarusha kufanikisha malengo yao kisiasa kwani hujui kuwa yale maandamano yalikuwa yanapinga uchaguzi batili uliomweka meya wa ccm madarakani na dhamira ilikuwa uchaguzi urudiwe? ila kwa kuwa imejulikana jamaa walikuwa wanakipigia jaramba kiti cha umea na uongozi wamefunga ndoa "mwafaka" hakuna cha uchaguzi kurudiwa wala nini walie tu. Pipooooozzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz
 
walifika saa nane mchana huku tukiwa na shauku kubwa ya kutoa heshima ya mwisho kwa mashujaa wetu. Walipanda jukwaani viongozi mbali mbali wa chama na dini wakituhamasisha hatutaacha kuandamana mpaka uchaguzi urudiwe, nasi tulishangilia tukiamini saa ya ukombozi imefika. Wengine walidiriki kusema ni Heri kufa ukiwa umesimama kwa miguu yako kuliko kuishi miaka mingi ukiwa umepiga magoti. Leo inasikitisha kuona Cdm wakikubali matokeo kwa kafara za wana Arusha coz wameshauriwa na KOHLER???!.

Mwanaharakati pole kwa memory hiyo but you must understand that "NOT EVERYTHING IT IS AS IT SEEMS TO BE". Kuna wakati inabidi ukubaliane na hali isiyokurithisha ili kuepuka athari za muda mrefu kwa jamii na kwa maendeleo. Mwenyewe sikupenda hali hii itokee lakini pia sikuwahi kufikiri watawala watakubali kuwa walikosea, siyo ccm hii wala serikali hii. For the sake of Arusha today and future kulikua na ulazima wa muafaka. Kilichotokea ni step katika mabadiliko yajayo. MABADILIKO NA MAISHA YETU HAYAISHII KWENYE UMEYA WE MUST GO ON, MUAFAKA HUU NI MSINGI WA MABADILIKO YAJAYO. CDM WAWATUMIKIE WANANCHI WA ARUSHA WALIOWACHAGUA MIAKA MITANO ISIISHIE KWENYE KUGOMBEA UMEA.
THAT'S POLITICS.
 
Sitaisahau Jan, 5 nilipokoswa koswa na Risasi za moto, Mabomu ya machozi na Virungu vya FFU nilipokuwa kwenye Maandamano ya kupinga Uchaguzi batili wa Meya wa Arusha. Sitaisahau pia ile siku niliyoacha shughuli zangu zote na kwenda kwenye mazishi ya tulioamini ni mashujaa waliokufa wakitetea haki ya wananchi wa Arusha. Tuliimba nyimbo nyingi za kishujaa bila kujali manyunyu ya mvua yaliyokuwa yakitudondokea na kufuatia na jua kali likituchoma. Tulikusanyika kuanzia saa mbili asubui lkn viongozi

mheshimiwa, ustaarabu wa mtu au chama pia hupimwa katika uwezo wa kujadiliana, kusamehe na kusahau. Ingekuwa si hivyo South Africa leo ingekuwa bado haikaliki. lakni Mandela na wote waliosota Robin Island gerezan walikubali kujadiliana, kusamehe na kusahau yooooooote na matokeo yake ndiyo hiyo bondeni (RSA) ambayo leo inasitawi! Au mwenzetu wewe ni wa jino kwa joni???
 
Mashujaa wetu kama hawa tunawaangusha jamani mkessssssssss.jpg
 
Gm32
Ahsante kwa fikra na busara zako hakika wewe umekomaa kimawazo na fikra pia lkn pia ni lazima tuwaeleze Wanachama na wapenzi wa Cdm sio kila jambo litalokalofanywa na viongozi wa chama litakuwa na positive emotional kwa wananchi. Ingekuwa vyema na busara kama Viongozi wa Cdm wangeleta Terms of Agreement kwa wananchi wa Arusha kabla ya kukubali huo mwafaka coz wananchi walidai uchaguzi urudiwe na si mgawanyo wa madaraka.
 
Mkuu kwa iyo we ulishanoa panga na mkuki ili vita iendelee au? Unawashauri nini wakenya na waziri mkuu wao mpya? Au tsvangrai na mugabe pale zbambwe? Kweli nimeamini kuna watu amani kwao si kitu.
Amani bila haki itatoka wapi? Je unataka kutuambia kuwa maandamano yale hayakustahili coz yalivunja amani?
 
Kwa hiyo wewe ulikuwa hutaki mwafaka upatikane!!basi kama ni hivyo basi wewe ni shetani na inabidi uogopwe kama ugonjwa wa ukoma!!
Kama ni hivyo basi wa kwanza kuogopwa ni viongozi wa Cdm waliotulaghai na kutuingiza mkenge wa kwenye maandamano wakati walikuwa wanaweza kufikia mwafaka kwa kugawana madaraka tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom