Koh Koh Koh.. Mbona Rais Samia Kama Kayaona ya Magufuli?

jumba bovu ni pamoja na urais wake. majizi yamemuua rais wetu halafu bi tozo akaangushiwa jumba bovu la urais na asivyojielewa kaanza kunogewa
 
Ukiwa Rais wa Taifa hili ukilala unatakiwa uwaze sehemu hizi bandari,wizara fedha ,wizara madini Sasa yeye amelala fofofo anasubiri report kuletewa Samia ni Kama mgeni kwenye nyumba hafai hafai hafai kabisa.

Angejikita kwenye kurejelea mchakato wa katiba mpya. Mengine yakafuata mkondo wake. Hata kama angekuja kustaafu angeondoka na legacy ya kudumu.

Kwa anavyokwenda jumba lote bovu litakuja kumhusu.
 
Mama hukumu aliyotoa jana ilikuwa ndogo sana, palepale alipaswa afukuze kazi waziri mhusika wa hiyo bandari, mkurugenzi wa bandari na management yooote....jeshi liingie kazini kwa muda...on the spot..

Wahusika weekend hii walipaswa wawe keko mahabusu...j3 mahakamani uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na mauaji kwa watanzania masikini.....wakisota jela mahabusu kama miaka kumi na mali zao zote ziwe mufilisi, baada ya 10yrs wanamalizwa tu huko kimyakimya...

Kwa sasa fukuza kazi wafanyakazi wooote wa bandari usiache hata mmoja...kuanzia juu mpaka mfagiaji wote rudisha mtaani...aazeni upya kuajili wapo watanzania wengi sana huku mtaani na bahasha zao.....wote wenye vyeo ya kati na jui muwafilisi haraka..
 
jumba bovu ni pamoja na urais wake. majizi yamemuua rais wetu halafu bi tozo akaangushiwa jumba bovu la urais na asivyojielewa kaanza kunogewa
Ukiitwa uthibitishe hizo allegation utaeza? ukimbiwa upeleke concrete evidence utaweza?
 
Kweli jamii forum ya zama hizi imechoka sana. Yaani Mzee Mwanakijiji ndio wakuja na mada nyepesi nyepesi za namna hii?

Yaani hawezi kuandika tena mada mpaka amuingize marehemu Magufuli na kumpamba?

Okay, turudi kwenye mada, bado sijapata logic yako ni nini?
Unataka kusema mama kwa sasa anamuiga Magufuli hivyo tumuunge mkono au tumkosoe?

Sote tunajua, tatizo la bandari ni tatizo la kimfumo (limetengenezwa na linalindwa na serikali ya CCM) na liko chini ya usimamizi wa mamlaka ya rais kwa kuwa karibu theluthi moja ya mapato ya nchi ya kila mwezi ya TRA yanapitia pale. Na sote tunakumbuka lilikuwa ni eneo la mahususi la kufanyia siasa za kiusanii katika utawala wa Magufuli (kumbuka issue za makontena ya makinikia, kuokotwa vichwa vya treni na mamia ya magari yasiyokuwa na wenyewe nk, na waokotaji walikuwa ni Magufuli na Majaliwa huku wakiwa wamezungukwa na kamera za kila kituo cha habari hapa Tz chini ya mwamvuli wa ziara za kushtukiza!)
Nakubaliana .
Magufuli alikuwa na usanii wa kupenda sifa na kuabudiwa.
Na hilo halina maana kuwa wananchi wa kipato cha chini hawakuwepo.
Wapo na wataendelea kuwepo.

Mama Samia aendelee kufufua uchumi na Bandari ya Bagamoyo Economic Zone.
 
Kila siku bandari bandari wakati watanzania wanachanjwa tozo kufanya uwekezaji hapo halafu mijitu inafanya ujinga ujinga tu.... Watanzani wako wengi sana mtaani huku hawana kazi, fukuza kazi hao wafanyakazi wa bandari wooote usiache hata mmoja...tuanze upya kwa kuajili vijana wengine...na kufanya temporary outsourcing hata kwa Maersky warun hiyo bandari kwa 5yrs watu wetu wajifunze...
 
Kweli jamii forum ya zama hizi imechoka sana. Yaani Mzee Mwanakijiji ndio wakuja na mada nyepesi nyepesi za namna hii?

Yaani hawezi kuandika tena mada mpaka amuingize marehemu Magufuli na kumpamba?

Okay, turudi kwenye mada, bado sijapata logic yako ni nini?
Unataka kusema mama kwa sasa anamuiga Magufuli hivyo tumuunge mkono au tumkosoe?

Sote tunajua, tatizo la bandari ni tatizo la kimfumo (limetengenezwa na linalindwa na serikali ya CCM) na liko chini ya usimamizi wa mamlaka ya rais kwa kuwa karibu theluthi moja ya mapato ya nchi ya kila mwezi ya TRA yanapitia pale. Na sote tunakumbuka lilikuwa ni eneo la mahususi la kufanyia siasa za kiusanii katika utawala wa Magufuli (kumbuka issue za makontena ya makinikia, kuokotwa vichwa vya treni na mamia ya magari yasiyokuwa na wenyewe nk, na waokotaji walikuwa ni Magufuli na Majaliwa huku wakiwa wamezungukwa na kamera za kila kituo cha habari hapa Tz chini ya mwamvuli wa ziara za kushtukiza!)
Naona tatizo lako kutajwa kwa Magufuli umechefukwa!
Hoja ipo wazi,mleta mada amejaribu kulinganisha tu maamuzi ya jana na aliokuwa akifanya Magufuli,hapo ndipo pa kujadili.
Anatajwa Hitler mpaka leo na kuna watu bado wanaamini katika maono yake itakua Magufuli?
Chuki zingine mzipotezee,mnaweza kujikuta mnapata kiungulia sugu shauri ya chuki kwa aliekufa
 
Tangu misingi ya Tanzania inawekwa watawala wote ni CCM, Tanzania haijawahi kutawaliwa na chama kingine zaidi ya CCM.

Cha ajabu ni kwamba kila kiongozi anaeingia kwenye uongozi anaukuta ufisadi na atajifanya kuumaliza kwa kutimuatimua na kuweka wa kwake.

Lakini pamoja na yote hayo ufisadi utaendelea hata kwa atakayekuja ufisadi utakuwepo na atauacha.

Sijui ndiokusema kuwa CCM wanapobadilishana uongozi wanabadilishana na mafisadi pia, kwa kila kiongozi anayeingia madarakani huja na mafisadi wake au ufisadi umegeuzwa kama kiki ya kujitafutia umaarufu?.
 
Sijui ni mimi tu, macho yangu au masikio yangu? Huku Bandari mbona kama kunaumiza kichwa sana Marais? Rais Samia jana kazungumza kama Magufuli, Kachukua hatua za papo hapo kama enzi za Magu na anajitangaza kusimama na wananchi kama Magu alivyokuwa anajitangaza kusimama na wanyonge. SSa anajitengenezea maadui wa ndani? Ameanza kuona nini? Maana maneno yake ukiyawekea sauti ya Magufuli hutaweza juona tofauti...

Waliomuunga mkono na kusita wapate nguvu mpya?
We mzee acha kuturudisha Misri. Wacha Mama achape kazi.
 
Kweli jamii forum ya zama hizi imechoka sana. Yaani Mzee Mwanakijiji ndio wakuja na mada nyepesi nyepesi za namna hii?

Yaani hawezi kuandika tena mada mpaka amuingize marehemu Magufuli na kumpamba?

Okay, turudi kwenye mada, bado sijapata logic yako ni nini?
Unataka kusema mama kwa sasa anamuiga Magufuli hivyo tumuunge mkono au tumkosoe?

Sote tunajua, tatizo la bandari ni tatizo la kimfumo (limetengenezwa na linalindwa na serikali ya CCM) na liko chini ya usimamizi wa mamlaka ya rais kwa kuwa karibu theluthi moja ya mapato ya nchi ya kila mwezi ya TRA yanapitia pale. Na sote tunakumbuka lilikuwa ni eneo la mahususi la kufanyia siasa za kiusanii katika utawala wa Magufuli (kumbuka issue za makontena ya makinikia, kuokotwa vichwa vya treni na mamia ya magari yasiyokuwa na wenyewe nk, na waokotaji walikuwa ni Magufuli na Majaliwa huku wakiwa wamezungukwa na kamera za kila kituo cha habari hapa Tz chini ya mwamvuli wa ziara za kushtukiza!)
You nailed it
 
Wanalazimisha mno kila kitu sifa apewe Magufuli...
As if kabla ya Magufuli Taifa halikuwepo kabisa.. ..

Anayopitia Samia hata Mwinyi alipitia..
Enzi ya Mwinyi ilikuwa kila kitu Nyerere..
Utasema Nyerere aliacha nchi imeendelea kama Ulaya..
Nongwa Tu hakuna lolote
Enzi za Mwinyi haikuwa kila kitu Nyerere.

Mwinyi alitenda kwa maono yake tukampenda ila alikuwa anmheshimu Mwalimu kwani hata pale alipomwingilia mzee Ruksa alikaa kimya.
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom