Koh Koh Koh.. Mbona Rais Samia Kama Kayaona ya Magufuli?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Sijui ni mimi tu, macho yangu au masikio yangu? Huku Bandari mbona kama kunaumiza kichwa sana Marais?

Rais Samia jana kazungumza kama Magufuli, Kachukua hatua za papo hapo kama enzi za Magu na anajitangaza kusimama na wananchi kama Magu alivyokuwa anajitangaza kusimama na wanyonge. Sasa anajitengenezea maadui wa ndani? Ameanza kuona nini? Maana maneno yake ukiyawekea sauti ya Magufuli hutaweza juona tofauti...

Waliomuunga mkono na kusita wapate nguvu mpya?
 
Duh...!.
P

Duh...ninapokaa kimya nina sababu...
Mkuu Mzee Mwanakijiji , kunapotokea injustices, aggression or oppression, unapokaa kimya, maana yake ni ume side na the aggressors, the oppressors to support the injustices.

Usinyamaze, keep shouting, keep writing, keep fighting. Fufua Cheche za Fikra, mwamshe Lula wa Ndali Mwananzela na wewe mwenyewe Mzee Mwanakijiji rejea ulingoni kidigitali zaidi kuisaidia nchi yako.

P
 
Aisee, Magufuli alishakufa mzee.

Naona umeshindwa kabisa kuzoea.

Kwahiyo sasa unataka kusemaje?

Wanalazimisha mno kila kitu sifa apewe Magufuli...
As if kabla ya Magufuli Taifa halikuwepo kabisa.. ..

Anayopitia Samia hata Mwinyi alipitia..
Enzi ya Mwinyi ilikuwa kila kitu Nyerere..
Utasema Nyerere aliacha nchi imeendelea kama Ulaya..
Nongwa Tu hakuna lolote
 
Kweli jamii forum ya zama hizi imechoka sana. Yaani Mzee Mwanakijiji ndio wakuja na mada nyepesi nyepesi za namna hii?

Yaani hawezi kuandika tena mada mpaka amuingize marehemu Magufuli na kumpamba?

Okay, turudi kwenye mada, bado sijapata logic yako ni nini?
Unataka kusema mama kwa sasa anamuiga Magufuli hivyo tumuunge mkono au tumkosoe?

Sote tunajua, tatizo la bandari ni tatizo la kimfumo (limetengenezwa na linalindwa na serikali ya CCM) na liko chini ya usimamizi wa mamlaka ya rais kwa kuwa karibu theluthi moja ya mapato ya nchi ya kila mwezi ya TRA yanapitia pale. Na sote tunakumbuka lilikuwa ni eneo la mahususi la kufanyia siasa za kiusanii katika utawala wa Magufuli (kumbuka issue za makontena ya makinikia, kuokotwa vichwa vya treni na mamia ya magari yasiyokuwa na wenyewe nk, na waokotaji walikuwa ni Magufuli na Majaliwa huku wakiwa wamezungukwa na kamera za kila kituo cha habari hapa Tz chini ya mwamvuli wa ziara za kushtukiza!)
 
Sijui ni mimi tu, macho yangu au masikio yangu? Huku Bandari mbona kama kunaumiza kichwa sana Marais? Rais Samia jana kazungumza kama Magufuli, Kachukua hatua za papo hapo kama enzi za Magu na anajitangaza kusimama na wananchi kama Magu alivyokuwa anajitangaza kusimama na wanyonge. SSa anajitengenezea maadui wa ndani? Ameanza kuona nini? Maana maneno yake ukiyawekea sauti ya Magufuli hutaweza juona tofauti...

Waliomuunga mkono na kusita wapate nguvu mpya?

Uongozi si vita. Angejikita katika haki zilizozikwa awamu ya tano ilikuwa inatosha sana.

Taifa lingepona, tungekuwa wamoja, tukapaa kiuchumi na mi 5 mingine ya haki ingemhusu.
 
Mambo ni moto mkuu
Screenshot_20211204-164758_Opera%20Mini.jpg
 
Ukiwa Rais wa Taifa hili ukilala unatakiwa uwaze sehemu hizi bandari,wizara fedha ,wizara madini Sasa yeye amelala fofofo anasubiri report kuletewa Samia ni Kama mgeni kwenye nyumba hafai hafai hafai kabisa.ndio maana JPM akilala akipata maruweruwe usiku anaamukia bandarini kimyakimya.
 
Uongozi si vita. Angejikita katika haki zilizozikwa awamu ya tano ilikuwa inatosha sana.

Taifa lingepona, tungekuwa wamoja, tukapaa kiuchumi na mi 5 mingine ya haki ingemhusu.
Naona unabwabwaja tu utapaaje kiumi ndugi ili halia huna pesa ya kuunedesha nchi kuggaramikia mega project .huku watu wakijipigia tu mahela hapo bandarini na ukwasi wa kutisha ili kule jikijijin hupeleki hata panadol

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli jamii forum ya zama hizi imechoka sana. Yaani Mzee Mwanakijiji ndio wakuja na mada nyepesi nyepesi za namna hii?

Yaani hawezi kuandika tena mada mpaka amuingize marehemu Magufuli na kumpamba?

Okay, turudi kwenye mada, bado sijapata logic yako ni nini?
Unataka kusema mama kwa sasa anamuiga Magufuli hivyo tumuunge mkono au tumkosoe?

Sote tunajua, tatizo la bandari ni tatizo la kimfumo (limetengenezwa na linalindwa na serikali ya CCM) na liko chini ya usimamizi wa mamlaka ya rais kwa kuwa karibu theluthi moja ya mapato ya nchi ya kila mwezi ya TRA yanapitia pale. Na sote tunakumbuka lilikuwa ni eneo la mahususi la kufanyia siasa za kiusanii katika utawala wa Magufuli (kumbuka issue za makontena ya makinikia, kuokotwa vichwa vya treni na mamia ya magari yasiyokuwa na wenyewe nk, na waokotaji walikuwa ni Magufuli na Majaliwa huku wakiwa wamezungukwa na kamera za kila kituo cha habari hapa Tz chini ya mwamvuli wa ziara za kushtukiza!)
Aisee Umepiga penyewe,Mwendazake alitufanya wajinga ...halafu eti bado tunaye Majaliwa😧😧
Mwanakijiji is no longer!
 
Weka wanajeshi bandarini kwisha habari
Sijui ni mimi tu, macho yangu au masikio yangu? Huku Bandari mbona kama kunaumiza kichwa sana Marais? Rais Samia jana kazungumza kama Magufuli, Kachukua hatua za papo hapo kama enzi za Magu na anajitangaza kusimama na wananchi kama Magu alivyokuwa anajitangaza kusimama na wanyonge. SSa anajitengenezea maadui wa ndani? Ameanza kuona nini? Maana maneno yake ukiyawekea sauti ya Magufuli hutaweza juona tofauti...

Waliomuunga mkono na kusita wapate nguvu mpya?
 
Wanalazimisha mno kila kitu sifa apewe Magufuli...
As if kabla ya Magufuli Taifa halikuwepo kabisa.. ..

Anayopitia Samia hata Mwinyi alipitia..
Enzi ya Mwinyi ilikuwa kila kitu Nyerere..
Utasema Nyerere aliacha nchi imeendelea kama Ulaya..
Nongwa Tu hakuna lolote
Kabisa mkuu.wanachotaka Ni kulazimisha kuwa waliopita hakuna chochote walichofanya au Kama tulikuwa katika ukoloni kabla ya awamu ya tano.
 
Back
Top Bottom