Kofi Annan, Luis Ocampo na Thabo Mbeki waombwe kusuluhisha vyama vya siasa Tanzania

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,017
Hali inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyokwenda.

DAMU imeshamwagika.

Watu wamepata VILEMA.

Wazee wa hapa nchini, pamoja na viongozi wa dini, wameshindwa kutuliza joto la kisiasa.

Umefika wakati wa kutafuta watu wazito wenye busara toka nje ya nchi kuja kusuluhisha.

Ni vizuri tukatafuta usuluhishi mapema kabla mambo hayajaharibika kabisa au wakati tumesambaratika.

Nadhani Mzee Koffi Annan, Jaji Luis Moreno Ocampo, na Mzee Thabo Mbeki, wanaweza kutusaidia ktk hili.
 
Hapa tuna kazi kweli kama MTU mwenye kalala macho anakomaa na test mwenyewe ka graduate anaitikia ndio Mzee kuna walakin hapa
 
Wewe mzee JokaKuu umeanza kuchanganyikiwa, hawana muda mchafu hao wa kuanza kusuluhisha “kujiliza” kwenu. Tanzania hakuna mgogoro wa kisiasa wala dalili ya mgogoro wa kisiasa. Rafiki wa CDM Kenyata huku akipewa sifa kede kede na CDM ameua zaidi ya watu 100. Hakuna aliyemgusa wala atakayemgusa.

Hizi kelele zote mwisho ni 2020, mkishashindwa ubunge mtakuwa kama NCCR Mageuzi, na CCM walivyo na fitna wataanza kukipa promo chama kingine cha upinzani. Nyie wazee wa CDM ni wanafiki sana, saivi mnajaribu kila njia kuleta hali ya taharuki, uzuri wa JPM hacheki na kima, ukifanya upuuzi anakutandika nyundo tu.
 
..hali inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyokwenda.

..DAMU imeshamwagika.

..watu wamepata VILEMA.

..wazee wa hapa nchini, pamoja na viongozi wa dini, wameshindwa kutuliza joto la kisiasa.

..Umefika wakati wa kutafuta watu wazito wenye busara toka nje ya nchi kuja kusuluhisha.

..Ni vizuri tukatafuta usuluhishi mapema kabla mambo hayajaharibika kabisa au wakati tumesambaratika.

..Nadhani Mzee Koffi Annan, Jaji Luis Moreno Ocampo, na Mzee Thabo Mbeki, wanaweza kutusaidia ktk hili.
Kuna ugomvi gani? Ni dictatorship ya mtu mmoja! Dictator mmoja na wala siyo ugomvi wa CCM na vyama vingine!
 
..hali inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyokwenda.

..DAMU imeshamwagika.

..watu wamepata VILEMA.

..wazee wa hapa nchini, pamoja na viongozi wa dini, wameshindwa kutuliza joto la kisiasa.

..Umefika wakati wa kutafuta watu wazito wenye busara toka nje ya nchi kuja kusuluhisha.

..Ni vizuri tukatafuta usuluhishi mapema kabla mambo hayajaharibika kabisa au wakati tumesambaratika.

..Nadhani Mzee Koffi Annan, Jaji Luis Moreno Ocampo, na Mzee Thabo Mbeki, wanaweza kutusaidia ktk hili.

Kwanza kabisa calibre ya hawa watu unaozungumzia hapa si wa kuja kujadili siasa nyepesi kama hizi za Tanzania. Kabla hujafikiria hata kusuluhishwa lazima ujiulize tatizo letu lipo wapi. Je tatizolipo kwenye tafsiri ya sheria au tatizo lipo kwa watu wenyewe. Kama tatizolipo kwenye tafsiri ya sheria labda unaweza kutafuta msuluhishi, lakini tatizo letu lipo zaidi kwenye watu wenyewe- in maturity of opposition parties!!
 
Mkuu JokaKuu hakuna cha kusuluhisha kama unamaanisha usuluhisho huo unahusisha CCM!

Nasema hakuna cha kusuluhisha kwa sababu usuluhishi unahitajika pale pande mbili hasimu zote kwa pamoja zinapokuwa hazipendezwi na kinachoendelea lakini situation inakuwa beyond their control kuleta utengamano wanaouhitaji!

Kinyume chake, CCM wala hawakerwi na kinachoendelea...

Mwenyekiti wa CCM wala hakerwi kwa yanayoendelea...

Rais wa nchi wala hakerwi kwa yanayoendelea...

Viongozi kadhaa wa CCM wala hawakerwi kwa yanayoendelea...

In short, wote hawa wanayapenda na kuyashadadia yanayoendelea!

Hao ukiwaambia uwasuluhishe watakushangaa na kukukejeli kwa sababu ndani ya fikra zao ni kwamba mchezo umefika patamu! Watafurahia kila aina ya rafu wanazopiga na kuhusudu umahiri wao katika upigaji wao wa rafu za wazi!

Hao Mabwana Mkubwa uliowataja ningetamani wapatanishe Wapinzani kwa sababu ukweli ni kwamba Wapinzani hivi sasa si wamoja na sina shaka wangetamani sana wawe wamoja kv hiyo ndiyo njia pekee ya kupambana na Zimwi la Kisiasa lenye matala Lumumba na Chamwino!

Zimwi hili la kisiasa bila aibu furaha yake ni kuona fitina, chuki, husuda na uhasama vinatawala miongoni mwa majirani zake!
 
Kwanza kabisa calibre ya hawa watu unaozungumzia hapa si wa kuja kujadili siasa nyepesi kama hizi za Tanzania. Kabla hujafikiria hata kusuluhishwa lazima ujiulize tatizo letu lipo wapi. Je tatizolipo kwenye tafsiri ya sheria au tatizo lipo kwa watu wenyewe. Kama tatizolipo kwenye tafsiri ya sheria labda unaweza kutafuta msuluhishi, lakini tatizo letu lipo zaidi kwenye watu wenyewe- in maturity of opposition parties!!

..hata kama tatizo ni hicho unachoita " immaturity of opposition parties" bado naamini kuna ulazima wa wasuluhishi kuja kututatulia mgogoro tulio nao.

..kuna tatizo ambalo tusipokuwa makini linaweza kutuletea madhara makubwa huko mbeleni. Sasa it is better kutafuta msaada kabla hali haijawa mbaya zaidi.
 
Mkuu JokaKuu hakuna cha kusuluhisha kama unamaanisha usuluhisho huo unahusisha CCM!

Nasema hakuna cha kusuluhisha kwa sababu usuluhishi unahitajika pale pande mbili hasimu zote kwa pamoja zinapokuwa hazipendezwi na kinachoendelea lakini situation inakuwa beyond their control kuleta utengamano wanaouhitaji!

Kinyume chake, CCM wala hawakerwi na kinachoendelea...

Mwenyekiti wa CCM wala hakerwi kwa yanayoendelea...

Rais wa nchi wala hakerwi kwa yanayoendelea...

Viongozi kadhaa wa CCM wala hawakerwi kwa yanayoendelea...

In short, wote hawa wanayapenda na kuyashadadia yanayoendelea!

Hao ukiwaambia uwasuluhishe watakushangaa na kukukejeli kwa sababu ndani ya fikra zao ni kwamba mchezo umefika patamu! Watafurahia kila aina ya rafu wanazopiga na kuhusudu umahiri wao katika upigaji wao wa rafu za wazi!

..siamini kama ccm wote wanafurahishwa na mambo ya hovyo-hovyo yanayoendelea.

..kinachokosekana na ujasiri tu wa kuwekana sawa ktk chama chao.
 
Back
Top Bottom