Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Aliyekuwa katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Koffi Annan amekosoa mahakama ya ICC kwa kuwaacha huru viongozi wa kenya waliokabiliwa na mashtaka ya ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Annan aliyekuwa mpatanishi mkuu wa viongozi wa kenya wakati wa ghasia hizo, amesema ICC walikosea kwenye maamuzi ya uhuru wa viongozi kwani hatua hiyo imezua uwezekano wa viongozi hao kuhusika na uingiliaji wa ushahidi.
Amesema Uhuru Kenyatta na William Ruto walipaswa kuwekwa kizuizini katika mahakama hiyo hadi kesi kukamilika.
Hata hivyo maoni yake hayataathiri kesi hiyo iliyokamilika baada ya washukiwa kutopatikana na hatia,Annan ameyasema hayo kwenye gazeti moja la uingereza na amedai ICC haikuwalinda mashahidi ipasavyo.