Kodi zitokanazo na kuingiza mashine ya Kusaga Mahindi/ Grain storage Silo

muuza ubuyu

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
3,511
3,477
Habari wakuu.

Nina plan ya kuagiza mashine ya kusaga unga (complete system, 10tons/24hrs) kutoka china na nimeambiwa CIF cost to Dar ni usd 23,000.

Pia nina plan ya kuagiza system nzima ya grain storage silo yenye capacity ya 500 Tons.

Kwa wanaojua ningeomba kujua kodi zinazoambatana na kuingiza mashine hii pamoja na Grain SILO ili niweze kuona kama ninaweza ku-afford.

Kama mambo yakiwa mazuri plan yangu kutimiza hili ni mwakani 2023.

Thanks
 
Je unaagiza kama kampuni au mtu binafsi, Tanzania hutoa wigo mpana wa motisha wa kodi. hasa kwa kampuni zilizosajiliwa Katika Kanda za Usindikaji wa Bidhaa kwa Mauzo Nje ya Nchi (EPZs) na Kanda Maalum za Kiuchumi (SEZs), makampuni hupewa msamaha wa ushuru wa kuingiza mali ghafi na zana za uzalishaji viwandani

1.Kwanza sajili kampuni/ yenye mtaji (project/MRADI) Zaidi ya dola Za kimarekani laki moja (100,000 usd), sajili TRA, the National Social Security Fund (NSSF), the Occupational Safety and Health Agency (OSHA) Na Worker's Compensation Fund (WCF)
2.Tembelea Tanzania Investment Centre (TIC) wana office kila kanda watakupa tax exemption certificate kwa ajili ya mashine zako hizo
3.Tafuta Wakala wa Kupokea na Kusafirisha Mizigo(clearing and forwarding Agency) mwenye Leseni ili aweze kupokea/kukomboa bidhaa zako namkabidhi nyaraka zote ikiwemo Nyaraka za msamaha wa kodi
muuza ubuyu
 
Je unaagiza kama kampuni au mtu binafsi, Tanzania hutoa wigo mpana wa motisha wa kodi. hasa kwa kampuni zilizosajiliwa Katika Kanda za Usindikaji wa Bidhaa kwa Mauzo Nje ya Nchi (EPZs) na Kanda Maalum za Kiuchumi (SEZs), makampuni hupewa msamaha wa ushuru wa kuingiza mali ghafi na zana za uzalishaji viwandani
Capital zaidi ya US $ 100,000 kwa sisi Watanzania wa kawaida si mchezo, japo sitakata tamaa!

Asante sana mkuu kwa ufafanuzi wako mzuri! Imenipa range ya namna gani ninatakiwa ku-stretch beyond my economical comfort zone!
 
Kwahiyo pesa na kwa hali ya sasa kununua mashine ya kusaga ton 10 toka china itakula kwako.
Kwahiyo hela unaweza chonga mashine hapahapa bongo full automatic ya ton 60 kwa siku na chenji inayobaki ukaweka kwenye mahindi.
Mashine za kichina zitapunguza cost ya umeme lakin bado unaweza epuka.
Mfano ukiwa na kinu oversize ( 150mmh) na mota 55 bado unaweza piga mzigo mkubwa sana kuliko hizo unazokimbilia.
Kwangu mim kmaa unataka kwenda china kununua zile maahine kanunue maahine kubwa za ton 200 na ambazo cost inaweza fika mpaka usd 2000000
 
Asante sana mkuu kwa ushauri. Unasemaje kuhusu Silo?

Mimi ni muumini wa kutunza nafaka (grains) bila kuwekea dawa ili nihakikishe ninalinda afya za wateja wangu. Kufanikisha hili ndiyo nikaja na wazo la kuwa na grain SILO walau ya tani 500, una ushauri wowote kuhusu hili?
 
Njoo nikupe mashine yenye uwezo wa kusaga tani 16 kwa siku kwa $8000 ilitumika kidogo sana; baada ya kukosa mahindi na usimamizi thabiti ikafungiwa tu ndani.

Sifa za mashine;-

  • ina vuta mahindi/mpunga
  • Ina chekecha na kupuliza vumbi
-ina mwagia mahindi maji kwa ajili ya kukoboa
  • Ina kausha mahindi ili yakobolewe
  • Inakoboa mahindi
  • Inasaga mahindi au nafaka zingine

Ina mashine zifuatazo;-

1.Mashine ya Kuvuta mahindi na kupiliza vumbi na Motor yake
2. Mashine ya kuchekecha mahindi/nafaka na Motor yake
3. Mashine ya kuvuta na kukausha mahindi/nafaka na Motor yake
4. Mashine ya kukoboa ( MPYA ) na Motor yake
5. Mashine ya kusaga na Motor yake

Hii ukisha seti tu we unkupokea unga..iko automated
 
Asante sana mkuu, naendelea kucheki options probably ninaweza kukucheki in future!
 
Njoo nikupe mashine yenye uwezo wa kusaga tani 16 kwa siku kwa $8000 ilitumika kidogo sana; baada ya kukosa mahindi na usimamizi thabiti ikafungiwa tu ndani.

Sifa za mashine;-

  • ina vuta mahindi/mpunga
  • Ina chekecha na kupuliza vumbi
-ina mwagia mahindi maji kwa ajili ya kukoboa
  • Ina kausha mahindi ili yakobolewe
  • Inakoboa mahindi
  • Inasaga mahindi au nafaka zingine

Ina mashine zifuatazo;-

1.Mashine ya Kuvuta mahindi na kupiliza vumbi na Motor yake
2. Mashine ya kuchekecha mahindi/nafaka na Motor yake
3. Mashine ya kuvuta na kukausha mahindi/nafaka na Motor yake
4. Mashine ya kukoboa ( MPYA ) na Motor yake
5. Mashine ya kusaga na Motor yake

Hii ukisha seti tu we unkupokea unga..iko automated
Hii iko wapi?
 
1.Kwanza sajili kampuni/ yenye mtaji (project/MRADI) Zaidi ya dola Za kimarekani laki moja (100,000 usd), sajili TRA, the National Social Security Fund (NSSF), the Occupational Safety and Health Agency (OSHA) Na Worker's Compensation Fund (WCF)
Mtaji wako wote utaishia hapa. Sera na sheria zetu inabidi zibadilishwe baadhi ya mambo tuyapuuze haya ni counterproductive kwenye ujasiliamali.
 
Duh, mkuu. Inakatisha tamaa kweli make kwenye kila wazo la ujasiriamali bado itakutana na sera zinazoendana na hizi tu. Najua jamaa pia hajataja TBS, TFDA nk.

Lakini tutapambana, kwani ukikaa tu nako ni shida
 
Yes hakuna kulala. Eneo pekee lenye usumbufu kidogo ni kwenye mechanized agriculture
 
Asante sana mkuu kwa ushauri. Unasemaje kuhusu Silo?

Mimi ni muumini wa kutunza nafaka (grains) bila kuwekea dawa ili nihakikishe ninalinda afya za wateja wangu. Kufanikisha hili ndiyo nikaja na wazo la kuwa na grain SILO walau ya tani 500, una ushauri wowote kuhusu hili?
Kwa maoni yangu grain silo ndo njia rahisi na nafuu za kutunzia mazao ila kwangu mimi na uzoefu wa bidhaa na mashine za kichina ni mara mia ukatafuta fundi tu akakutengenezea hapahapa nyumbani itakuwa nafuuu zaidi
 
Nashukuru sana kwa mawazo yako, nilishawahi kuongea na Sido Moshi (walishawahi kuniuzia mashine za kusaga na kukoboa) wakaniambia hata silo wanatengeneza, ila sasa sijajua efficiency yake katika kutunza nafaka dhidi ya wadudu (sitaki kutumia madawa) na unyevu na system ya monitoring mle ndani, sema za kichina kwa kweli zina system nzuri na sophisticated japo labda durability ndo shida.

Thanks kwa ku-share experience mkuu.
 
Back
Top Bottom